Taasisi za kuimarisha utawala bora, "Oversight institutions" | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Taasisi za kuimarisha utawala bora, "Oversight institutions"

Discussion in 'KATIBA Mpya' started by PERECY, Jan 16, 2012.

 1. PERECY

  PERECY Member

  #1
  Jan 16, 2012
  Joined: Jan 11, 2012
  Messages: 29
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Wapendwa wanaJF,

  Suala la Katiba Mpya lilianza kupigiwa kelele zamani na wananchi wapenda ukweli na wenye maono akiwepo Makwaia wa KUHENGA, mwandishi wa Kitabu cha CCM NA MUSTAKABALI WA NCHI YETU, ambapo katika Sura ya 15 ameandika: KATIBA MPYA NDIYO HATMA NJEMA YA NCHI YETU.

  Mwandishi hapa amesifia utaratibu wa Rais anapomaliza kipindi chake cha miaka 10, kwa utaratibu wa Katiba anapumzika na hilo limewezekana bila kikwazo kutokea ambapo hakuna Rais mstaafu amebughudhiwa na mwenzake hata kama tetesi za ubadhirifu kuwepo. Hivyo amani hata kama ni kidogo.

  Tatizo linaonekana katika Mamlaka aliyopewa Rais ya kuteua viongozi wengi - madaraka yasiyo na vizingiti. Taasisi ya HakiElimu imethubutu kuhoji mengi katika kuboresha elimu na demokrasia (ikiwa ni sehemu ya utawala bora), iwapo ilikuja kuonekana 'inaweka vidole katika macho ya wakubwa'. Bahati mbaya sana Rais amesaini Muswada wa Marekebisho ya katiba kuwa sheria, ambapo tayari imeshalalamikiwa haitakidhi/haitafikia na kupokea maoni ya 'walaji' muhimu wa Katiba hiyo ambao ni wananchi wa kawaida kwa ujumla wao.

  Kwa kuwa hata Mwalimu Nyerere aliwahi kusema, "Kwa mamlaka haya niliyo nayo naweza kabisa nikawa dikteta....", na bado ni katika Katiba hii hii.

  Napendekeza wanaJF mtoe maoni na mapendekezo zaidi ni namna gani Katiba iumbwe ikiwa na vipengele vyenye kuwezesha uanzishaji wa Mamlaka na Taasisi huru za kusimamia utawala bora nchini. Tunahitaji kupiga hatua ya mbele zaidi, kwani suala la rushwa bado ni tatizo, uteuzi wa wakuu wa wilaya, mikoa, mawaziri, majaji, mwenyekiiti wa Tume ya Uchaguzi, mabalozi, n.k., kwa utaratibu wa sasa - unyongaji wa utawala bora ni dhahiri!

  Ni mimi mwanaJF mchanga,

  Perecy.
   
 2. doctorz

  doctorz JF-Expert Member

  #2
  Jan 16, 2012
  Joined: Aug 10, 2010
  Messages: 907
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Je tutafika?
   
 3. PERECY

  PERECY Member

  #3
  Jan 22, 2012
  Joined: Jan 11, 2012
  Messages: 29
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Wana JF:

  Salamu tena!

  Napenda niombee mjadala kuhusu Taasisi za kusimamia utawala bora ujadiliwe kwa kina, hasa nikitoa mwongozo ufuatao, baada ya kuona tangu nipendekeze, kuna mchangiaji mmoja tu amejitokeza, tena kwa kusema tu: Je, Tutafika?

  Ieleweke kuwa, miongoni mwa taasisi za kusimamia utawala bora ni: (1) Bunge na Kamati zake kama PAC, LAAC na POAC, (2) Ofisi ya Mthibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali, (NAO); (3) Mamlaka ya Usimamizi Manunuzi ya Umma, (PPRA); (4) Tume ya Maadili ya Viongozi wa Umma, The Ethics Secretariat, (5) PCCB, na (6) Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora, CHRGG.

  Sasa, katika hali halisi imeonekana kama hizi taasisi zimekuwa kama "Mbwa asiye na meno", mimi si msemaji wa kwanza kuhusu hili. Ushahidi na wanahabari, wanaharakati, na watu wengi wakiwepo wafadhili wa nchi wetu wanasema kwamba uhalisia wa taasisi hizi hauonekani.

  Hivyo basi, kwa kuwa taasisi hizi haziwezi kuchukua hatua, kimsingi hazijaweza kuhimiza uwajibikaji!

  Kwa kuwa tunataka kuona Tanzania yenye mabadiliko makubwa, hasa kuhimiza uwazi na uwajibikaji, narudia kupendekeza kwamba Jukwa la wanaJF hebu likosoe, lipendekeze, na liseme kwa uwazi zaidi namna gani tunakwama na tufanyeje kufika mbele katika taasisi hizi.

  Tuliona wakati fulani wakati wa utawala wa Rais Mkapa, HakiElimu, asasi isiyo ya kiserikali, iliwahi kufungiwa kwa kuwa ilionekana mwiba katika ukweli hasa katika suala la elimu na demokrasia. Mimi Perecy nikiwa pia ni Rafiki wa Elimu, harakati za hiari zinazopata uraghbishi kutoka asasi ya HakiElimu, nawiwa kuendelea kuomba wanaJF kukuza mjadala huu, kwani ukweli ubutu wa asasi hizi ni dhahiri kabisa.

  PCCB haijafanya chochote kuhusu rushwa. Rushwa kubwa na wahusika wake wapo mitaani (mafaili ofisini), na huku wakiwa katika nafasi za kazi serikalini, ambapo hakuna uhakika kwamba hatua madhubuti zitachukuliwa. Rushwa ndogo ndio hazishughulikiwa kabisa. Bunge mahali kkwingi tu linakwama kutetea maslahi mapana ya umma. Tume ya maadili ya viongozi wa umma ofisi zake mimi hata sijui zikowapi. Mapungufu katika kusimamia utawala bora, kuchukua hatua na uwajibikaji wa taasisi hizi ni mengi. Zimebaki na maadhumuni yake katika makaratasi zaidi kuliko katika vitendo hai ambavyo pia vingelete uhai na uaminifu wa serikali kwa wananchi.

  Najua wana Jf sio watu lelemama, wanajadili mambo kwa kina; na wanapika watu wa nyadhifa zote kwa kuwapitisha katika tanuru hili la "Great Thinkers"; hebu hizi taasisi tuzijadili kwa upya na tuhimize mabadiliko yake.

  Nawashukuru sana kwa kuwa sehemu yangu muhimu ya kujifunza!

  Ni mimi,

  Perecy Ugula
  MwanaJF Mchanga.
   
Loading...