hakuna shida
Member
- Dec 16, 2015
- 25
- 5
TAARIFA YA KUKOSEKANA KWA UMEME KWA BAADHI YA MIKOA ILIYOUNGWA KWENYE GRIDI YA TAIFA JANUARI 31, 2016
Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) linawatangazia wateja wake wa mikoa ya Singida, Shinyanga, Tabora, Mwanza, Musoma, Mara, Babati, Simiyu na baadhi ya maeneo ya mikoa ya Arusha, Kilimanjaro na Tanga kuwa yatakosa umeme siku ya JUMAPILI tarehe 31 JANUARI, 2016 kuanzia Saa 1:00 Asubuhi hadi Saa 11.00 Jioni. Mkoa wa Dodoma utaathirika ikiwa kazi hiyo itafanyika katika kituo cha kupooza na kusambaza umeme cha Dodoma.
Sababu ni kazi inayoendelea kufanywa na Mkandarasi anayejenga njia kuu ya kusafirisha umeme wa msongo mkubwa wa kilovoti 400, inayojulikana kama ‘Backbone’ kutoka Iringa kwenda Shinyanga.
Mradi huo ambao utaimarisha hali ya upatikanaji wa umeme nchini.
Uongozi unasikitika kwa usumbufu wowote utakaojitokeza.
Imetolewa na: OFISI YA UHUSIANO,
TANESCO - MAKAO MAKUU.