Taarifa ya malinzi mchana huu

Taarifa ya malinzi mchana huu

Charles Mtekateka

JF-Expert Member
Joined
Feb 13, 2009
Posts
317
Reaction score
89


​
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI​
YAH: KUENGULIWA KWANGU KUGOMBEA URAIS WA TFF 2013​
Ndugu zangu,kupitia vyombo vyenu vya habari ninaomba niueleze umma wa watanzania,hususani wadau wa mpira wa miguu,yafuatayo kuhusu kuenguliwa kwangu. Awali ya yote nieleze kusikitishwa kwangu na maamuzi yaliyotolewa na kamati ya rufaa ya TFF ya kuniengua kugombea urais wa TFF.Sikubaliani na maamuzi haya . Katika kuniengua kamati ya rufaa ya uchaguzi ya TFF imetoa sababu mbili (nanukuu magazeti ya jana tarehe 12/02/2013 maana hadi leo sijakabidhiwa barua ya kuenguliwa). Kukosa uadilifu kwa kupinga waraka uliotolewa na TFF wa kubadili Katiba ya TFF mwezi Desemba 2012. Kukosa uzoefu wa miaka mitano ya uongozi. Ndugu zangu,kiini cha maamuzi ya Kamati ya rufaa dhidi yangu ni pingamizi lililowekwa na mtu mmoja anayeitwa AGAPE FUE.Bwana Agape Fue aliniwekea pingamizi katika kamati ya uchaguzi akidai mimi nilipinga waraka wa kubadili katiba ya TFF na pia sina uzoefu wa miaka mitano ya uongozi wa mpira.Kinyume na matakwa ya kamati ya uchaguzi kama yalivyotangazwa kuwa mtoa pingamizi aje mwenyewe kutetea pingamizi lake ,Bwana Agape Fue hakutokea mbele ya Kamati ya Bwana Lyatto.Matokeo yake tarehe 31/01/2012 kamati ya uchaguzi ya TFF ilitoa maamuzi ya ya kutupilia mbali pingamizi hili. Bwana Agape Fue hakuishia hapo kwa mara nyingine tarehe 06/02/2013 alikata rufaa kwenye kamati ya rufaa ya uchaguzi akidai kamati ya uchaguzi haikumtendea haki. Rufaa hii haikuwa na anwani wala namba ya simu ya Bw.Agape Fue.Rufaa ilisikilizwa tarehe 10/02/2013 na maamuzi ya kukata jina langu yakatangazwa jioni ya tarehe 11/02/2013. Mpaka leo najiuliza hivi huyu Bw. Agape Fue ni mwanaume au ni mwanamke?(hakueleza kama ni Bwana au Bibi Agape Fue). Agape Fue ni nani hasa? Anaishi wapi?Je ni Mtanzania au sio Mtanzania maana kikanuni wasio watanzania hawaruhusiwi kujihusisha na uchaguzi wa TFF (rejea kifungu cha 9 cha kanuni za uchaguzi),pingamizi lake halikuambatana na udhibitisha wa uraia. Kwa nini alichukua maamuzi haya? Sipati jibu. Iweje mtu achukue maamuzi mazito ya kumkatia mtu rufaa kisha uishie kusaini karatasi na kuwaachia wengine wakusemee na usije hata kushuhudia kinachoendelea kama kweli una maslahi na madai yako? Waandishi wa habari mnisaidie kupata majibu. Ndugu zangu ,mtoa pingamizi alidai haikuwa sahihi kupinga azimio la kubadili katiba ya TFF kwa njia ya waraka.Naomba nisistize mambo matatu: Wajumbe wa mkutano mkuu wa TFF wanawakilisha matakwa ya vyama vilivyowatuma kwenda kwenye mkutano mkuu wa TFF,na ndio maana chama cha mpira cha mkoa wa Kagera (KRFA) kiliitisha kikao cha kamati ya utendaji ili kamati iweze kutoa mwongozo kwa wajumbe wake kuhusu nini kifanyike kuhusu waraka ulioletwa na TFF,hivyo maamuzi yaliyotolewa ya kuukataa waraka huu yalikuwa ni maamuzi ya chama cha mpira mkoa wa Kagera na wala hayakuwa ni maamuzi ya Jamal Malinzi,iweje malinzi niadhibiwe kwa maamuzi haya,kwa nini usiadhibiwe mkoa mzima na mikoa yote iliyopinga waraka?hii ni haki kweli? Siamini kama kuna mjumbe wa mkutano mkuu aliyekiuka maamuzi ya kamati yake ya utendaji. Katika mchakato wa kubadili katiba kwa njia ya waraka kilichokuwa kinagomba sio maudhui (content) ya mabadiliko ya Katiba bali utaratibu uliotumika kubadili Katiba. Swali la msingi tulilojiuliza wajumbe wa kamati ya utendaji KRFA ni kwamba je kwa mujibu wa Katiba ya TFF kifungu 22 na kifungu 30 wapi katiba inatamka kuwa inaweza kubadilishwa kwa njia ya waraka? Mpaka leo hilo jibu hakuna,labda aliyeniwekea pingamizi atusaidie kupata jibu la swali hili. Katiba ya TFF iko wazi kabisa inatamka kuwa Katiba itabadilishwa kwa njia ya Mkutano Mkuu tu (General Assembly). Ni kweli FIFA iliagiza yafanyike mabadiliko ya Katiba ya kuingiza kipendele cha ‘club licencing’ katika Katiba ,lakini je FIFA katika agizo hilo ilisema Katiba ya TFF ivunjwe ili kutimiza azma hiyo? Ikumbukwe kuwa mwaka 2004 FIFA iliagiza TFF iingize kwenye Katiba kipengele cha Katibu Mkuu awe wa kuajiriwa badala ya kuchaguliwa,agizo hili lilitekelezwa kwa kupitishwa na Mktano Mkuu wa TFF,iweje leo utaratibu huu ukiukwe? Hata majuzi CAF walipotaka kubadili katiba ili Rais wa CAF atokane na wajumbe wa Kamati ya Utendaji jambo hili lilitekelezwa kwa kuitisha mkutano mkuu wa dharura uliofanyika Seychelles majuzi. Katiba ndio msingi mkuu wa uendeshajiwa TFF,nitaipigania siku zote.Huo ndio utaratibu,si CAF si FIFA si Vyama vya mpira vya nchi,hakuna anayebadili Katiba kwa njia ya waraka,kama kuna mwenye ushahidi aulete. Kuengua jina langu eti kwa kuwa nilipinga waraka wa kubadili Katiba sio uamuzi sahihi. Kuhusu uzoefu wa miaka mitano katika Uongozi: Ikumbukwe kuwa katika uchaguzi mkuu wa TFF mwaka 2008 niligombea na jina langu lilikatwa na kamati ya uchaguzi ya TFF.Nilikata rufaa katika Kamati ya Rufaa ya TFF na kushinda . Hukumu hii ni halali hadi leo.Iweje leo hii miaka minne baadae Kamati hiyo hiyo ya rufaa (kubadili majina ya wajumbe sio kubadili taasisi) inione sina uzoefu?.Si hilo tu ,hata katika kujaza fomu namba moja ya kugombea niliambatanisha vielelezo vyote vya uzoefu wangu ikiwa ni pamoja na kudhibitisha kuwa katika kipindi cha miaka mine iliyopita nimekuwa: -Mjumbe wa Baraza la michezo mkoa wa Dar es salaam. -Mwenyekiti wa kamati ya mashindano chama cha mpira mkoa wa Pwani COREFA. -Mjumbe wa mkutano mkuu wa mkoa wa Kagera -Mwenyekiti wa chama cha mpira mkoa wa Kagera Hii ni pamoja na kuongoza Yanga 2002-2005. Hivi katika nafasi hizi za uongozi ipi ni ya kuongoza ‘bonanza’? Nimedhalilishwa sana. HITIMISHO Vyombo vya habari kupitia makala,tahariri na maoni ya wasikilizaji/wasomaji/watazamaji vimesifia sana awamu mbili za uongozi wa Bwana Leodeger Tenga.Bwana Tenga amesifiwa kwa umahiri wake wa kuleta utulivu katika sekta ya mpira wa miguu Tanzania.Amesifiwa kwa kujenga taasisi imara ambayo mhimili wake mkuu ni sekretarieti makini na kamati mbali mbali zilizo imara .Let him rise to the occasion,muda wa kuonyesha uongozi imara ni huu,historia itamhukumu kwa jinsi gani atasimamia suala hili,haki sio lazima itendeke lakini pia inatakiwa ionekane inatendeka. Kamati ya utendaji ya TFF inayo mamlaka ya kubatilisha maamuzi haya kwa maslahi ya mpira wa Tanzania.Ninamshauri Rais wa TFF aitishe kikao cha dharura cha kamati ya utendaji ili kijadili hali hii na kunirudishia haki yangu ya kugombea urais wa TFF. Nihitimishe kwa kuwaomba wadau wa mpira wa miguu Tanzania wawe watulivu wakati tukisubiri kupata ufumbuzi wa suala hili. Mungu ibariki Afrika, Mungu ibariki Tanzania. Ahsanteni sana,
JAMAL MALINZI​
S.L.P 10000 DAR ES SALAAM​
13/FEBRUARY/2013​
 
Kuna watu wanasema siasa ni mbaya sana, haya michezo nayo? Imani nazo vipi?
Biashara nayo vipi?
Kilimo nacho?
Muziki nao?
Bongo movies nazo?
Mambo ya kisheria nayo?
 
Haya maamuzi ya kamati ya rufaa yangewahi kidogo kutolewa ningeenda kuyapendekeza yaingizwe katika maajabu saba ya Africa
 
Je ni wewe uliyeandika bila kuweka aya katika makala yako ama huyu jamaa mwenyewe Malinzi? Kama ni yeye basi hafai kuwa kiongozi.

Sidhani kama waraka huu upo katika hali yake ya awali kama ulivyotolewa na Malinzi. Hii ni soft copy lakini nina imani copy iliyotolewa kwa waandishi wa habari ina sahihi ya Malinzi!!!!

Tiba
 
Lakini,yawezekanaje nafasi nyeti kama ya Rais wa TFF ibaki na mgombea mmoja Bwana Athuman Nyamlani? Lazima jambo lifanyike hapa...lazima

nafasi za uongozi katika nchi hii ni za kupeana so ukimuona mtu anatidhia usalama wa kazi ya kupewa unamfanyia fitina na kumwondoa.This is Tanzania bwana,nchi ya maajabu.
 
Malinzi mwenyewe huna wema wowote na mpira wa bongo mwiz tu

Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums
 
hivi vyama vya soka vina matatizo..kuanzia Fifa..Caf hadi Tff...
angalia sept blatter alivyomfanyia yule bin hanan wa qatar
angalia issa hayatou anavyofanya..

lakini pia turudi nyuma kipindi cha joao havelange...alivyolazimisha blatter awe rais fifa

na sasa tenga anataulazimsha kutuwekea Nyamlani....
 
Sidhani kama waraka huu upo katika hali yake ya awali kama ulivyotolewa na Malinzi. Hii ni soft copy lakini nina imani copy iliyotolewa kwa waandishi wa habari ina sahihi ya Malinzi!!!!

Tiba


mkuu Tiba

hii ni soft copy niliamua kuwashirikisha ndugu zangu, kesho magazeti na redio zetu leo hii ndo watasoma
 
hivi vyama vya soka vina matatizo..kuanzia Fifa..Caf hadi Tff...
angalia sept blatter alivyomfanyia yule bin hanan wa qatar
angalia issa hayatou anavyofanya..

lakini pia turudi nyuma kipindi cha joao havelange...alivyolazimisha blatter awe rais fifa

na sasa tenga anataulazimsha kutuwekea Nyamlani....
Hivi kumbe ni Tenga ndiye anamtaka Nyamlani! Sikuwa na habari
 
Hapa Nyamlani kazi anayo, huyu bwana Malinzi akomae tu kilio chake kitasikika na wajumbe watatenda haki. hizi zote ni fitina tu kwenye ulaji
 
fitina (fitna) za CIA na FBI zinaishia kwenye kuifanya Amerika iendelee kuwa taifa kubwa na tajiri ili itawale dunia.
Fitna za Wakenya ni kutawala ukanda wa afrika Mashariki na maziwa makuu

Fitna za Tanzania ni kupata nafasi za uongozi wa umma ili kujaza matumbo ya familia na ndugu wa karibu.
basi na tuendelee kufurahia ushindi wa mechi za kirafiki na makombe ya kagame tu tujifurahishe
 
Back
Top Bottom