Taasisi gani ilichunguza tuhuma za Ombeni Sefue

SONGOKA

JF-Expert Member
Mar 8, 2012
1,841
1,843
Mode kwa utashi wako, iache thread hii ili tupate specific information

Wakuu, tuhuma zozote ili zithibitishwe au zikanushwe lazima kuwe na uchunguzi wa kina, na kimsingi taasisi za uchunguzi ziko nyingi na mfano wake ni, Tume ya maadili, TAKUKURU, POLISI,TISS, CAG na Kamati teule kutoka mamlaka mbalimbali.

Je tuhuma za rushwa na matumizi mabaya ya madaraka zinazomkabili Ombeni Sefue, ambazo tayari majibu ya kumsafisha yameshatolewa tena ndani ya siku mbili zilichunguzwa na taasisi gani kati ya hizo?? Je idara ya habari maelezo wanaweza kutwambia report ya uchunguzi waliipata wapi?? na waliochunguza wanaweza kutwambia terms of reference za uchunguzi huo zilikuwa zipi .

Ili tujiridhishe kuwa Sefue ni msafi, tunaomba mtwambie jina la taasisi iliyosimamia uchunguzi huo mpaka report ikatoka na kufikishwa habari maelezo na kwa vyombo vya habari

Mwisho, kwanini Dr fortunatus namahala alisimamishwa hapohapo na waziri mkuu kwa tuhuma za mdomo tu, lakini Ombeni Sefue tunaambiwa mwenye ushahidi aupeleke mahakamani??

Kwanini yule mama aliyemtuhumu (Tatu Abdallah) asingeambiwa pia apeleke ushahidi mahakamani??

Mtujuze kuhusu hili
 
Back
Top Bottom