Taasisi za Dini Zatajwa Kuhusika na Utoroshaji wa Makontena Bandarini

Chachu Ombara

JF-Expert Member
Dec 11, 2012
6,042
10,787
Mashirika ya dini ni miongoni mwa taasisi zilizotakiwa kuwasilisha nyaraka kwa ajili ya kuhakiki kama yalilipa ushuru wa bandari uliosababisha Serikali kupoteza Sh48 bilioni.

Uwapo wa taasisi hizo za kiimani kwenye sakata hilo ulibainishwa jana katika orodha ya iliyotangazwa jana na Mamlaka ya Bandari (TPA) ambayo ina kampuni na taasisi 40 zaidi ya orodha iliyotangazwa juzi yenye kampuni 243. Kwa tangazo la jana, kampuni na taasisi zinazotakiwa kuwasilisha nyaraka kuhusu malipo hayo sasa ni 283.

Tangazo la TPA lilitolewa jana likiwa na tarehe ya Desemba 24, linazitaka taasisi hizo ambazo ni Baraza la Kikristo Tanzania (CCT) na Shirika la Misaada la Kanisa Katoliki, Caritas Tanzania na nyingine 281 kwenda kuchukua barua zao kwa ajili ya uhakiki wa malipo ya ushuru huo yaliyofanyika kuanzia Julai 2014 hadi Aprili, 2015.

Taasisi nyingine maarufu zilizopo katika orodha hiyo ni klabu maarufu ya mchezo wa soka ya Azam Football, kampuni maarufu ya Toyota Tanzania Ltd na Bakhresa Food Products.

Juzi Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa alizihusisha baadhi ya taasisi hizo 283 na upitishaji wa makontena 11,884 na magari 2,019 kwenye bandari bila kulipia ushuru wa bandari.

Kubainika kwa ukwepaji huo ushuru, kunafanya idadi ya makontena yaliyohusika katika suala hilo kufikia 14,664. Awali makontena 349 yaligundulika kupitishwa kinyemela baada ya Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa kufanya ziara bandarini na mengine 2,431 kubainika baadaye.

Mbarawa aliwataka mawakala wa forodha na kampuni hizo 283 zinazotuhumiwa katika utoaji wa makotena na magari bila kulipia ushuru kupeleka vielelezo vya uthibitisho ndani ya siku saba kuanzia juzi.

Msemaji wa CCT, Mchungaji John Kamoyo alisema watafanya kama lilivyoagiza kwenda kuchukua barua zao.

“Kama walivyoeleza sisi tutaenda kuchukua barua na kufahamu kilichopo ndani na tutafanya kama walivyoagiza,” alisema Kamoyo huku akikataa kuhusisha wito huo na suala lolote linalohusina na ukwepaji wa kodi.

Katibu mtendaji wa Caritas Tanzania, Laurent Masui alisema atashirikiana na mamlaka hiyo kutimiza agizo hilo.

“Ni kweli tunahusika na utoaji mizigo bandarini lakini kwa wateja mahususi kutoka mashirika ya kidini ambayo husamehewa baadhi ya kodi na ushuru. Lakini tozo nyingine huwa tunalipa na kwa kuwa tangazo lenyewe linaonekana ni la kiutawala, basi nitawatuma maofisa wangu haraka wafuatilie ili tujue kama tulizidisha ushuru au tulitoa pungufu,” alisema Nasui.
 
Haya najua hii habari kwa sababu imetanjwa CCT na kanisa katoliki hutowaona watu kutokwa na mapovu. kwani habari imeshasomwa Zaidi ya mara 200 lakini alochangia mmoja lakini nenda kwenye ile habari ya bakwata na uangalie watu povu lilivyowatoka...
 
Haya najua hii habari kwa sababu imetanjwa CCT na kanisa katoliki hutowaona watu kutokwa na mapovu. kwani habari imeshasomwa Zaidi ya mara 200 lakini alochangia mmoja lakini nenda kwenye ile habari ya bakwata na uangalie watu povu lilivyowatoka...
wimbo ushazoeleka. tunachotaka ni pesa tu
 
Wengi walijificha kwenye migongo ya makanisa,ng'o na mengineyo. Tunataka tujuwe majina yao na walichokuwa wanaleta kwenye makontena.
 
Mwanzo waliirukia bakwata ili hizi taasisi nyengene zipate kuweka mambo yao sawa ili ukaguzi ukija wawe safi huu ni ubaguzi mkubwa
 
Kiufupi serikali iondoe misamaha ya kodi ktk taasisi hizi za dini. Nakumbuka mustafa mkulo aliwahi kutaka kuondoa misamaha hii ya kodi makanisa yakaja juu, naamini misamaha hii ya kodi ikiondolewa nchi inaweza kukusanya hata 2 trion kwa mwezi, tatzo lililopo ni kuwa je magufuli ataweza kulitumbua hili jipu?
 
Haya najua hii habari kwa sababu imetanjwa CCT na kanisa katoliki hutowaona watu kutokwa na mapovu. kwani habari imeshasomwa Zaidi ya mara 200 lakini alochangia mmoja lakini nenda kwenye ile habari ya bakwata na uangalie watu povu lilivyowatoka...

Tuliona alipotajwa Bakhresa watu walipigana kutetea humu, sisi wengine tu tofauti. Kama taasisi za kidini zilihusika kukwepa kodi ziwajibike kwa dhambi hiyo. Hatutetei ujinga kama baadhi ya maimuna humu
 
Haya najua hii habari kwa sababu imetanjwa CCT na kanisa katoliki hutowaona watu kutokwa na mapovu. kwani habari imeshasomwa Zaidi ya mara 200 lakini alochangia mmoja lakini nenda kwenye ile habari ya bakwata na uangalie watu povu lilivyowatoka...
hapa ndio utajua unafiki Wa watu
 
Kiufupi serikali iondoe misamaha ya kodi ktk taasisi hizi za dini. Nakumbuka mustafa mkulo aliwahi kutaka kuondoa misamaha hii ya kodi makanisa yakaja juu, naamini misamaha hii ya kodi ikiondolewa nchi inaweza kukusanya hata 2 trion kwa mwezi, tatzo lililopo ni kuwa je magufuli ataweza kulitumbua hili jipu?
Tutaweza kulipia huduma nyingine zinazotolewa na mashirika haya ya kidini hasa HOSPITALI na misaada mingine tutaikosa kama kuchimbiwa visima,vituo vya wasiojiweza hasa watoto n.kBado srikali haijajipanga katika maeneo hayo
 
Usikashifu mtu bila kujua swala lenyewe kikamilifu. Hayo makontena ni ya shirika la misaada la kanisa katoliki liitwalo Caritas na halina uhusiano binafsi na Mhashamu Policarp Kardinali Pengo. Kama amenenepa ni sisi waumini tunamlisha na hategemei ukwepaji kodi ili ale.

Sidhani kwamba ati taasisi ya kidini au kanisa lolote likivunja sheria ndo wauminni wake wapashe misuli kulitetea, tena kufikiria hivyo kunazidi upotovu uliotukuka. Amini nawaambieni, si kwa faida ya waunmini wote ila waroho wachache ambao wamo hata ufanye nini kwa sababu ya hulka ya kibinadamu, kumtetea mwovu ati kwa kuwa mpo dini moja ni dhambi ambayo adhabu yake yawezafananaishwa na ile ya kufungiwa jiwe kubwa na kutupwa ktk kina cha bahari ili asije akakumbukwa.

Hebu fikiria wewe binafsi, umefaidika vipi na upotovu huo, kama hapana basi usipoteze nguvu yako kutetea, kwa sababu wahusika ndani ya hizo taasisi nao wanao ndugu zao wa karibu wa kuwapendelea na hawatakukumbuka wewe hata usali mpaka uchubuke magoti.

Kwani mnafikiri ati kanisa likisafirisha madawa ya kulevya wauimini wake hawatadhulika! HAPANA...

Uchunguzi ufanywe na wote wanaohusika wajitenge kabisa na hizi taasisi za kidini ambazo mara nyingi zillianzishwa kwa malengo mazuri tu ya kusaidia jamii.

Lakini kuhusu swala la kufuta misamaha ya kodi kabisa, hilo halijakaa vizuri, fikra iwe kuhakikisha misamaha inayotolewa inakuwa ni ile iliyo kusudiwa tu, mfano, vifaa vya hospitali (pamoja na magari), vifaa vya ujenzi vya kanisa au misikiti, na kama ni magari, ihakikishwe kweli magari haya yanatumika kutoa huduma zilizokusudiwa.

Ukisikia kiongozi wa dini kamnunulia gari kwa msamaha wa kodi ndugu yake, (mama, baba na hata wengine wanavi mada) we unafikiri mimi kama muumini wa kawaida nafaidika nini! Wote watende kadiri ya wanavyotakiwa hakuna mmoja kuonewa haya, hata Mungu mwenyewe hapendi hayo, haya na sisi wanadamu sasa tunaanza kubishana kisa dini! tuache haya ya watu binafisi ndani ya taasisi yashuhulikiwa no excuses.
 
Hawa jamaa wananufaika sana na mfumo wa wizi wa serikali za tanzania tangu uhuru
Na usije ukashangaa hii post ikawa suspended na ikaondoshwa kabisa. Unajua mimi kitu kimoja kinanisumbua sana kukifahamu. karibu hizi taasisi zinapata misamaha ya kodi lakini ukienda kutika hospital zao au shule zao, gharama ya kupata huduma ni sawa na taasisi ambazo hazilipi kodi...sasa hii inamsaidiaje mtanzania?
 
Wabanwe mpaka walipe pesa zetu wasilete ujinga hakuna kucheka na mtu hapa kazi tu.
 
Hii ngumu kumeza tatizo kubwa la watanzania tunatawaliwa na unafiki mkubwa, adui wa Tanzania ni Watanzania wenyewe.

Kwenye huu uzi unaona kabisa wale Wakirstu waliokuwa wanapiga kelele kwenye sakata la Bakwata kuingiza magari kinyume na sheria hata mmoja uwezi kumuona kwenye huu uzi wakikemea Wakirstu wenzao, namna hii hatuwezi kujenga taifa lenye nidhamu kama kuna double standard.

Watanzania wazalendo wenye uchungu na taifa lao mpo wapi kukemea hui ufisadi.

Nakala kwa... @kahtaan, @FaizaFoxy, @njiwa, @THE BIG SHOW
 
Hivi lile sakata la BAKWATA na TRA limeishia wapi vile!!?
Mkuu wewe ni mwandishi wa habari zama zaidi kwenye sakata la Kanisa kukwepe kodi uwafahamishe Watanzania acha ushabiki mandazi mkuu.
 
Haya najua hii habari kwa sababu imetanjwa CCT na kanisa katoliki hutowaona watu kutokwa na mapovu. kwani habari imeshasomwa Zaidi ya mara 200 lakini alochangia mmoja lakini nenda kwenye ile habari ya bakwata na uangalie watu povu lilivyowatoka...

Kule BAKWATA kuna misikiti iliomba msamaha wa kodi wa mavogue ukiangalia msikiti ulivyo choka mbaya alafu umeagiza Vogue kwa ajili ya Sheikh.
 
Wagalatia bana wanajifanya kuupita kwa mbali huu kama hawauoni kisa unawahusu wao daah!! Hii nchi bana eti ndiyo watu wanataka mabadiliko.
 
Back
Top Bottom