Wale mnaosema huu ni wakati wa vijana naomba mfikirie tena.
Kauli za Nape si za kiungwanahata kidogo. Huu ni msiba mkubwa kwa taifa.
Sidhani kuna mtoto anaajua siasa ni nini. Na hata kama anajua kuna ubaya gani yeye kushiriki shughuli za kisiasa kama mtu anayejifunza?
Leo Nape anatumia damu za watoto hao na raia wengine wasio na hatia kutangaza habari za siasa.
Lile bomu lingeangukia na kuua viongozi wa CDM sijui kama angesema limepangwa.
Nape labda tukukmbushe haya
1. Mwakyembe kutaka kuuawa na kutaja hadi wahusika tukio lile lilipangwa na nani?
2. Mengi na mtoto wake kuwekewa mtego, tukio lile lilipangwa na nani?
3. Ulimboa kung'olewa kucha na meno tukio hilo lilipangwa na nani?
4. Mwangosi kutolewa roho, tukio hio lilipangwa na nani?
5. Kibanda kung'olewa meno na jicho, tukio hilo limepangwa na nani?
6. Mbwambo kuchinjwa kwa msumeno kule Tengeru, tukio hilo lilipangwa na nani?
7. Kule Igunga mtu kutoweka, tukiolilipangwa na nani?
Orodha ni ndefu na katika matukio yote hayo hakuna majibu hadi sasa.
Si chama au serikali ya chama chako imewahi kutolea majibu. Majibu ni upepo utapita.
Nape wewe unaishi Tanzania, na nyadhifa zako pamoja na maisha yako ni kwasababu upo Tanzania .
Yakitokea yasiyotarajiwa na yasiyo ombewa si wewe si mimi au yule atakayekuwa salama.
Hakuna shujaa kati kati ya vita na vurugu
Nakusihi sana mdogo wangu iangalie Tanzania kwanza halafu ndipo uangalie mambo mengine.
Unaandika kwa jeuri na dharau kwasababu upo ndani ya Tanzania iliyotulia na inayolekea kuchafuka.
Kwanini kijana wa umri wako unafikia mahali pa kujisahau namna hiyo?
Kama Nyerere alisema CCM si mama yake, wewe ni nani nakwa uwezo upi unadhani CCM ni bora kuliko roho za Watanzania wasio na hatia.
Hivi wanajamvi, hawa ndio vijana tunaowapigia debe waliongoze taifa kweli!
Kama Nape kasema hivi nani kabaki na kabaki na busara ipi?
Nape, ubinadamu ni bora kuliko bendera za chama. Utangulize ubindamu na usilewe na dunia hii.
Leo unaona roho za watu na damu zao ni nyepesi kwasababu una rungu, umesahau kuwa unaishi ndani ya nyumba ya glass.
Mungu akusadie uone kile uischokiona sasa hivi, na heri ya kukaa kimya ili watu wawe na shaka nawe kuliko kuongea na kuwatoa mashaka waliyokuwa nayo juu yako.
Bado ni mdogo Nape, tuulize tumeyaona mengi, tumewaona wafalme wakipaa na kuanguka.