Taasisi 4 za serikali hoi kifedha, ipo Tume ya Umwagiliaji, Wabunge wacharuka

Mdakuzi mkuu

JF-Expert Member
Dec 27, 2016
212
719
1. Ofisi ya Binge
2. Tume ya Umwagiliaji
3. Zimamoto na Uokoaji
4. Idara ya Mifugo
Inasemekana hazijapata fedha ya robo ya mwaka.

==========

Dodoma. Wabunge wameicharukia Serikali kwa kutofikia lengo la kupeleka fedha za maendeleo katika robo ya kwanza ya bajeti ya mwaka 2016/17 ambayo inaonyesha taasisi nne ziko katika hali mbaya kwa kutopelekewa kabisa.

Taasisi hizo zimetajwa kuwa ni Ofisi ya Bunge, Tume ya Umwagiliaji, Idara ya Mifugo na Zimamoto na Uokoaji.

Taarifa ya Kamati ya Bunge ya Bajeti ya kipindi cha Januari 2016 hadi Januari 2017, iliyosomwa bungeni jana na mwenyekiti wake, Josephat Kandege, ilisema Mamlaka ya Serikali za Mitaa nayo imo katika kundi la walioathirika kwa kupata fedha kwa asilimia 57.

Kandege alisema kamati ilibaini mbali na Serikali kuvuka lengo la kupeleka fedha za matumizi ya kawaida (OC) lakini haikupeleka fedha yoyote kwa ajili ya utekelezaji wa shughuli za utawala kwa halmashauri zote nchini.

“Pia, Serikali ilipeleka asilimia 19 tu ya fedha za matumizi ya kawaida zilizotengwa kwa ajili ya kugharimia sekta ya afya. Hali hii imesababishwa na baadhi ya mafungu kupewa fedha nyingi zaidi ya zilizokuwa zimepangwa kutolewa katika kipindi husika,” alisema.


Chanzo: MWANANCHI
 
"Nchi hii ni yakuwapa wengine misaada"-magu
"hatuhitaji hela za MCC umeme vijijuni mbele kwa mbele:;-anonymous

Leo zaidi ya nusu mwaka wa fedha maji wamepewa 10% ya maendeleo

Viwanda wamepata 2billion kati ya 9 billion za maendeleo
 
Ni wizara chache sana hupewa kipaumbele cha fedha, zingine zote watumishi wanasubiri mishahara tu.
 
Back
Top Bottom