Taarifa za Chama toka NAPE kuhusu Mlipuko: KAULI ya KIKWETE hukusu shambulizi la BOMU Arusha


nngu007

nngu007

JF-Expert Member
Joined
Aug 2, 2010
Messages
15,871
Likes
90
Points
145
nngu007

nngu007

JF-Expert Member
Joined Aug 2, 2010
15,871 90 145
HII NDIYO KAULI YA RAIS JAKAYA KIKWETE KUHUSU SHAMBULIO LA MLIPUKO WA BOMU KWENYE MKUTANO WA CHADEMA ARUSHA
-Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amepokea kwa mfadhaiko, mshituko na huzuni kubwa taarifa za shambulio la mlipuko lililotokea katika mkutano wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) mjini Arusha jioni ya leo, Jumamosi, Juni 15, 2013, tukio ambalo limesababisha vifo vya watu wawili na majeruhi ya Watanzania kadhaa.


Aidha, Rais Kikwete ametuma salamu za rambirambi kwa jamaa na ndugu wa wafiwa wote na pia ametuma pole nyingi kwa majeruhi ambao wameumizwa na kujeruhiwa katika tukio hilo ovu na katili.

Vile vile, Rais Kikwete amewatumia salamu za pole viongozi wa CHADEMA kufuatia tukio hilo la woga mkubwa na pia kuviagiza vyombo vya ulinzi na usalama kuchukua hatua stahiki za kuchunguza kwa haraka, kubaini, kuwakamata na kuwafikisha mbele ya sheria wote waliohusika na tukio hilo, wawe watu wa ndani ya nchi ama nje ya nchi.

Katika salamu zake za rambirambi na za pole kwa Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mheshimiwa Magesa Mulongo, Rais Kikwete amesema: "Nimepokea kwa mfadhaiko, mshituko na huzuni kubwa shambulio la mlipuko lililotokea katika mkutano wa CHADEMA mjini Arusha jioni ya leo, tukio ambalo limesababisha vifo na majeruhi ya Watanzania wenzetu."

Amesema Rais Kikwete: "Nakutumia wewe Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mheshimiwa Magesa Mulongo salamu zangu za rambirambi kufuatia vifo na pole nyingi kutokana na majeruhi katika tukio hilo na naomba kupitia kwako unifikishie salamu zangu za rambirambi kwa jamaa na ndugu wa wafiwa na pole nyingi sana kwa majeruhi."

"Kadhalika naomba unifikishie salamu zangu za pole kwa viongozi na wanachama wa CHADEMA kutokana na tukio hilo. Naomba uwajulishe kuwa uchungu wao ni uchungu wetu sote na msiba wao ni msiba wetu pia. Nataka wajue kuwa tupo pamoja nao katika kipindi hiki kigumu na cha majonzi na huzuni mkubwa," amesema Mheshimiwa Rais Kikwete.

Rais Kikwete amemwambia Mkuu wa Mkoa wa Arusha: "Kadhalika, nimeviagiza vyombo vya ulinzi na usalama kuchukua hatua za haraka kuwasaka wahusika, kuwakamata na kuwafikisha kwenye vyombo vya sheria. Aidha, nawataka viongozi wa Serikali ngazi ya kitaifa, Mkoa wa Arusha na Wilaya ya Arusha mjini kuhakikisha kuwa majeruhi wote wanapata matibabu ya haraka na huduma za tibabu stahiki."

Aidha, Rais Kikwete ametoa wito maalum kwa wananchi akisema: "Kwa wananchi wenzangu, Watanzania wenzangu, napenda kutoa wito wa kuviachia vyombo vya ulinzi na usalama kufanya kazi yao vizuri ili tuweze kuwabaini waovu waliofanya kitendo hiki."

" Natambua kuwa yatakuwepo maneno mengi na hisia mbali mbali zitakazojaribu kulielezea tukio hilio ovu na katili kwa njia mbali mbali. Nawasihi tujiepushe na kuchukua dhana na hisia zetu au maneno ya watu wengine kuwa ni ukweli wa tukio hili. Tujipe nafasi ya kutafakari vizuri na kufanya uamuzi ulio bora."

Ameongeza Rais Kikwete: "Mimi siamini kuwa Watanzania au wafuasi wa vyama vya siasa wanachukiana kiasi cha kufanyiana matendo ya unyama wa aina hii. Naamini kuwa hiki ni kitendo cha mtu ama watu wasioitakia mema nchi yetu, watu ambao wanatafuta kila sababu ya kupandikiza chuki miongoni mwa raia ama makundi ya raia, ili nchi yetu iingie kwenye machafuko makubwa."

"Ndugu zangu, Watanzania wenzangu, naomba tuzinduke, ili tusiwape nafasi watu hawa waovu ya kuweza kutimiza malengo yao ya kuvuruga amani na utulivu wa nchi yetu kwa kuleta mifarakano baina yetu. Mungu Ibariki Tanzania, Munfu Ibariki Afrika."

Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
IKULU,
DAR ES SALAAM


------------------------------
Kauli ya Nape ya Chama fuata kiambatanisho - https://www.jamiiforums.com/jukwaa-...-yawezekana-ulipangwa-na-chadema-wenyewe.html

 
Nicholas

Nicholas

JF-Expert Member
Joined
Mar 7, 2006
Messages
25,231
Likes
2,519
Points
280
Nicholas

Nicholas

JF-Expert Member
Joined Mar 7, 2006
25,231 2,519 280
CCM:Arusha ndio basi tena.Mnafutika ktk ramani yao:Mwigulu alicha watu wake pale iliboro wakishangashangaa....km ktk picture. wanashangashangaa tuu..ili akapige mishemishe..polisi wapitishe picture yale ktk vichochoro vya soweto na pale club..watakuwa walimwona tuuu....akinyata kuja toa maelekezo.
 
mwenezi

mwenezi

JF-Expert Member
Joined
Dec 18, 2012
Messages
505
Likes
14
Points
35
mwenezi

mwenezi

JF-Expert Member
Joined Dec 18, 2012
505 14 35
hapa naona kidampa anapishana kauli na boss.
 
Tatu

Tatu

JF-Expert Member
Joined
Oct 6, 2006
Messages
1,079
Likes
38
Points
145
Tatu

Tatu

JF-Expert Member
Joined Oct 6, 2006
1,079 38 145
Naona JK anajiwekea ushahidi ICC kwamba ali-react na serikali yake pia haihusiki na unyama huo. Lakini kwa mtu mwenye akili anajua moja kwa moja serikali ya JK inahusika kwa namna moja au nyingine. Katika chaguzi zote zilizofanyika mwisho wa wiki, iweje viongozi na wafuasi wa chadema tu ndio washambuliwe?

Haiingii akilini hata kidogo. Ni watu kama wakina Nape wanaojaribu kujiona wako juu ya sheria ndio wanaweza kusema Chadema wamejishambulia wenyewe.
 
DOUGLAS SALLU

DOUGLAS SALLU

JF-Expert Member
Joined
Nov 13, 2009
Messages
16,522
Likes
9,325
Points
280
DOUGLAS SALLU

DOUGLAS SALLU

JF-Expert Member
Joined Nov 13, 2009
16,522 9,325 280
Naona JK anajiwekea ushahidi
ICC kwamba ali-react na serikali yake pia haihusiki na unyama huo.
Lakini kwa mtu mwenye akili anajua moja kwa moja serikali ya JK
inahusika kwa namna moja au nyingine. Katika chaguzi zote zilizofanyika
mwisho wa wiki, iweje viongozi na wafuasi wa chadema tu ndio
washambuliwe?

Haiingii akilini hata kidogo. Ni watu kama wakina Nape wanaojaribu
kujiona wako juu ya sheria ndio wanaweza kusema Chadema wamejishambulia
wenyewe.
JK hata aruke sarakasi gani yeye na mahenchmen wake lazima wataishia jela
 
U

ungonella wa ukweli

JF-Expert Member
Joined
Mar 27, 2012
Messages
4,214
Likes
1
Points
0
U

ungonella wa ukweli

JF-Expert Member
Joined Mar 27, 2012
4,214 1 0
Mwigulu anajua vizuri juu ya kuhusika kwake huko arusha kwenye tukio la bomu!
 
C

chama

JF-Expert Member
Joined
Aug 6, 2010
Messages
8,005
Likes
17
Points
0
C

chama

JF-Expert Member
Joined Aug 6, 2010
8,005 17 0
nngu007
Ni kibaya kipi alichosema Nape Nnauye? nyie hamtaki kuelezwa ukweli lakini huo ndio ukweli wenyewe!
 
Last edited by a moderator:
mwekundu

mwekundu

JF-Expert Member
Joined
Mar 4, 2013
Messages
21,031
Likes
10,394
Points
280
mwekundu

mwekundu

JF-Expert Member
Joined Mar 4, 2013
21,031 10,394 280
Nape,Mwigulu ndo wanajua walichokifanya ndo mana wanajihami na propaganda-mwisho wa yote ni aibu na umauti damu za watu hazipoteagi bure

Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums
 
A

Apollnary

JF-Expert Member
Joined
Mar 5, 2011
Messages
209
Likes
1
Points
0
Age
59
A

Apollnary

JF-Expert Member
Joined Mar 5, 2011
209 1 0
Nguu07 bwana una mambo ya ajabu sana
Nilipoona uchambuzi wako nikajua Nnape kaongea maneno ya ajabu sana
Ninamaliza kusoma ulichosema Nnape kasema,naendelea kukushangaa ulivyo bi standard katika analysis yako kama unavyofanya kila siku...

Ujue Nnape ni SIASA pia
na Kikwete ni SERIKALI
na hao wawili,wana semi autonomy ya kutamka maneno

Lakini all ina all.wote wawili wametamka maneno ambayo hayana "maudhi" kama ulivyojaribu ku potray wewe
 
S

sir.ben

JF-Expert Member
Joined
Feb 14, 2013
Messages
389
Likes
0
Points
33
S

sir.ben

JF-Expert Member
Joined Feb 14, 2013
389 0 33
nngu007
Ni kibaya kipi alichosema Nape Nnauye? nyie hamtaki kuelezwa ukweli lakini huo ndio ukweli wenyewe!
kwamba mamako anamshkaj mwingine?
 
Last edited by a moderator:
Nguruvi3

Nguruvi3

Platinum Member
Joined
Jun 21, 2010
Messages
13,005
Likes
9,153
Points
280
Nguruvi3

Nguruvi3

Platinum Member
Joined Jun 21, 2010
13,005 9,153 280
Wale mnaosema huu ni wakati wa vijana naomba mfikirie tena.

Kauli za Nape si za kiungwanahata kidogo. Huu ni msiba mkubwa kwa taifa.
Sidhani kuna mtoto anaajua siasa ni nini. Na hata kama anajua kuna ubaya gani yeye kushiriki shughuli za kisiasa kama mtu anayejifunza?

Leo Nape anatumia damu za watoto hao na raia wengine wasio na hatia kutangaza habari za siasa.
Lile bomu lingeangukia na kuua viongozi wa CDM sijui kama angesema limepangwa.

Nape labda tukukmbushe haya
1. Mwakyembe kutaka kuuawa na kutaja hadi wahusika tukio lile lilipangwa na nani?
2. Mengi na mtoto wake kuwekewa mtego, tukio lile lilipangwa na nani?
3. Ulimboa kung'olewa kucha na meno tukio hilo lilipangwa na nani?
4. Mwangosi kutolewa roho, tukio hio lilipangwa na nani?
5. Kibanda kung'olewa meno na jicho, tukio hilo limepangwa na nani?
6. Mbwambo kuchinjwa kwa msumeno kule Tengeru, tukio hilo lilipangwa na nani?
7. Kule Igunga mtu kutoweka, tukiolilipangwa na nani?

Orodha ni ndefu na katika matukio yote hayo hakuna majibu hadi sasa.
Si chama au serikali ya chama chako imewahi kutolea majibu. Majibu ni upepo utapita.

Nape wewe unaishi Tanzania, na nyadhifa zako pamoja na maisha yako ni kwasababu upo Tanzania .
Yakitokea yasiyotarajiwa na yasiyo ombewa si wewe si mimi au yule atakayekuwa salama.
Hakuna shujaa kati kati ya vita na vurugu

Nakusihi sana mdogo wangu iangalie Tanzania kwanza halafu ndipo uangalie mambo mengine.
Unaandika kwa jeuri na dharau kwasababu upo ndani ya Tanzania iliyotulia na inayolekea kuchafuka.

Kwanini kijana wa umri wako unafikia mahali pa kujisahau namna hiyo?
Kama Nyerere alisema CCM si mama yake, wewe ni nani nakwa uwezo upi unadhani CCM ni bora kuliko roho za Watanzania wasio na hatia.

Hivi wanajamvi, hawa ndio vijana tunaowapigia debe waliongoze taifa kweli!
Kama Nape kasema hivi nani kabaki na kabaki na busara ipi?

Nape, ubinadamu ni bora kuliko bendera za chama. Utangulize ubindamu na usilewe na dunia hii.

Leo unaona roho za watu na damu zao ni nyepesi kwasababu una rungu, umesahau kuwa unaishi ndani ya nyumba ya glass.

Mungu akusadie uone kile uischokiona sasa hivi, na heri ya kukaa kimya ili watu wawe na shaka nawe kuliko kuongea na kuwatoa mashaka waliyokuwa nayo juu yako.
Bado ni mdogo Nape, tuulize tumeyaona mengi, tumewaona wafalme wakipaa na kuanguka.
 
utaifakwanza

utaifakwanza

JF-Expert Member
Joined
Feb 1, 2013
Messages
14,153
Likes
1,784
Points
280
Age
49
utaifakwanza

utaifakwanza

JF-Expert Member
Joined Feb 1, 2013
14,153 1,784 280
Chadema ni watekelezaji wa hili tukio, waache usanii
 
utaifakwanza

utaifakwanza

JF-Expert Member
Joined
Feb 1, 2013
Messages
14,153
Likes
1,784
Points
280
Age
49
utaifakwanza

utaifakwanza

JF-Expert Member
Joined Feb 1, 2013
14,153 1,784 280
Naunga mkono maneno ya nape.
 
Communist

Communist

JF-Expert Member
Joined
Jun 1, 2012
Messages
5,382
Likes
43
Points
135
Communist

Communist

JF-Expert Member
Joined Jun 1, 2012
5,382 43 135
Sidhani kama huyu jamaa yuko sawa kichani. Ngoja tuone mwisho wake.


Nape labda tukukmbushe haya
1. Mwakyembe kutaka kuuawa na kutaja hadi wahusika tukio lile lilipangwa na nani?
2. Mengi na mtoto wake kuwekewa mtego, tukio lile lilipangwa na nani?
3. Ulimboa kung'olewa kucha na meno tukio hilo lilipangwa na nani?
4. Mwangosi kutolewa roho, tukio hio lilipangwa na nani?
5. Kibanda kung'olewa meno na jicho, tukio hilo limepangwa na nani?
6. Mbwambo kuchinjwa kwa msumeno kule Tengeru, tukio hilo lilipangwa na nani?
7. Kule Igunga mtu kutoweka, tukiolilipangwa na nani?
 
utaifakwanza

utaifakwanza

JF-Expert Member
Joined
Feb 1, 2013
Messages
14,153
Likes
1,784
Points
280
Age
49
utaifakwanza

utaifakwanza

JF-Expert Member
Joined Feb 1, 2013
14,153 1,784 280
Chadema siku zenu zinahesabika, hamuwezi kuwa mnasababsha damu kuwagika kila siku bana
 
Communist

Communist

JF-Expert Member
Joined
Jun 1, 2012
Messages
5,382
Likes
43
Points
135
Communist

Communist

JF-Expert Member
Joined Jun 1, 2012
5,382 43 135
Chadema siku zenu zinahesabika, hamuwezi kuwa mnasababsha damu kuwagika kila siku bana
Jumlisha idadi ya kura halafu utajua kinachoendelea. Na tunangoja hilo daftari ndio utaelewa vizuri.
 
B

buluwaya

JF-Expert Member
Joined
Feb 15, 2013
Messages
207
Likes
0
Points
33
Age
39
B

buluwaya

JF-Expert Member
Joined Feb 15, 2013
207 0 33
nngu007
Ni kibaya kipi alichosema Nape Nnauye? nyie hamtaki kuelezwa ukweli lakini huo ndio ukweli wenyewe!

Una hamu ya Ukweli kuhusu nini wewe. Kuhusu huyu Nape?Huu hapa ukweli sasa: Nape form six Private Candidate. Kisomo cha kuunga-unga. Hana akili kihiiiivyo!
Hatuwezi kusema hana akili kabisa, lakini tunaweza kusema CCM ina watu bora kuliko yeye.
Hajui Propaganda ni taaluma ya kusomea. Haijui inafanywaje. Kasomea wapi? Kigamboni alikoenda kusoma kwa kubebwa?

Mbona Waalimu wa hilo somo kina Paul Sozigwa hawapo tena! CCM tokeni madarakani kwa amani jamani. Mstafute kutoka na roho za watu.
 
Lady doctor

Lady doctor

JF-Expert Member
Joined
Apr 13, 2013
Messages
8,762
Likes
64
Points
0
Lady doctor

Lady doctor

JF-Expert Member
Joined Apr 13, 2013
8,762 64 0
Nimeipenda sana kauli ya Mh. Raisi ila huyu Nape mbona mropokaji hivyo ana uhakika gani kwamba Chadema ndio wamepanga hilo tukio la kigaidi?

Ccm kuweni makini na Nape atawapoteza mazima kwasababu kauli zake hazina mantiki yoyote
 
T

tusichoke

JF-Expert Member
Joined
Apr 2, 2011
Messages
1,294
Likes
9
Points
135
T

tusichoke

JF-Expert Member
Joined Apr 2, 2011
1,294 9 135
Tatizo nape anadhani kuwa ccm ndio deal,kwanza 2015 anapotea kwenye ramani si tu ya tanzania bali hata ndani ya ccm.
 

Forum statistics

Threads 1,273,084
Members 490,268
Posts 30,470,668