Mkuu huwezi kujua dini yangu kwa kutumia darubini,ninacho kikataa ni kutumia lugha za kuudhi
Na mimi naona Usivyopenda kutumia Lugha ya maudhi.Kwenda zako we ngiri kipofu
Aisee kumbe dini inatumika kama mwamvuliMashirika ya dini ni miongoni mwa taasisi zilizotakiwa kuwasilisha nyaraka kwa ajili ya kuhakiki kama yalilipa ushuru wa bandari uliosababisha Serikali kupoteza Sh48 bilioni.
Uwapo wa taasisi hizo za kiimani kwenye sakata hilo ulibainishwa jana katika orodha ya iliyotangazwa jana na Mamlaka ya Bandari (TPA) ambayo ina kampuni na taasisi 40 zaidi ya orodha iliyotangazwa juzi yenye kampuni 243. Kwa tangazo la jana, kampuni na taasisi zinazotakiwa kuwasilisha nyaraka kuhusu malipo hayo sasa ni 283.
Tangazo la TPA lilitolewa jana likiwa na tarehe ya Desemba 24, linazitaka taasisi hizo ambazo ni Baraza la Kikristo Tanzania (CCT) na Shirika la Misaada la Kanisa Katoliki, Caritas Tanzania na nyingine 281 kwenda kuchukua barua zao kwa ajili ya uhakiki wa malipo ya ushuru huo yaliyofanyika kuanzia Julai 2014 hadi Aprili, 2015.
Taasisi nyingine maarufu zilizopo katika orodha hiyo ni klabu maarufu ya mchezo wa soka ya Azam Football, kampuni maarufu ya Toyota Tanzania Ltd na Bakhresa Food Products.
Juzi Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa alizihusisha baadhi ya taasisi hizo 283 na upitishaji wa makontena 11,884 na magari 2,019 kwenye bandari bila kulipia ushuru wa bandari.
Kubainika kwa ukwepaji huo ushuru, kunafanya idadi ya makontena yaliyohusika katika suala hilo kufikia 14,664. Awali makontena 349 yaligundulika kupitishwa kinyemela baada ya Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa kufanya ziara bandarini na mengine 2,431 kubainika baadaye.
Mbarawa aliwataka mawakala wa forodha na kampuni hizo 283 zinazotuhumiwa katika utoaji wa makotena na magari bila kulipia ushuru kupeleka vielelezo vya uthibitisho ndani ya siku saba kuanzia juzi.
Msemaji wa CCT, Mchungaji John Kamoyo alisema watafanya kama lilivyoagiza kwenda kuchukua barua zao.
“Kama walivyoeleza sisi tutaenda kuchukua barua na kufahamu kilichopo ndani na tutafanya kama walivyoagiza,” alisema Kamoyo huku akikataa kuhusisha wito huo na suala lolote linalohusina na ukwepaji wa kodi.
Katibu mtendaji wa Caritas Tanzania, Laurent Masui alisema atashirikiana na mamlaka hiyo kutimiza agizo hilo.
“Ni kweli tunahusika na utoaji mizigo bandarini lakini kwa wateja mahususi kutoka mashirika ya kidini ambayo husamehewa baadhi ya kodi na ushuru. Lakini tozo nyingine huwa tunalipa na kwa kuwa tangazo lenyewe linaonekana ni la kiutawala, basi nitawatuma maofisa wangu haraka wafuatilie ili tujue kama tulizidisha ushuru au tulitoa pungufu,” alisema Nasui.
We katonta. Unafahamu Mabilion mangapi Bakhresa kalipia ktk nchi hii?
Hebu nambie Kanisa Katoliki Limechangia hata shs Moja ktk Kodi za nchi hii? Wezi wakubwa
Vizuri ungemuuliza mama yako ndiyo anajua habari zake, wewe unatumia hizi lugha halafu unakimbilia kwa Mods kauzu kweli wewe punguani.Aulizwe baba Ritz
Teh teh teh!!Cc:mods
Mkuu sijui unaongea nini serikali inasema taasisi za dini za Kikristo wamefanya udanganyifu kuna ukwepaji wa kodi wa kiasi cha bilioni 48 wewe unaleta story za Bible.Nilichojifunza kwenye UZI hu ni hiki; Wakristo walivyosikia kuna wito wa kufanya uhakiki wa kodi TRA fasta viongozi wao wame respond but ile barua ya TRA kwenda BAKWATA hadi leo sijawahi kusikia responce yoyote kuyoka kwa any senior official wa Bakwata. Nimejifunza pia bado watu tuna chuki za kidini; yaani kama kosa limefanywa na taasisi ya dini yako watu wa dini husika mnataka kutetea and verse versa. Sina hakika na vitabu vya kiislam vinavyo sema but kwenye Biblia kuna msisitizo mkubwa wa muumini kulipa KODI. Na wale ambao hua wanatufundisha kwamba neno la Mungu linasema tuzitii mamlaka za dunia, maandiko yale yanaendelea kwa kugusia ulipaji wa kodi.
Utafiti wangu binafsi labda pia ni hu; ukienda kwenye taasisi za Kikristo unaweza kuziona mali zinazo milikiwa na taasisi hizo but kwa taasisi za Kiislam hua ni ngumu sana kuyaona walau magari au mali za misikiti.
Mkuu serikali inapoteza mapato ya bilioni 48 halafu Watanzania wale wanaojitapa wanataka mabadiliko wapo kimya kulisema hili kisa linawahusu Kanisa.
Mada hapa ni Kanisa kufanya udanganyifu kukwepa kodi kwa hiyo kama Home Shopping wanakwepa kodi basi Kanisa nalo linapata excuse kufanya udanganyifu wa ukwepaji kodi?Mbona huongelei kuhusu Bakheresa na Home Shopping Centre? By the way kama sikosei wameambiwa wapeleke evidence za malipo. Itakuwaje kama zililipwa halafu wajanja wakatia mfukoni. Hongereni awamu ya nne kwa kutajirisha wateule wenu
Hongera xn mkuu na Mungu AkubarikiSidhani kwamba ati taasisi ya kidini au kanisa lolote likivunja sheria ndo wauminni wake wapashe misuli kulitetea, tena kufikiria hivyo kunazidi upotovu uliotukuka. Amini nawaambieni, si kwa faida ya waunmini wote ila waroho wachache ambao wamo hata ufanye nini kwa sababu ya hulka ya kibinadamu, kumtetea mwovu ati kwa kuwa mpo dini moja ni dhambi ambayo adhabu yake yawezafananaishwa na ile ya kufungiwa jiwe kubwa na kutupwa ktk kina cha bahari ili asije akakumbukwa.
Hebu fikiria wewe binafsi, umefaidika vipi na upotovu huo, kama hapana basi usipoteze nguvu yako kutetea, kwa sababu wahusika ndani ya hizo taasisi nao wanao ndugu zao wa karibu wa kuwapendelea na hawatakukumbuka wewe hata usali mpaka uchubuke magoti.
Kwani mnafikiri ati kanisa likisafirisha madawa ya kulevya wauimini wake hawatadhulika! HAPANA...
Uchunguzi ufanywe na wote wanaohusika wajitenge kabisa na hizi taasisi za kidini ambazo mara nyingi zillianzishwa kwa malengo mazuri tu ya kusaidia jamii.
Lakini kuhusu swala la kufuta misamaha ya kodi kabisa, hilo halijakaa vizuri, fikra iwe kuhakikisha misamaha inayotolewa inakuwa ni ile iliyo kusudiwa tu, mfano, vifaa vya hospitali (pamoja na magari), vifaa vya ujenzi vya kanisa au misikiti, na kama ni magari, ihakikishwe kweli magari haya yanatumika kutoa huduma zilizokusudiwa.
Ukisikia kiongozi wa dini kamnunulia gari kwa msamaha wa kodi ndugu yake, (mama, baba na hata wengine wanavi mada) we unafikiri mimi kama muumini wa kawaida nafaidika nini! Wote watende kadiri ya wanavyotakiwa hakuna mmoja kuonewa haya, hata Mungu mwenyewe hapendi hayo, haya na sisi wanadamu sasa tunaanza kubishana kisa dini! tuache haya ya watu binafisi ndani ya taasisi yashuhulikiwa no excuses.
Kijana umechambia @Tangawizi au?Mbona huongelei kuhusu Bakheresa na Home Shopping Centre? By the way kama sikosei wameambiwa wapeleke evidence za malipo. Itakuwaje kama zililipwa halafu wajanja wakatia mfukoni. Hongereni awamu ya nne kwa kutajirisha wateule wenu
Inatia kinyaa kwa viongozi wa dini kukwepa kulipa kodi, mtoto akifa kwa kukosa dawa kwenye zahanati damu imo mikononi mwao!Wengi walijificha kwenye migongo ya makanisa,ng'o na mengineyo. Tunataka tujuwe majina yao na walichokuwa wanaleta kwenye makontena.
Kwa hili nakuunga mkono ustaadh @Ritz. Utajiri wa baadhi ya wachungaji na Mapadre unazua maswali. Hadi sass Hospitali ya Dodoma Christian Medical Centre DCMC inajulikana ni ya kanisa na kuna magari yameingizwa eti ni ya hospitali kumbe watu washayanywa. Ile hospitali inamilikiwa na Askofu Mstaafu wa kanisa moja kubwa hapa nchini la CCT.Mkuu hapa tunaangalia utaifa kwanza siyo ushabiki mandazi wa kidini, kama Bawakata wamefanya hayo wachukuliwe hatua za kisheria na CCT na Kanisa Katoliki wamefanya udanganyifu pia wachukuliwe hatua za kisheria.
Hapa Kazi Tu.
We nae acha ubwege na nasuruali fupi ka kipedo, dini zote zinachakachua ya mwarabu na ya huyo myahudi/mzungu wazishughilikie waovu kwenye hizi tasisi za kidini wajulilane na wawajibishweWaliolaaniwa wanaumbuka.
Alhamdulillah.
Laana ni laana tu. Hata ukiificha vipi lzm Itoke.
Sisi tukisema Hizi imani zingine ni Usanii na Utapeli Mnalalamika na Kutulaani Tazama sasa. NCHI YETU inamalizwa na Chombo kile kile alichotuletea MZUNGU nacho ni UGALATIA.
Km mimi ni magufuli basi naanzisha Dhehebu langu la Kisukuma. Hii ni Cancer ya Nchi yetu.
Imani ya kizungu inajulikana manake mpk picha za wazungu mmezisambaza mpk mavyumbani mwenu.We nae acha ubwege na nasuruali fupi ka kipedo, dini zote zinachakachua ya mwarabu na ya huyo myahudi/mzungu wazishughilikie waovu kwenye hizi tasisi za kidini wajulilane na wawajibishwe
Komando kipedo mi sio mshaki wa dini zenu- situmii imani kendeaha maishaImani ya kizungu inajulikana manake mpk picha za wazungu mmezisambaza mpk mavyumbani mwenu.
Hio ya Kiarabu sajawahi kuiona bibie.
Halafu mtazame Papa uone km hana kipedo.