Taarifa ya Jeshi la Polisi kuelekea sikukuu ya Eid - el - Fitr

Taarifa ya Jeshi la Polisi kuelekea sikukuu ya Eid - el - Fitr

amakyasya

JF-Expert Member
Joined
Jun 26, 2013
Posts
3,480
Reaction score
918
Polisi wameahidi kuimarisha ulinzi na kuweka camera za CCTV maeneo ya kumbi za starehe.

========================


image061.jpg

Jeshi la Polisi Tanzania linapenda kutoa shukrani za dhati kwa wananchi wote, vyama vya siasa, taasisi mbalimbali za serikali, madhehebu ya dini, asasi za kiraia na vyombo vya habari kwa ushirikiano wa dhati katika kusimamia masuala ya amani na usalama hapa nchini.

Tunapoelekea kipindi hiki cha kusherehekea sikukuu ya Eid-El-Fitr, Jeshi la Polisi linatoa wito kwa wananchi wote kuwa makini na kusheherekea sikukuu hiyo kwa amani na utulivu pasipo vitendo ama viashiria vyovyote vya uvunjifu wa amani.

Ikumbukwe kuwa, wananchi wenye imani ya kiislam na hata madhehebu mengine hutumia muda huo kwenda kuabudu pamoja na muendelezo wa sherehe hizo kwenye maeneo mbalimbali ya starehe. Uzoefu umeonyesha kuwa baadhi ya watu hutumia kipindi hicho cha sikukuu kama mwanya wa kufanya matukio ya uhalifu kutokana na mikusanyiko hiyo ya watu.

Jeshi la Polisi linapenda kuwaondoa hofu wananchi wote kuwa, limejipanga kikamilifu kuhakikisha wananchi kote nchini wanasherekea sikukuu hiyo kwa amani na utulivu. Ulinzi umeimarishwa kwenye maeneo yote ya kuabudia, fukwe za bahari, sehemu za starehe na maeneo mengine yote, aidha, tunapenda kuwatahadharisha wale wote ambao watakuwa wakitumia barabara, kuwa makini kwa kuzingatia sheria za usalama barabarani na hasa kwa madereva wa magari na pikipiki kuepuka kwenda mwendo kasi na kutumia vilevi wawapo kazini.

Katika kuhakikisha usalama kwenye kumbi za starehe, wamiliki wa kumbi hizo wazingatie uhalali na matumizi ya kumbi zao katika uingizaji wa watu kulingana na uwezo wa kumbi hizo, badala ya kuendekeza tamaa ya fedha kwa kujaza watu kupita kiasi.

Jeshi la Polisi linapenda kuwashukuru wale wote ambao tayari wamefunga kamera za CCTV katika maeneo yao ya starehe, hususani yale yanayokuwa na mikusanyiko mikubwa ya watu, yakiwemo maduka, hoteli na maeneo ya benki. Aidha, Jeshi la Polisi linaendelea kuwasisitiza wale ambao bado hawajaweka kamera hizo, kuweka ili ziweze kusaidia kubaini wahalifu na hata kurahisisha ukamataji endapo uhalifu unatokea.

Vilevile, wazazi wawe makini na watoto wao na hasa disko toto, ili kuepuka ajali na matukio mengine yanayoweza kusababisha madhara juu yao.

Aidha wananchi wachukue tahadhari watokapo kwenye makazi yao wasiache nyumba wazi ama bila mtu na watoe taarifa kwa majirani zao, na pale wanapowatilia mashaka watu wasiowafahamu wasikae kimya bali watoe taarifa haraka kwenye vituo vya Polisi vilivyo karibu nao au kwa namba ya simu ifuatayo 0754 785557, ili hatua stahiki ziweze kuchukuliwa haraka.

Imetolewa na:
Advera John Bulimba - SSP
Msemaji wa Jeshi la Polisi.


My take: Polisi wekeni ulinzi wa kutosha hawa jamaa wengi wao wanafungulia kwa vurugu sana. Msikose kuweka camera hizo pia kwenye magesti na kwenye mabucha ya kitimoto ulinzi uimarishwe.
 
Polisi wameahidi kuimarisha ulinzi na kuweka camera za CCTV maeneo ya kumbi za starehe.
Source: Majira gazeti la leo.

My take: Polisi wekeni ulinzi wa kutosha hawa jamaa wengi wao wanafungulia kwa vurugu sana. Msikose kuweka camera hizo pia kwenye magesti na kwenye mabucha ya kitimoto ulinzi uimarishwe.
Hivi usalama wa mtanzania ni wAkati wa sikukuu tu? Hizi kamera zimeazimwa wapi na zinarudishwa lini? Kwani bei ya camera ni sh ngapi?
 
Hivi usalama wa mtanzania ni wAkati wa sikukuu tu? Hizi kamera zimeazimwa wapi na zinarudishwa lini? Kwani bei ya camera ni sh ngapi?
Wana hofu sana na hawa jamaa maalshabaab wana vurugu sana kwenye sikukuu zao.
 
Safi sana jeshi polisi haya ndio maendeleo na mabadiliko tunayotaka...kidigital.
 
Maana humu kuna mi watu kazi yao kubisha na kupinga hata yale ambao ni muhim kwa jamii na taifa kwa ujumla...wanataka poliso waendelee kufanyakazi kwa hisia ovyo kabisa...tunaanzia sikuu kidigital na litakuwa moja kwa moja kudhibiti na kupambana na uhalifu....bravo polisi.
 
Back
Top Bottom