Taarifa ya Vyama vya Siasa ya Kuhitimisha maombolezo ya Hayati Rais Magufuli

Huyu alikubalika na Watanzania wengi na alichukiwa na Majizi na Mafisadi. Ni rahisi hivyo. Msiba wake umedhihirisha hilo kwa vitendo na ikabidi ubuniwe mkakati wa kumpska mwenda zake mafuta ya oil chafu kwa wenye hofu. Ni rahisi kama hivi tu.
Wengi walienda kuhakiki Kama kweli kafa. Full stop.
 
Wengi walienda kuhakiki Kama kweli kafa. Full stop.

Na mwili wa mwenda zake ukazungushwa kuacha Nuru kwa Taifa na Nuru hii itaendelea kung'ara Bara na Visiwani, ndani ya CCM wakitaka na ikibidi nje ya CCM wasipotaka. Iko available kwa Watanzania wote kuitumia kama mtaji wao mahususi wa kisiasa.
 
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
  • Ndugu wana habari karibuni katika hiki kikao.
  • Ndugu wasikilizaji kupitia wana habari waliopo hapa karibuni.
  • Umma wa wasikilizaji kupitia hivi vyombo vya habari nanyi nasema karibuni.

YAH; TAFAKARI MAALUM YA KUHITIMISHA KIPINDI CHA MAOMBOLEZO YA KITAIFA YA TOKA TAREHE 17 MACHI 2021 YA ALIYEKUWA RAIS WA AWAMU YA TANO YA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA HAYATI DKT JOHN POMBE JOSEPH MAGUFULI NA SALAM MAHSUSI ZA PONGEZI NA HONGERA KWA RAIS WA SITA WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA MHE MAMA SAMIA SULUHU HASSAN.
  • Ndugu wana habari.
  • Ndugu watanzania wenzangu mliopo hapa
  • Umma wa wasikilizaji kupitia hivi vyombo vya habari

Awali ya yote naomba kumshukuru Mwenyezi Mungu mwingi wa Rehema kwa kutujalia Baraka zake na kutujalia uhai. Tupo hapa tunazungumza tukiwa wote salama Siku ya leo ya kuhitimisha maombolezo ya hayati Dkt. John Pombe Joseph Magufuli

Leo ni siku muhimu sana ya kuhitimisha kipindi cha maombolezo ya kitaifa ya toka Tarehe 17 machi 2021 hadi leo Tarehe 06 Aprili 2021 ya kuhusu msiba wa aliyekuwa ni Rais wa awamu ya tano ya Jamhuri Ya Muungano wa Tanzania hayati Dkt. John Pombe Joseph Magufuli.

Na kwa umuhimu wa pekee, vilevile hii ni siku rasmi ya kuhitimisha utolewaji wa salamu za pole kwa Mhe Rais wa
sita wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na vilevile ni siku adhimu ya kumpongeza huyu Mhe Rais wetu mama Samia Suluhu Hassan.

Kwa kuwa alitakalo Mola ndilo humfika Binadamu na kwa kuwa sote tumetoka kwa mwenyezi Mungu na kwake tutarejea. Kwa hiyo sasa, watanzania tuendelee kumuombea kwa mwenyezi Mungu Pepo Ya ahela iwe daima naye hayati Dkt. John Pombe Joseph Magufuli

Kwa uzito maalum wa utamaduni wa mila na jadi za utu na ubinadamu, watanzania wa mapenzi mema tuendelee kuiombea familia ya mjane Mhe. mama Janeth Joseph Magufuli.

Mwenyezi Mungu adumishe subira katika kipindi chote cha mapitio ya huzuni kubwa waliyonayo hii familia ya hayati Dkt. John Pombe Joseph Magufuli.

Mhe. mama Janeth Joseph Magufuli, watanzania wa mapenzi mema sote tunakupenda sana na daima tutakuenzi kwa sala na Dua. Pole sana kwa kuondokewa na Rafiki ambaye alikuwa ni ndugu yako na mwenzako sana na alikuwa ni zawadi yako kutoka kwa Mwenyezi Mungu naye ni hayati Dkt. John Pombe Joseph Magufuli.

Kwa niaba ya familia yangu na kwa niaba ya chama changu cha ADA-TADEA, Na vivyo hivyo kwa niaba ya Dhamana ya Uongozi wangu wa kiti cha Baraza la vyama vya siasa Tanzania, kwa heshima na kwa unyenyekevu mkubwa natoa pole kwa huzuni kubwa iliyopo kwa familia yako na kwa Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Mhe mama Samia Suluhu Hassan.

Ndugu wana habari,
Ndugu watanzania wenzangu,

Mhe Rais wa awamu ya tano hayati Dkt. John Pombe Joseph Magufuli leo tunakamilisha maombolezo ya kifo chake kilichotokea Tarehe 17 Machi 2021.

Miongoni mwa mambo makuu yatakayoliliwa na kukumbukwa ni haya yafuatayo;

Hayati Dkt. John Pombe Joseph Magufuli, kwanza naomba ikumbukwe kwamba, huyu Mheshimiwa alikuwa ni Binadamu, na kwa kuwa sote sisi Binadamu siyo watu wakamilifu kwa kauli na matendo yetu hayawezi kukosa kasoro za mapungufu ya kukwazana hapa Duniani. Kwa hiyo sasa, kwa kuwa ni Thawabu kwa Mwenyezi Mungu kunena mema ya marehemu wote na kwa hiyo sasa, naomba kusema machache ya kumbukizi za wema wa utumishi wake wa kipindi cha kutumikia kiti cha Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Naomba itoshe niseme machache nayo ni haya yafuatayo;
A. Hayati Rais Dkt. John Pombe Joseph Magufuli ametuachia umaana wa kufutwa dhana katili iliyokuwa inadhuru na kudhulumu umaana wa ndoto ya Taifa letu, ndoto ya Uhuru ni maendeleo kwa ustawi wa Jamii, Uchumi na Taifa.

B. Hayati Dkt. John Pombe Joseph Magufuli kaondoka Duniani akiwa amedhibiti dhana potofu na ovu ya kuwa sisi ni Nchi ya Taifa la kujengwa na wenye Moyo na kuliwa na wenye meno, hususani wenye mirija ya unyonyaji wa mali na Rasilimali za Nchini kupitia watu potofu wa ndani ya Nchi na watu wa nje ya Nchi.

C. Hayati Rais Dkt. John Pombe Joseph Magufuli alijipambanua kuwa ni kiongozi wa vitendo dhahiri vya sifa ya kuitwa ni kiongozi wa vitendo vya ngao kinga dhidi ya vishawishi vya aina zote za utamu wa itifaki dhulumati. Itifaki dhulumati ni zile za mizimu ya kutengeneza giza la kuduwaza na kudumaza

D. na kupofusha misimamo sahihi ya uzalendo wa wajibu wa kutetea maslahi ya Taifa kupitia kiti cha Urais wa Nchi ya Taifa laTanzania.

E. Hayati Rais Dkt. John Pombe Joseph Magufuli katuachia utumishi wa fikra zilizopigwa msasa na kaacha masomo ya maangalizo ya kuundwa na Nasaha zisemazo kwamba;

i. Tanzania hakuna mtu wa kutoka nje ya Serikali ya umma wa watanzania wazalendo na watiifu atakuja aseme ana Imani za kutenda misaada ya kuwezesha kukombolewa Taifa letu.

ii. Na kwa hiyo sasa, Tanzania hakuna mtu wa kutoka nje ya Serikali ya umma wa watanzania anayeweza kusema kuwa ana upendo na kwamba ana huzuni ya kujifikirisha na ajitume kwamba katoka nje ya Nchi kuja kuondoa

madhila ya Tanzania. Madhila ya maadui Umasikini, maradhi na ujinga kwa Jamii na kwa Taifa letu la Tanzania. Marehemu katuusia sana tujigundue na tujifahamu Tanzania itajengwa na watanzania wenyewe.

F. 1. Na kwa hiyo sasa, wananchi tujifahamu kwamba, Tanzania ukombozi wake hautowajibikiwa kifikra na hautowajibikiwa kwa vitendo au kimtazamo okovu na Taassisi za nje ya Taifa letu.

2. Aidha katusomesha na kutuacha na maono ya Hekima ya kuongoza Busara zetu zitambue kwamba mtegemea cha Ndugu hufa masikini.

3. Na kwa hiyo sasa, misaada ya kutoka nje ya Nchi yetu ni mfano wa vikolezo kama hamira za unga wa maandazi. Kwa hiyo sasa, hii misaada tuipokee kwa dhana ya kuwa

kwamba ni vichocheo vya kurutubisha palipo na maumivu yetu ya leo ambayo nimaumivu mema. Maumivu ya leo ni kwa faida ya kuwa na maisha ya furaha na ya Riziki ya kutosha kwa kesho yetu na ya vizazi na vizazi.

G. Hayati Rais Dkt. John Pombe Joseph Magufuli amemaliza wajibu wake hapa Duniani. Taifa kaliacha na serikali na sisi wananchi katuacha tumekanyika tuwe na misimamo thabiti ya kukataa vishawishi vya itifaki za Chui waliovaa Ngozi za kondoo, kumbe hawa Chui wana nia ovu na nia katili ya kudhuru na kudhulumu Maisha ya furaha na ya Heshima za utu na Uhai wa Binadamu wa Tanzania.

H. Kwa hiyo sasa, hayati Rais Dkt. John Pombe Joseph Magufuli kifikra na vitendo, tumuenzi na awe hai tuendeleze Imani ya Uhuru ni kazi.

I. 1. Ikumbukwe kwamba, gharama ya kuwa nchi Huru ni kufanya kazi kwa imani ya kusadiki kwamba mumivu ya leo ni kwa furaha ya kesho

2. Na kwa hiyo sasa, Tunuku zake tuzizawadie kwa kukubali Rais wa sita wa Tanzania Mhe Mama Samia Suluhu Hassan inapopasa kuwa kwamba atunyweshe dawa chungu tuwe tayari kuinywa na tupongeze anatupatia tiba salama kwa Maendeleo ya Nchi yetu.

J. Watanzania wa mapenzi mema wote, Naomba tumuunge mkono huyu mama mwendelezaji wa mapambano ya Uhuru ni kujitegemea. Hivyo tuwe macho dhidi ya mifumo ya Tabia za Michwa ambao hupukutisha nguzo kimyakimya.

K. Watanzania na kwahiyo sasa, tuimarishe Umoja na mshikamano wa kushinda Utapeli wa panya-Watu wa kuuma na kupuliza. Watanzania tukatae utapeli wa watu wa kughushi usamaria wa Wema Bandia. Tuzibe mifereji ya kutoroshea maslahi ya Jamii na Taifa. Wote tuwe bega kwa bega na Mhe Rais wetu mama Samia Suluhu Hassan.

L. Mhe Rais Mama Samia Suluhu Hassan, Apewe Hongera sana kwa kuwa muumini wa safari ya Nyayo za waasisi wa Taifa hili. Mungu mwingi wa Rehema akupe kinga ya Malaika wake.

M. Mhe Rais Mama Samia Suluhu Hassan,
Ikubalike ujio wake ni Ari mpya na ni chachu ya kuzimua kukomboana kifikra sisi kwa sisi – wewe ndio Darubini ya kuchanganua na kupambanua tulikotoka, tulipo na Tuendako.

Ndugu wanahabari,
Ndugu watanzania wenzangu mliopo hapa,
Umma wa wasikilizaji kupitia hivi vyombo vya habari.


1. Kwa kuwa Taifa letu lipo katika mazingira mapya ya uongozi wa Serikali ambao sasa ni wa awamu ya sita ya Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan. Kwa hiyo basi nami sambamba na kutoa pole kwa ajili ya hili hitimisho la maombolezo.

2. Nachukua fursa hii nami niseme machache ya pongezi maalum kwa hatua mtambuka zilizotekelezwa na hii Serikali ya awamu ya sita ya Mhe. Rais Mama Samia Suluhu Hassan.

3. Maelezo ya mchango wa maoni yangu kwa Serikali ya awamu ya sita yatahusu wito maalum kwa watumishi wa Serikali hii.

4. Natoa wito maalum wa kuhimiza viongozi na watumishi wa Serikali hii waunge mkono kwa vitendo utashi wa nia ya ujumbe wa hotuba ya kwanza ya Mhe. Rais Mama Samia Suluhu Hassan, kuapa kuwa Rais wa sita wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania.

5. Na kwa hiyo sasa, viongozi na watumishi wa Serikali ya awamu ya sita wa Dhamana mtambuka na waasa kwamba.,

6. Ungeni mkono kwa kauli na matendo Dira ya Taifa ya kuhusu nia ya utawala bora iliyotambulishwa na ujumbe Rasmi wa hotuba ya baada ya Mhe. Samia Suluhu Hassan kuapa kuwa Rais wa sita wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania tarehe 19 Machi, 2021.

7. Mhe Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania mama Samia Suluhu Hassan, kwa kuwa kupitia hotuba yake kwa jamii na kwa Taifa ametangaza makusudio yake ya kuwa kwamba, nukuu:-

Huu ni wakati wa kuzika tofauti zetu na kuwa wamoja kama Taifa, kufarijiana kuonyesha upendo, undugu wetu, kudumisha Amani yetu kuenzi utu wetu, uzalendo wetu na utanzania wetu. Alinena haya tarehe 19 Machi, 2021.

8. Kwa hiyo sasa, nawasihi washauri wa vyeo vya dhamana za utumishi wa kusimamia mahusiano ya kati ya wadau wa vyama vya siasa na mamlaka mtambuka ya dhamana za serikali; sasa tengenezeni mfumo rafiki wa kuunda mawasiliano ya kuondoa changamoto za kugonganisha nia njema na ambayo ni wito kwa utashi wa kutekelezwa kwa dhima ya matakwa ya kuwa kwamba tuzike hasama za kati ya Tasnia ya siasa na mamlaka ya serikali.

9. Na kwa kuwa siasa ni matope na mtu akicheza na tope anachafuka, kwahiyo sasa serikali ioteshe mizizi inayozaa haki na usawa. Mzizi wa Amani, Upendo na mshikamano wa kati ya Tasnia ya siasa na mifumo mtambuka ya dhana ya kuitwa ni mzizi uitwao haki na usawa.

10. Viongozi wa serikali na wasimamizi wa Haki za Demokrasia ya vyama vingi, mfumo ambao chimbuko lake Kitaifa ni wito wa Hayati Baba wa Taifa Mwl. J.K. Nyerere. Na kwa kuwa uongozi mkuu wa serikali ya awamu ya sita una utashi wa nia ya dhamiri njema ya sawa na Hayati Baba wa Taifa Mwl. J.K.Nyerere, ya kuhusu kudumisha Amani na Utulivu wa Kitaifa. Na kwa kuwa hii ndiyo Dira ya kauli ya Mhe. Rais Mama Samia Suluhu Hassan.

11. Kwa hiyo sasa watumishi wa serikali epukeni vitendo hasi vya kwenda kinyume na hii Dira yenye ufanikishaji kwa umaana wa hotuba yenye agizo la tarehe 19 Machi, 2021 la Mhe. Rais Mama Samia Suluhu Hassan.

12. Kwa mtazamo wangu nadiriki kusema kwamba Tasnia ya siasa na wadau wake tupo tayari kushirikiana na serikali katika kudumisha Amani, Upendo na mshikamano wa kushauriana na kukosoana sisi kwa sisi watanzania. Hii iwe ni badala ya baadhi ya wadau wa siasa kutumia marafiki wa Tanzania wa Nchi za nje wawe ndio sikio sikivu kwa maumivu ya wavaa viatu vya siasa za Tanzania.

13. Kwa umuhimu wa pekee kipaumbele cha kwanza cha kuotesha fumbuzi za kuondoa kusigana kwa kati ya wadau wa vyama vya siasa na mamlaka za Dola sasa pawepo vikao vya Baraza la vyama vya siasa. Hivi vitendeke kwa mujibu wa sheria na kanuni za vyama vya siasa Tanzania.

14. Ipambanulike kwamba, rekebisho kwa kasoro ya kukosekana vikao vya Baraza, hii ni fursa ya kuotesha ishara njema ya kipandio cha kujenga kuundika hali na sababu za kusadikika vema, nia ya serikali ya awamu ya sita katika ufufuaji uhai wa Demokrasia ya vyama vingi hapa Tanzania.

15. Kwa hiyo sasa, watumishi wa serikali na viongozi wa serikali sasa pandisheni viwango vya sifa za kukweza umaana wa Tanzania ina mfumo wa vyama vingi na ni vinavyopatiwa haki zote za Katiba ya Nchi yetu.

Ndugu wanahabari,
Ndugu watanzania wenzangu mliopo hapa,
Umma wa wasikilizaji kupitia hivi vyombo vya habari kero ya wafanya Biashara.


16. Kwa kuwa kuvunjika jembe siyo mwisho wa Uhunzi na kipimo cha jembe jipya ni shambani.
Nami napenda nisiwe mchoyo wa fadhila za kupongeza utumishi wa serikali hii yenye utashi wa nia ya kuondoa kero katili zilizo dhuru na kudhulumu Haki za mali asili za mapato ya wafanya biashara.

17. Napenda kuunga mkono wito wa Waziri wa fedha Mhe. Dkt Mwigulu Nchemba wa mbiu ya wito wa rudisheni pesa Benki.

18. Nachukua fursa hii kuchangia ushauri ufuatao kwa Mhe. Waziri wa mipango na fedha na kwa mwanasheria mkuu wa serikali ya Jamhuri ya muungano wa Tanzania

19. Nawashauri hawa viongozi waibue uvumbuzi wa kisheria wa kusadikisha dhamiri njema za serikali za kulinda maslahi ya kati ya Benki na mteja anayeweka pesa zake Benki.

20. Maneno matupu hayavunji mfupa na aliyeumwa na nyoka kila mtikisiko wa jani hauishi hofu.

21. Na kwa umuhimu wa pekee ni vema serikali ikatoka hadharani pamoja na Tume ya maadili. Hapa watangaze mjengeko wa utaratibu wa mfumo wa Tume. Tume hii ihakiki visingizio vya kuhusu madhila yote yaliyotendeka.

22. Taifa linahitaji osho la kuondoa uchafu wote wa kanuni potofu na ovu zilizohasi haki za watanzania kumiliki haki za mapato halali ya kuitwa ni pesa za wafanya biashara. Ikumbukwe kwamba wafanyabiashara ndio sumaku ya kuvutia wawekezaji wa kutoka nje ya Nchi ya Tanzania.

23. Wizara ya mipango na fedha na mwanasheria mkuu wa serikali vumbueni mfumo wa sheria ya kukuza msisitizo wa Imani na staha kwa Haki za pesa za wafanya biashara.

24. Tanzania kuwepo kwa hali na sababu inayodhoofisha kukua kwa Kampuni za wananchi ambao ni wawekezaji wazalendo huwa ni kukosekana kwa mfumo wa uwezeshaji kulipwa madeni ya mitambo ya kutoka Nchi za nje.

25. Kodi ya VAT inadhoofisha sana uchangamfu wa biashara nyingi, hivyo Wizara ya kilimo na wizara ya Uwekezaji na wizara ya Fedha, hawa kundi viongozi bila kuwa na makutano ya fikra ya kuunda umoja wa sheria rafiki ya kukuza wafanya biashara, yaani sisi Nchi yetu itakuwa na hali ya mdororo kwa kukua kwa biashara za kuongeza kipato kwa Taifa.

26. Hali iliyopo hivi sasa ni uwepo wa mfumo uliodumaa bila utanuzi wa wigo kwa kuongezeka viwanda.

27. Hali hii inasitisha kuongezeka kwa ajira za kuzaliwa na viwanda mama vilivyopo vya wengi wa wazalendo.

28. Mhe. Rais Mama Samia Suluhu Hassan, nampongeza kwa kuwa ngao kinga dhidi ya Umma kukata tamaa na dhidi ya Umma kupoteza matumaini kwa uendelevu wa kupatikana matokeo chanya kwa ustawi na maendeleo ya Jamii, uchumi na Taifa.

29. Napongeza matendo ya serikali ya chini ya usimamizi wa Rais wa awamu ya sita. Matendo haya ni uamusho mpya unaokweza morali na kukuza ari mpya ya Umma kuwa ni rafiki na serikali hii ya Mhe. Rais Mama Samia Suluhu Hassan.

30. Mhe. Rais Mama Samia Suluhu Hassan nampa hongera sana kwa hatua zake zote alizoelekeza zitimizwe na utumishi wa awamu ya serikali yake.
Wahenga husema bila kufungua gamba la kitabu huwezi kujua kilichomo ndani ya maandishi ya kitabu. Ni kweli ujio wake ni zinduko la mbinu mpya kwa kuundika maisha ya furaha kwa watanzania wote.

31. Nampa hongera sana kwa uongozi wake wa mfumo wa osho la kung’arisha uwajibikaji wa serikali kupitia matumizi bora ya mamlaka ya kiti chake cha sifa zake za utawala bora.

32. Tahadhari za kuzuia mazalio ya hoja za kisiasa dhidi ya serikali ya awamu ya sita.

(a) Watumishi wa Umma ongezeni viwango bora vya kutoa huduma kwa haraka na huduma zikidhi matarajio ya Umma uliozoea kupokea huduma zenye vitendo adilifu.

(b) Umma unamwitikio mwema na ni mwitikio rafiki wenye matarajio ya kuendelea kupokea huduma bila tozo za Rushwa.

(c) Kwa hiyo sasa watoa huduma kwa Jamii kuweni na kauli adilifu ziwe za kukweza mshikamano wa Umma na Dhamiri njema za Rais wa sita Mhe. Mama Samia Suluhu Hassan.

33. Mhe. Rais mama Samia Suluhu Hassan hongera sana kwa kusindikiza maombolezo ya huu msiba mkubwa kwa kuwa na uongozi wa kauli na matendo ukombozi kwa uokovu wa maslahi ya kujengeka ustawi na maendeleo ya Jamii, Uchumi na Taifa.

34. (a) Hongera sana kwa utendaji thabiti wenye misimamo madhubuti yenye kukweza miiko ya Dira ya safari ya mabadiriko yaliyoleta mageuzi toka mwaka 2015.

(b) Haya mageuzi ni yaliyoundwa na uwajibikaji pacha wa awamu ya tano nayo ni ya kuongozwa na Hayati Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akiwa na changio la Baraka zako Mhe. Rais mama Samia Suluhu Hassan.

35. Mhe. Rais mama Samia Suluhu Hassan huyu ni kiongozi mbora na mbobezi kwa ujenzi wa fumbuzi za kuunda makutano ya kati ya fikra za wadau wa vyama vingi na umaana wa hekima ya ujumbe wa hotuba yake ya tarehe 19 Machi,2021.

36. Kwa hiyo sasa natumia fursa kuomba siku ikikupendeza utuite viongozi wa Baraza la Vyama vya siasa Tanzania tuje kupokea nasaha zako.

37. Mhe. Rais mama Samia Suluhu Hassan hotuba yako ya kwanza tayari imeandikisha maono sahihi katika fikra za wadau wa tasnia ya siasa na imedhibiti mitazamo ya kuhasimiana kati ya serikali na wadau wa Vyama vya siasa.

38. Mwenyezi Mungu mwingi wa Rehema amjalie afya njema Mhe. Rais mama Samia Suluhu Hassan.

39. Watanzania tuendelee kumuomba Mwenyezi Mungu ampe Pepo ya Ahera Hayati Dkt. John Pombe Joseph Magufuli, mwanga wa milele umuangazie na apumzike kwa Amani ahera marehemu Dkt. John Pombe Joseph Magufuli Amen.


Ahsanteni kwa kunisikiliza.


Ndimi

John Paul Shibuda
Katibu Mkuu wa Chama cha ADA – TADEA
NA
Mwenyekiti
Baraza la Vyama vya siasa Tanzania.
Too long I didn't even read it baada ya kuona ni huyu shibuda
 
Na mwili wa mwenda zake ukazungushwa kuacha Nuru kwa Taifa na Nuru hii itaendelea kung'ara Bara na Visiwani, ndani ya CCM wakitaka na ikibidi nje ya CCM wasipotaka. Iko available kwa Watanzania wote kuitumia kama mtaji wao mahususi wa kisiasa.
Kuna makundi mawili ya nuru. Nuru ya watu wasiojielewa kama hao uliowataja na wale wenye uelewa ambao hawaamini kitu kijingajinga.
 
Back
Top Bottom