Taarifa ya utekelezaji wa agizo la kukata umeme kwa wadaiwa sugu

mzee wa mkeka

Senior Member
Mar 12, 2017
142
236
Habari wadau wa jukwaa hili adhimu;

TANESCO yaanza operesheni ya kuwakatia umeme wadaiwa sugu zikiwemo taasisi za serikali.

Shirika la umeme nchini TANESCO limeanza operesheni ya kuwakatia umeme wadaiwa sugu zikiwemo taasisi za serikali ikiwa ni utekelezaji wa agizo la Rais Magufuli alilotoa hivi karibuni.

Kaimu meneja uhusiano wa TANESCO Bi Leila Muhaji amesema zoezi hilo limeanza nchi nzima na kuongeza kuwa shirika hilo lilitoa muda wa siku kumi na nne wadaiwa wawe wamelipa madeni yao lakini hadi leo wapo ambao bado wako kimya.

Baadhi ya wananchi wamekuwa wamekuwa na maoni tofauti juu ya suala hilo huku wengine wakiishauri tANESCO kufungia taasisi za serikali luku ili waweze kulipa kadiri wanavyotumia.

Licha ya uwepo wa madeni hayo ambayo TANESCO inadai yanasababisha wajiendeshe kwa hasara, taarifa ya mdhibiti na mkaguzi mkuu wa hesabu za serikali iliyokabidhiwa kwa rais inaeleza kuwa shirika hilo linajiendesha kwa hasara ambapo linanunua umeme shilingi 544 kwa unit lakini inauza kwa shilingi 279 kwa unit.

Hii ni thread maalum kwa ajili ya kukusanya taarifa za utekelezaji wa agizo la rais Magufuli kwa TANESCO la kukata umeme kwa wadaiwa wote sugu nchi nzima.
Hivyo yeyote mwenye taarifa ya KA_TA kwenye sehemu alipo aiweke hapa.
Asante kwa ushiriki wako.

UPDATES:

Taasisi zilizokatiwa umeme mpaka sasa:

-Mamlaka ya maji safi kigoma (KUWASA)

-Polisi kurasini - Dar

-Mamlaka ya maji kahama - shinyanga (KASHIWASA)

-Gereza la bukoba mjini - umeme umerudishwa

-
Kambi ya polisi buyekera - bukoba mjini

-Kambi ya magereza - bukoba mjini

-Mamlaka ya maji safi bukoba

-Mamlaka ya maji safi Tabora

-Mamlaka ya maji safi Musoma

-Mamlaka ya maji safi na maji taka shinyanga (SHUWASA)

-Mamlaka ya maji safi bukoba (BUWASA)
 
Dawa ya Deni ni kulipa ila Wadaiwa sugu ni Taasisi za Serikali kwa hiyo Serikali izilipie taasisi zake ili Tanesco ipate fedha ya kuipatia Serikali.Naona kama mzunguko usio na faida.
 
Kahama wamekata toka Jana na hatuna maji tunanunua ndoo mia5 hadi Elf1 noma sana
Binafsi naona ni utesaji wa wananchi, kama mteja wa mamlaka ya maji analipa ankara zake kwa muda sahihi sidhani kama ni busara kukatia umeme mamlaka na hatimaye mwananchi anayelipa ankara yake akose huduma ya maji.
Hapa inafaa kuwawajibisha watendaji wakuu wa mamlaka husika kwa kushindwa kutimiza wajibu wao
 
Tunateseka Kiukweli Hospital ya Wilaya maji Hakuna tanks za maji zinakaribia kuisha, nimetoka kuangalia hospital wodi ya Akina mama na watoto ni shida balaa Sijui2 namna ya kuweka picha ningewawekea ttzo kubwa ni watu wachache ktk hizi taasisi za umma pesa ya umeme Inalipwa na watu wanaingiza ktk miradi yao ili wapate faida ndo walipe sasa kwa Awamu hii ni balaa wanazikopa pesa na hakuna faida ndo kimbembe watumbuliwe2 watendaji
 
Poleni sana; ila kwa kiongozi anayeangalia kwa jicho la tatu hawezi kata umeme kwa mamlaka ya maji ambayo wateja wake wote wanalipa ankara zao kwa wakati, njia sahihi ni kuwatumbua mabosi wa mamlaka husika.
Gharama ya kukosa maji kwa taasisi nyeti kama taasisi za afya ni kubwa sana. Inabidi waziri wa afya aingilie kati.
Hali ikiendelea hivi wanaoenda hospitali watapata maambukizi mengine hapo hospitali, pia huduma za wazazi bila maji ni karaha tupu
 
Back
Top Bottom