Taarifa ya daktari wa rais

hawakuwa wachapa kazi kama kikwete, hawakuwa wanafuatilia mambo kama kikwete, kikwete ameweka "historia" kwa kuwa rais mfuatiliaji wa mambo ya TZ ndani na nje ya nchi

HIYO BARUA IMETOA UFUNUO WA KWAMBA SAFARI NYINGI ZA MUHESHIMIWA RAIS NJE YA NCHI NI ZA MATIBABU, NA KAMA SAFARI NYINGI NI ZA MATIBABU BASI ANA MATATIZO MAKUBWA YA KIAFYA AMBAYO YANAFICHWA.
PIA INAONYESHA RAIS AMEKUWA AKIAMA DR/HOSPITALI MARA UFARASA, MARA USA, MARA GERMANY NA HII NI DALILI YA MTU ANAYETAFUTA TIBA YA KITU KINACHOMSUMBUA

Tafakari!
 
Sasa imewekwa wazi, na wananchi wameondolewa wasiwasi kuwa Rais wao ni mgonjwa baada ya kuwa anazidiwa mara kadhaa kila anapopatwa na kile kinachoelezwa kuwa uchovu wa kazi.
Leo Daktari wa Rais Jakaya Kikwete, Peter Mfisi ameibuka na kuqweka kila kitu hadharani kuhusu afya ya Rais wetu.
Daktari huyo akiwa Ikulu, akasema Rais Kikwete hana Ukimwi, hana kansa, hana dalili za kiharusi na kamwe hakuna kaugonjwa kokote kwenye damu yake wala nyama zake.
Hatua hiyo inakuja siku chache baada ya Rais Kikwete kuishiwa nguvu wakati akihutubia katika Jubilee ya miaka 100 ya Kanisa la Africa Inland Tanzania (AICT) jijini Mwanza wiki iliyopita.
"Naelewa fika kutokana na kiapo cha udaktari na maadili yangu, siruhusiwi kutoa hadharani undani wa habari yoyote inayohusu mgonjwa ninayemtibu bila ridhaa yake...
... Kwa kuwa huyu ni Rais wa nchi, na suala la afya yake ni kwa maslahi ya Taifa na umma wa Watanzania kwa ujumla, na kwa kuwa yeye ameridhia kutolewa kwa habari za afya yake ili watu wajue ukweli na kuondoa hofu, nimeamua kufanya hivyo,"alisema Mfisi.
Alisema kila mara Kikwete amekuwa akipimwa na kufanyiwa uchunguzi wa afya yake na madaktari wa Tanzania na wale wa nje ambako huenda mara kwa mara na wote wamebaini kuwa hana kaugonjwa kokote kanakowez kufikiriwa na yeyote.
Mungu Mkubwa jamani, yote mabaya yaliyokuwa yakielezwa na wale wachokozi, kumbe hamna kitu na hiyo imethibitishwa na madaktari wake na wale wa nje, ambao nasikia hawana punje ya rushwa hata kusema uongo.

Kwa hiyo ina maana haujajulikana?
 
jamani mie nauliza kwani mheshimiwa anaumwa nini ..naona hapo wote hamkubaliani na hiyo report ya Dr wake ..


Nadhani First lady unajua tatizo la Mkuu wetu kuliko hata Daktari. Sasa siju unategemea kujibiwa na nani wakati tukitilia shaka maelezo ya daktari wake tunakuuliza wewe?
 
tutumie muda zaidi kuitafakari hii taarifa yake kwa makini sana, hebu m.m.k.j tuambie umeelewa hapa anachokimaanisha daktari wa mkuu. Isije iwaka ni profile satatment kuficha ukweli kama ambavyo birthday yake ilivyoandaliwa kwa ajili ya kutufanya kusahau la kuishiwa nguvu mwanza

Acha uvivu kaka,kila kitu Mwanakijiji tuuuu,muoneeni huruma mwenzenu jamani,yaani wewe kuielewa taarifa mpaka Mwanakijiji aongee...Lol!!!!!!!
 
Dah mi hata sijui nimwamini nani katka hili. Ila LISEMWALO LIPO KAMA HALIPO LAJA. ngoja nisubiri kwenye kona, huenda nikaja kutambua ukweli siku za mbeleni.
 
Acha uvivu kaka,kila kitu Mwanakijiji tuuuu,muoneeni huruma mwenzenu jamani,yaani wewe kuielewa taarifa mpaka Mwanakijiji aongee...Lol!!!!!!!
Ndio wale wale ambao hata kusali ni wavivu wanapigia wachungaji simu usiku na kuwaomba wawaombee!
 
tatizo wanasiasa wetu wameongopa kupita kiasi, sasa hata wanaposema ukweli inakuwa vigumu wananchi waliodanganyika kwa muda mrefu kuamini.

the bottom line is, rais hayuko fit enough. wapo marais wazee zaidi barani Afrika wanaopiga mzigo kuliko Kikwete, plus migogoro ya kisiasa mizito (Kibaki + Mugabe), lakini hutasikia hata siku moja engine zina mgogoro.
 
Ndio wale wale ambao hata kusali ni wavivu wanapigia wachungaji simu usiku na kuwaomba wawaombee!
kiongozi umenichekesha sana..mwe unapiga simu kwa mchungaji kumuambia awaombeee teh
 
tatizo wanasiasa wetu wameongopa kupita kiasi, sasa hata wanaposema ukweli inakuwa vigumu wananchi waliodanganyika kwa muda mrefu kuamini.

the bottom line is, rais hayuko fit enough. wapo marais wazee zaidi barani Afrika wanaopiga mzigo kuliko Kikwete, plus migogoro ya kisiasa mizito (Kibaki + Mugabe), lakini hutasikia hata siku moja engine zina mgogoro.

mkuu umetoa mifano sawia..Mugabe anapigwa mikwara kila upande plus viungulia anavopewa na tshivangarai lakini yuko stable anadunda tu .JK engine inatakiwa kufanyiwa overhaul
 
Acha uvivu kaka,kila kitu Mwanakijiji tuuuu,muoneeni huruma mwenzenu jamani,yaani wewe kuielewa taarifa mpaka Mwanakijiji aongee...Lol!!!!!!!

Ni kweli naweza kuwa mvivu, lakini nadhani mwenzangu utakuwa mvivu zaidi wa kuelewa nilichokuwa nikimaamisha. Nacho ni ushirikishaji wa mtu katika kubadilishana mawazo. Pole mvivu mwenzangu. Ila unakusudia kupotosha mjadala hilo halikuwa la kujadili.
 
HIYO BARUA IMETOA UFUNUO WA KWAMBA SAFARI NYINGI ZA MUHESHIMIWA RAIS NJE YA NCHI NI ZA MATIBABU, NA KAMA SAFARI NYINGI NI ZA MATIBABU BASI ANA MATATIZO MAKUBWA YA KIAFYA AMBAYO YANAFICHWA.
PIA INAONYESHA RAIS AMEKUWA AKIAMA DR/HOSPITALI MARA UFARASA, MARA USA, MARA GERMANY NA HII NI DALILI YA MTU ANAYETAFUTA TIBA YA KITU KINACHOMSUMBUA

Ndugu yangu taratibu na huko kuunganisha dots, usije ukafumua yaliyojificha.
 
Alitamka mwenyewe kuwa alishauriwa akakataa; sasa atakuwa anafuata ushauri.
Namshauri JK afuate hata ushauri juu ya kuwang'oa mafisadi vinginevyo huku kuanguka kwake kunaweza kuwa kuanguka kabisa na mafisadi wake
 
Acheni unyanyapaa jamani.Stigma and Discrimination is evil.Ingekuwa wewe?

Usijisikie vibaya. Hayo ndo matokeo ya siasa ktk nchi ambazo hazina ethics. Si umesikia yaliyotokea ufaransa? Tungekuwa na utaratibu mzuri kama huo uongo ungekoma na heshima ingekuwa juu, lakini siyo hali tuliyonayo.
 
Jamani sasa mtu asiugue...yeye ni binadamu kama binadamu wengine kwa nini watu wanajaribu kumpangia nini anaumwa daktari amefafanua kinachomsumbua mheshimiwa nadhani inatosha.
 
Rais amefanyiwa colonoscopy mwaka 2007, mnatuambia leo !!???
Kwa kawaida Rais anapofanyiwa kipimo kama hiki inabidi itangazwe promptly,
- kwanza kwa sababu ninavyoelewa mimi mgonjwa anakuwa sedated for a few hours, Rais anakuwa hana uwezo wa kuendesha nchi muda huo, sasa who was running the show during those few hours ?
- It also serves the purpose ya kuelimisha wananchi umuhimu wa wao pia kufanya vipimo hivi.

Lakini sisi kila kitu siri tuuu.....

Colonoscopy alifanyiwa mwaka 2007 ufaransa kwahiyo someone was acting President; lakini hili la kusema kuwa walishauriwa kuwa afanye tena baada ya miaka saba ndio linanifanya niwe na shaka na ripoti ya huyu daktari!! Kumbuka Mkulu ana miaka 59 sasa chances za vimelea kuota kwenye utumbo mkubwa ni significant!!
 
i know this young man who is the predaa dr....kijana umekosea sana...kuiweka ripoti ya rais kwa urefu as if kuna kitu mnatetea hapo...psychology nyepesi hapo ni kuwa you have been toooo defensive which leaves quaetions as to what is the motive of being too elaborative....hata kama amekulazimisha utoe ripoti ungekuwa too brief...

....sasa ripoti yako ya kitaalamu umeiandika kisiasa ...itabidi uwe tayari kujibizana na wanasiasa.....

..huwa nafuatilia ripoti za marais mbalimbali duniani.....na ripoti za namna hii huwa brief short and clear......abide to your proffession ,....usimsikilize kikwete...ambaye yeye mwenyewe amekiri hapa kuwa ushauri wenu huwa anaukiuka......lakini kwenye ripoti yako umemsifu kwa kufuata ushauri....ianamaana kwa kumsifu kuwa aanafuata ushauri na amekiri hafuati..umesema uwongo...and this subject and jeoperdise all your report ...and it worth be called the scrap propaganda report!!!!

umeitukana fani yako mdogo wangu ..mfisi!!!

Mficha kidonda guu huota tende...
Hili swala la kufichaficha mambo halipati kuisha, tulitegemea briefing ya Dr. siku hiyo hiyo ya tukio, maana anakili hata vipimo vya Mh. Rais alivipata right away, lakini wapi... mpaka Tz blogsphere ilikomalie ndiyo waingie kwenye 'overdrive' kujihami na kujaribu kuweka mambo sawa.

Hii report ilivyo ndefu imenikumbusha thread hii: https://www.jamiiforums.com/jukwaa-la-siasa/17215-rais-kikwete-aenda-marekani.html#post274647. Ambapo machinery ya Ikulu ilibidi ifanyekazi overtime kuhalalisha mambo.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom