Taarifa ya TANESCO: Katizo la umeme kwa baadhi ya mikoa iliyoungwa na gridi ya taifa 14February 2016

hakuna shida

Member
Dec 16, 2015
25
5
SHIRIKA LA UMEME TANZANIA






TAARIFA YA KUKOSEKANA KWA UMEME KWA BAADHI YA MIKOA ILIYOUNGWA KWENYE GRIDI YA TAIFA FEBRUARI 14, 2016

Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) linawatangazia wateja wake wa mikoa ya Singida, Shinyanga, Tabora, Mwanza, Musoma, Mara, Babati, Simiyu, Dodoma na baadhi ya maeneo ya mikoa ya Arusha, Kilimanjaro na Tanga kuwa yatakosa umeme siku ya JUMAPILI tarehe 14 FEBRUARI, 2016 kuanzia Saa 1:00 Asubuhi hadi Saa 11.00 Jioni.

Sababu ni kazi inayoendelea kufanywa na Mkandarasi anayejenga njia kuu ya kusafirisha umeme ya msongo mkubwa wa kilovoti 400, maarufu kama ‘Backbone’ kutoka Iringa kwenda Shinyanga.

Mradi huo unalenga kuimarisha hali ya upatikanaji wa umeme nchini na utekelezaji wake upo katika hatua za mwisho.

Uongozi unasikitika kwa usumbufu wowote utakaojitokeza.


Imetolewa na: OFISI YA UHUSIANO,
TANESCO - MAKAO MAKUU.
 
Hiii inamaaa hakuna valentine day mkafanye usafi majumbani kwenu nyumba zipumue

Cc.mshana jr
 
hawa watu ni wapuuzi kweli kwa hiyo tarehe 14 imeanza leo Kahama!!!!!! tulishazoea haina haja ya kutangaza, umeme wa Kahama kila baada ya dk 10 wanakata kurud masaa 6--8!!!!!!!!
 
Back
Top Bottom