Taarifa ya TANESCO ya kuomba radhi Mkoa wa Shinyanga, Wilaya ya Kishapu

viatu virefu

Senior Member
May 25, 2015
166
195
TAARIFA YA KUOMBA RADHI MKOA WA SHINYANGA, WILAYA YA KISHAPU
Shirika la umeme Tanzania Tanesco Mkoa wa Shinyanga linawaomba radhi wateja wake wote Wilayani Kishapu kwa kukosekana kwa huduma ya umeme kuanzia saa 9:00 alasiri.

Katizo hilo lilitokana na hitilafu kwenye transfoma inayohudumia mji wa Mhunze na hivyo kusababisha baadhi ya maeneo kukosa huduma ya umeme.
Maeneo yaliyoathirika ni baadhi ya maeneo ya Mhunze center, Shireccu kiwandani na pampu za maji.

Mafundi wa TANESCO wanaendelea na jitihada za kutatua tatizo ili kurejesha umeme haraka iwezekanavyo kwenye maeneo yote yalioathirika.

Tunaomba radhi kwa usumbufu wowote uliojitokeza.

KWA MAWASILIANO WASILIANA NA KITUO CHA HUDUMA KWA WATEJA
0787521070 ,0754521070, 028 276 2120, 0768 985 100 au 022 219 4400
Imetolewa na Ofisi ya Uhusiano TANESCO Makao Makuu
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom