Taasisi ya Trademark East Africa kuisaidia Zanzibar

Pascal Mayalla

Platinum Member
Sep 22, 2008
37,962
2,000
Waziri Mhe. Balozi Amina Salum Ally Alipotembelea TradeMark East Africa1.jpg
Waziri Mhe. Balozi Amina Salum Ally Alipotembelea TradeMark East Africa3.jpg
Waziri Mhe. Balozi Amina Salum Ally Alipotembelea TradeMark East Africa4.jpg
Waziri Mhe. Balozi Amina Salum Ally Alipotembelea TradeMark East Africa5.jpg
Waziri Mhe. Balozi Amina Salum Ally Alipotembelea TradeMark East Africa6.jpg
Waziri Mhe. Balozi Amina Salum Ally Alipotembelea TradeMark East Africa6.jpg
Waziri Mhe. Balozi Amina Salum Ally Alipotembelea TradeMark East Africa7.jpg
Waziri Mhe. Balozi Amina Salum Ally Alipotembelea TradeMark East Africa8.jpg
Waziri Mhe. Balozi Amina Salum Ally Alipotembelea TradeMark East Africa1.jpg
Waziri Mhe. Balozi Amina Salum Ally Alipotembelea TradeMark East Africa1.jpg
Waziri Mhe. Balozi Amina Salum Ally Alipotembelea TradeMark East Africa3.jpg
Waziri Mhe. Balozi Amina Salum Ally Alipotembelea TradeMark East Africa4.jpg
Waziri Mhe. Balozi Amina Salum Ally Alipotembelea TradeMark East Africa5.jpg
Waziri Mhe. Balozi Amina Salum Ally Alipotembelea TradeMark East Africa6.jpg
Waziri Mhe. Balozi Amina Salum Ally Alipotembelea TradeMark East Africa6.jpg
Waziri Mhe. Balozi Amina Salum Ally Alipotembelea TradeMark East Africa7.jpg
Waziri Mhe. Balozi Amina Salum Ally Alipotembelea TradeMark East Africa8.jpg
Taasisi ya TradeMark East Africa, TMEA, imeahidi kuisaidia Zanzibar, katika kukuza biashara na kuondoa vikwazo vya Biashara kwa bidhaa za Zanzibar, ili ziweze kuingia kwenye soko ya nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki ambapo bidhaa hizi zikiingia sokoni, hazitakuwa tena ni bidhaa za Zanzibar bali zitakuwa ni bidhaa za Tanzania.


Ahadi hiyo imetolewa na Mkurugenzi wa Taasisi ya TradeMark East Afrika, Tawi la Tanzania, Bw. John Ulanga, akijibu ombi la Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, lililoletwa na Waziri wa Viwanda, Biashara na Masoko wa Zanzibar, Balozi, Amina Salum Ally, kwa taasisi hiyo, wakati Waziri huyo alipofanya ziara ya kuitembelea taasisi hiyo, jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.


Akiwasilisha ombi rasmi kwa la Zanzibar kwa taasisi hiyo, Waziri Balozi Amina Salum Ally ameiomba taasisi hiyo, ya TMEA, kuisaidia Zanzibar kuondoa vikwazo vya kibiashara kwa bidhaa kutoka Zanzibar, kuingia katika masoko ya Tanzania baa, soko la Afrika ya Mashariki na masoko ya kimataifa.


Balozi Amina, amesema, ili Tanzania ya viwanda iweze ilete manufaa kwa Tanzania kwa jumla, lazima Tanzania hiyo ya Viwanda iwafaidie watu wa pande zote mbili za muungano, na namna ya Zanzibar kufaidika na Tanzania ya Viwanda, ni kwa bidhaa kutoka Zanzibar, kupata masoko ya kutosha ya kitaifa na kimataifa ambapo yatahamashisha uzalishaji zaidi na kuvutia uwekezaji katika kujenga viwanda Zanzibar.


Akijibu maombi hayo, Mkurugenzi wa Taasisi ya TradeMark East Afrika, Tawi la Tanzania, Bw. John Ulanga, amesema taasisi yake imelipokea ombi hilo kwa mikono miwili, na kukiri kuwepo kwa ushiriki hafifu kwa wafabiashara wa Zanzibar katika maonyesho mbalimbali ya kimataifa ya biashara, kunakopelekea bidhaa za Zanzibar kutofahamika ipasavyo na hivyo kushindwa kuvutia masoko ya kimataifa.


Ulanga, amesema, TMEA, imejisikia fahari sana kutembelewa na Waziri kutoka Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, hivyo yeye na timu yake, wamelipokea ombi la Zanzibar kwa mikono miwili na watalifanyia kazi mapema iwezekanavyo.


Hivi karibuni, TIMEA ilitoa zaidi ya shilingi bilioni 200, kuiwezesha Chemba ya Biashara ya Tanzania, Tanzania Chamber of Commerce, Industry and Agriculture (TCCIA) na ile ya Zanzibar, Zanzibar National Chamber of Commerce Industry and Agriculture (ZNCCIA) kushirikiana katika kuwajengea uwezo, wanachama wake.


TradeMark East Africa (TMEA) ni shirika lisilo la kiserikali, la maendeleo kwa lengo la kuongezeka ustawi wa kiuchumi katika nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki kwa njia ya biashara. TMEA inafanya kazi kwa karibu na taasisi za Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC), serikali za kitaifa, sekta binafsi na asasi za kiraia.
TMEA inachangia ukuaji wa biashara Afrika Mashariki kwa kufungua fursa za kiuchumi kupitia:
• Kuongezeka kwa fursa za upatikanaji wa masoko;
• Kuboresha mazingira ya biashara; na
• Kuboresha biashara ya ushindani.
Kuongezeka kwa kiwango cha biashara kuchangia ukuaji wa uchumi, na kupunguza umaskini na hatimaye kuongezeka ustawi.


TMEA ina makao yake makuu mjini Nairobi nchini Kenya, na ina matawi katika miji ya Arusha, Bujumbura, Dar es Salaam, Juba, Kampala na Kigali.
Ili kujua zaidi kuhusu TMEA, tafadhali tembelea tovuti TMEA katika www. www.trademarkea.com


Paskali


Maelezo ya Picha

1.Waziri wa Viwanda, Biashara na Masoko wa serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Balozi, Amina Salum akizungumza na Mkurugenzi wa Taasisi ya TradeMark East Afrika, Tawi la Tanzania, Bw. John Ulanga, wakati Waziri huyo alipofanya ziara ya kuitembelea taasisi hiyo, jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.Taasisi ya TradeMark East Africa, TMEA, imeahidi kuisaidia Zanzibar, katika kukuza biashara na kuondoa vikwazo vya Biashara kwa bidhaa za Zanzibar, ili ziweze kuingia kwenye soko ya nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki ambapo bidhaa hizi zikiingia sokoni, hazitakuwa tena ni bidhaa za Zanzibar bali zitakuwa ni bidhaa za Tanzania.

2.Waziri wa Viwanda, Biashara na Masoko wa serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Balozi, Amina Salum akizungumza na Mkurugenzi wa Taasisi ya TradeMark East Afrika, Tawi la Tanzania, Bw. John Ulanga, wakati Waziri huyo alipofanya ziara ya kuitembelea taasisi hiyo, jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.Taasisi ya TradeMark East Africa, TMEA, imeahidi kuisaidia Zanzibar, katika kukuza biashara na kuondoa vikwazo vya Biashara kwa bidhaa za Zanzibar, ili ziweze kuingia kwenye soko ya nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki ambapo bidhaa hizi zikiingia sokoni, hazitakuwa tena ni bidhaa za Zanzibar bali zitakuwa ni bidhaa za Tanzania.

3.Waziri wa Viwanda, Biashara na Masoko wa serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Balozi, Amina Salum akizungumza na Mkurugenzi wa Taasisi ya TradeMark East Afrika, Tawi la Tanzania, Bw. John Ulanga, wakati Waziri huyo alipofanya ziara ya kuitembelea taasisi hiyo, jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.Taasisi ya TradeMark East Africa, TMEA, imeahidi kuisaidia Zanzibar, katika kukuza biashara na kuondoa vikwazo vya Biashara kwa bidhaa za Zanzibar, ili ziweze kuingia kwenye soko ya nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki ambapo bidhaa hizi zikiingia sokoni, hazitakuwa tena ni bidhaa za Zanzibar bali zitakuwa ni bidhaa za Tanzania.

4.Maofisa waTaasisi ya TradeMark East Afrika, Tawi la Tanzania, wakimsikiliza Waziri wa Viwanda, Biashara na Masoko wa serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Balozi, Amina Salum (hayuko pichani), wakati Waziri huyo alipofanya ziara ya kuitembelea taasisi hiyo, jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki ambapo, Taasisi ya TradeMark East Africa, TMEA, imeahidi kuisaidia Zanzibar, katika kukuza biashara na kuondoa vikwazo vya Biashara kwa bidhaa za Zanzibar, ili ziweze kuingia kwenye soko ya nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki ambapo bidhaa hizi zikiingia sokoni, hazitakuwa tena ni bidhaa za Zanzibar bali zitakuwa ni bidhaa za Tanzania.

5.Waziri wa Viwanda, Biashara na Masoko wa serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Balozi, Amina Salum akipokea kabrasha la TMEA, toka kwa Mkurugenzi wa Taasisi ya TradeMark East Afrika, Tawi la Tanzania, Bw. John Ulanga, wakati Waziri huyo alipofanya ziara ya kuitembelea taasisi hiyo, jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki ambapo, Taasisi ya TradeMark East Africa, TMEA, imeahidi kuisaidia Zanzibar, katika kukuza biashara na kuondoa vikwazo vya Biashara kwa bidhaa za Zanzibar, ili ziweze kuingia kwenye soko ya nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki ambapo bidhaa hizi zikiingia sokoni, hazitakuwa tena ni bidhaa za Zanzibar bali zitakuwa ni bidhaa za Tanzania.

6.Waziri wa Viwanda, Biashara na Masoko wa serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Balozi, Amina Salum katika picha ya pamoja na Mkurugenzi wa Taasisi ya TradeMark East Afrika, Tawi la Tanzania, Bw. John Ulanga, wakati Waziri huyo alipofanya ziara ya kuitembelea taasisi hiyo, jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki ambapo Taasisi ya TradeMark East Africa, TMEA, imeahidi kuisaidia Zanzibar, katika kukuza biashara na kuondoa vikwazo vya Biashara kwa bidhaa za Zanzibar, ili ziweze kuingia kwenye soko ya nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki ambapo bidhaa hizi zikiingia sokoni, hazitakuwa tena ni bidhaa za Zanzibar bali zitakuwa ni bidhaa za Tanzania.

7.Waziri wa Viwanda, Biashara na Masoko wa serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Balozi, Amina Salum akihojiwa na mwandishi wa habari Pascal Mayalla,, wakati Waziri huyo alipofanya ziara ya kuitembelea taasisi hiyo, jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.Kushoto ni na Mkurugenzi wa Taasisi ya TradeMark East Afrika, Tawi la Tanzania, Bw. John Ulanga ambapo Taasisi ya TradeMark East Africa, TMEA, imeahidi kuisaidia Zanzibar, katika kukuza biashara na kuondoa vikwazo vya Biashara kwa bidhaa za Zanzibar, ili ziweze kuingia kwenye soko ya nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki ambapo bidhaa hizi zikiingia sokoni, hazitakuwa tena ni bidhaa za Zanzibar bali zitakuwa ni bidhaa za Tanzania.

8.Mkurugenzi wa Taasisi ya TradeMark East Afrika, Tawi la Tanzania, Bw. John Ulanga akihojiwa na mwandishi wa habari Pascal Mayalla,, wakati wa ziara ya Waziri wa Viwanda, Biashara na Masoko wa serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Balozi, Amina Salum Ally alipofanya ziara ya kuitembelea taasisi hiyo, jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki, ambapo Taasisi ya TradeMark East Africa, TMEA, imeahidi kuisaidia Zanzibar, katika kukuza biashara na kuondoa vikwazo vya Biashara kwa bidhaa za Zanzibar, ili ziweze kuingia kwenye soko ya nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki ambapo bidhaa hizi zikiingia sokoni, hazitakuwa tena ni bidhaa za Zanzibar bali zitakuwa ni bidhaa za Tanzania.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom