Taarifa ya kukosekana kwa umeme mkoani Dodoma

Frankwills

Member
Dec 16, 2015
9
2
SHIRIKA LA UMEME TANZANIA (TANESCO)


TAARIFA YA KUKOSEKANA KWA UMEME MKOANI DODOMA.

Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) linawatangazia wateja wake wa Mkoa wa Dodoma kuwa kumetokea hitilafu katika Transfoma kubwa inayosambaza Umeme katika mkoa huo na kupelekea Dodoma mjini na baadhi ya wilaya zake kukosa Umeme tangu saa 3.15 asubuhi ya leo Desemba 24, 2015.

Mafundi wetu wapo tayari katika mtambo huo kubaini chanzo cha tatizo hilo. Tutawapa taarifa pindi matengenezo yatapokamilika na Umeme kurudi katika hali ya kawaida.

Uongozi unaomba radhi kwa usumbufu wowote utaojitokeza.

Imetolewa na; Ofisi ya Uhusiano
TANESCO Makao Makuu.
 
watu wa Dodoma sio watu wa kuhoji maswala, wakatieni umeme tu bila hata tangazo wataelewa tu.
 
Back
Top Bottom