Taarifa ya daktari wa rais | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Taarifa ya daktari wa rais

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Halisi, Oct 8, 2009.

 1. Halisi

  Halisi JF-Expert Member

  #1
  Oct 8, 2009
  Joined: Jan 16, 2007
  Messages: 2,810
  Likes Received: 83
  Trophy Points: 145
  DIRECTORATE OF PRESIDENTIAL COMMUNICATIONS
  UNITED REPUBLIC OF TANZANIA

  Telephone: 255-22-2114512, 2116898
  E-mail: press@ikulu.go.tz
  Fax: 255-22-2113425

  PRESIDENT’S OFFICE,
  THE STATE HOUSE,
  P.O. BOX 9120,
  DAR ES SALAAM.
  Tanzania.

  TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

  Mimi naitwa Dk. Peter Mfisi, ni mmoja wa madaktari wa Mhe. Rais. Nipo Ikulu. Nimekuwa na Mhe. Rais tangu wakati wa kampeni mwaka 2005 mpaka sasa. Mwenzangu ni Dk. Mohamedi Janabi ambaye ni daktari bingwa wa maradhi ya moyo katika Hospitali Kuu ya Taifa Muhimbili.

  Nimewaiteni waandishi wa habari kufafanua masuala muhimu kuhusu afya ya Mhe. Rais kufuatia tukio la Jumapili iliyopita, Oktoba 4, 2009, pale Mwanza.

  Tukio hilo limeleta mshtuko kwa watu wengi na kuendelea kuwa jambo linalozua mjadala kuhusu hali ya afya ya Mhe. Rais. Naelewa sababu ya wananchi kuwa na hofu na kuwapo kwa mjadala miongoni mwao. Rais ndiyo kiongozi wetu mkuu katika taifa na hivyo kuwa mwenye afya njema ndiyo matakwa ya kila mwananchi.

  Naelewa fika kuwa kutokana na kiapo changu cha udaktari na maadili yangu ya kazi siruhusiwi kutoa hadharani undani wa habari yoyote inayohusu mgonjwa ninayemtibu bila ridhaa yake.

  Hata hivyo, kwa kuwa huyo ni Rais wa nchi, na suala la afya yake ni kwa maslahi ya taifa na umma wa Watanzania kwa jumla, na kwa kuwa yeye ameridhia kutolewa kwa habari za afya yake ili watu wajue ukweli na kuondoa hofu, nimeamua kufanya hivyo.

  Kama sote tujuavyo, Jumapili iliyopita, Oktoba 4, 2009 mwaka huu, Mhe. Rais Jakaya Mrisho Kikwete, akiwa anashiriki katika sherehe za miaka 100 ya Kanisa la Africa Inland Church Tanzania (AICT) kwenye Uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza, aliishiwa nguvu na kulazimika kwenda kwenye chumba cha mapumziko.

  Baada ya mapumziko ya dakika 10 hivi, Mhe. Rais alirejea kwenye shughuli hiyo na kuendelea kushirikiana na waumini wa AICT hadi mwisho wa ratiba yake.

  Ninapenda kusisitiza kuwa tukio la Mwanza limetokana na Mhe. Rais kuzidiwa na uchovu, na wala siyo kwa sababu nyingine yoyote ya kiafya. Wakati tukio hilo linatokea nilikuwepo, nilichukua vipimo muhimu kama daktari anavyotakiwa kufanya linapotokea tukio kama lile kwa mtu. Vipimo vyote vilithibitisha kuwa Mhe. Rais hakuwa na matatizo yoyote ya kiafya ambayo yangeweza kuhusishwa kuwa chanzo cha tukio lile.

  Pressure yake ilikuwa 130/85mmhg ambayo ni kiwango cha kawaida kwa mtu wa umri wake. Mapigo ya moyo wake yalikuwa 76 kwa dakika ambayo pia ni ya kawaida. Sukari kwenye damu ilikuwa 5.5mmol/l ambayo nayo ilikuwa ya kiwango cha kawaida. Joto la mwili lilikuwa digrii 37.5 centigrade ambalo ni la kawaida. Mhe. Rais pia hakuwa na kiungo chochote kilichoonekana kutetereka, jambo ambalo lilithibitisha kuwa hakupata kiharusi.

  Kutokana na matokeo hayo, sikuona hatari yoyote ya yeye kuendelea kushiriki katika sherehe hiyo muhimu kwa wakati huo. Ndiyo maana niliruhusu aendelee kushiriki sherehe zile mpaka alipomaliza na kuondoka.

  Baada ya kurudi Dar es Salaam siku ile niliwasiliana na madaktari wanzangu wa hapa nchini na nje ya nchi ambao tumekuwa tunashirikiana nao katika kuchunguza na kufuatilia afya ya Mhe. Rais. Wote hao baada ya kuwasimulia kilichotokea na matokeo ya vipimo nilivyomfanyia Mhe. Rais, kwa tafakuri zao hawakuwa na wasiwasi wowote kuwa tukio hilo lilisababishwa na jambo jingine lolote, isipokuwa uchovu. Imani yao inatokana na ukweli kuwa wanaifahamu vizuri hali ya afya ya Mhe. Rais kwa kuwa wanahusika katika kuifuatilia mara kwa mara. Mmoja wao alimuona Mhe. Rais siku moja kabla ya kuondoka New York ambapo alipata nafasi ya kuchunguza afya yake.

  Mimi na mwenzangu Dk. Mohammed Janabi, ndiyo wenye dhamana ya kuiangalia afya ya Mhe. Rais Kikwete kila siku. Tumekuwa tunafanya hivyo kwa zamu na wakati mwingine kwa pamoja, inapobidi kufanya hivyo. Katika kufuatilia hali ya afya ya Mhe. Rais tumekuwa pia tukimfanyia uchunguzi wa afya yake kwa vipindi maalum hapa nchini na nje ya nchi kwa vipimo ambavyo hapa nchini havipo. Napenda kuwahakikishia wananchi wenzagu kuwa katika miaka hii minne Mhe. Rais wetu amefanyiwa uchunguzi wa kina wa afya yake. Nadiriki kusema kuwa hakuna kipimo ambacho hatujapata kukifanya katika uchunguzi wa mambo muhimu ya afya yake.

  Kwa sababu ya kuwatoa hofu wananchi na kwa vile mwenyewe anaridhia tufanye hivyo napenda kuwapa ufafanuzi kuhusu hali ya afya ya Mhe. Rais. Katika hali ya kawaida nisingefanya hivyo kwa sababu maadili ya kazi ya udaktari yanakataza. Naamini madaktari wenzangu wataelewa mazingira niliyokuwa nayo. Katika kufuatilia afya ya rais tumekuwa tunaangalia na kuchunguza mambo yafuatayo.

  (a) Blood Pressure: Tunafuatilia kwa karibu sana hali ya nguvu ya msukumo wa damu (blood pressure). Tunampima mara kwa mara na mwenyewe tumempa mashine ya kujipima kila siku na anafanya hivyo. Kwa jumla pressure yake iko kwenye viwango vya kawaida. Aidha, uzito wake wa mwili unaendena ipasavyo na urefu wake. Mhe. Rais ni mtu mwenye mazoea ya kufanya mazoezi na yuko makini katika chakula anachokula. Sisi tunahusika kwa ukamilifu na kuelekeza kuhusu chakula anachokula. Hatuna matatuzi na Mhe. Rais kwa jambo hilo. Ana nidhamu ya kujipima pamoja na mazoezi na chakula.

  (b) Moyo: Tumekuwa tunafuatilia kwa karibu hali ya afya ya moyo wake. Tumemfanyia vipimo kama vya ECHO, ECG na vinginevyo, na hatujabaini kuwepo tatizo lolote.

  (c) Ubongo: Mwaka uliopita, 2008, Mhe. Rais tulimfanyia uchunguzi wa afya ya ubongo wake katika Hospitali ya Taifa Muhimbili hapa Dar es Salaam. Tulitumia kipimo cha CT – Scan na matokeo yameonyesha kuwa hana matatizo.

  (d) Ini, Figo, Bandama, Kongosho: Mhe. Rais Kikwete kila mwaka tunapomfanyia uchunguzi wa jumla wa afya yake tumekuwa tunamfanyia kuchunguza viungo vyake muhimu vya tumboni kama vile ini, figo, bandama na kongosho. Tumekuwa tunafanya hivyo kwa kutumia kipimo cha ultra sound na kwa kupima damu yake kwa kutumia vipimo muhimu. Uchunguzi huo umebaini kuwa viungo vyote hivyo ni salama na vinafanya kazi vizuri.

  (e) Mfumo wa njia ya Chakula: Mfumo mzima wa njia ya chakula (alimentary canal), yaani koromeo la chakula, tumbo, utumbo mdogo na utumbo mkubwa nao tumeufanyia uchunguzi wa kina kama kuna tatizo lolote katika kipindi cha miaka miwili hii. Mwaka 2007, tulimfanyia kipimo cha colonoscopy mjini Paris, Ufaransa, kuchunguza hali ya afya ya utumbo mkubwa. Matokeo ya uchunguzi yalionyesha kuwa utumbo wake mpana uko salama kabisa na hakuna matatizo yeyote. Daktari bingwa aliyemfanyia uchunguzi huo ameshauri kuwa Mhe. Rais hahitaji kufanya kipimo hicho tena mpaka baada ya miaka saba. Nakumbuka pia daktari huyo alimtania Mhe. Rais kuwa angefurahi kuazima utumbo wake.

  Wiki mbili zilizopita, Mhe. Rais akiwa mjini New York, Marekani, alifanyiwa kipimo cha endoscopy kuchunguza kuanzia koromeo la chakula, tumbo, na utumbo mdogo. Matokeo ya uchunguzi huo yametoa majibu mazuri kuwa yako salama. Makusudio ya kufanya vipimo hivi viwili ni kuchunguza maradhi ya kansa na viashiria vya ugonjwa huo. Bahati nzuri hana maradhi hayo na wala hakuna dalili yoyote iliyoonyesha kuwapo viashiria vya kansa.

  (f) Tezi la Shingo (Thyroid Glands): Aidha, wakati wa safari yake hivi karibuni majuzi mjini New York, Marekani, Mhe. Rais tulimfanyia uchunguzi wa afya ya tezi la shingo pamoja na kiwango chake cha utoaji wa homoni. Matokeo ya vipimo vyote vilivyofanyika yameonyesha kuwa hakuna matatizo yoyote.

  (g) Tezi la Kibofu (Prostate): Septemba, mwaka huu, 2009, tulifanya uchunguzi wa hali ya afya ya tezi la kibofu (prostate) kwa kutumia mashine maalum na kwa kuchunguza damu yake. Vipimo vyote hivyo vimeonyesha hali si mbaya. Tezi lake lina ukubwa wa kawaida na hata vipimo vya viashiria vya kansa ya tezi hilo (PSA) tunavyofanya kwenye damu vilikuwa katika kiwango cha kawaida. Mhe. Rais hana matatizo ya prostate.

  (h) Macho, Masikio na Pua: Tumeshamfanyia vipimo vya macho, masikio na pua na vyote viko salama. Mhe. Rais anavaa mawani lakini hayo si maradhi. Watu wengi baada ya kufikia umri wa miaka 40 si ajabu huhitaji mawani. Tunapofanya uchunguzi wa macho, ukiacha ile ya kuchunguza uwezo wa kuona, tunaangalia pressure ya macho na hali ya viungo vya nje na ndani ya jicho. Mhe. Rais hana matatizo yoyote.

  (i) Damu: Tumekuwa tunamfanyia Mhe. Rais uchunguzi wa damu yake kwa vipimo mbalimbali vinavyotumika kutambua maradhi mbalimbali yahusuyo damu yenyewe na mwili mzima wa mwanadamu. Tumekuwa tunafanya hivyo kila baada ya miezi sita au panapojitokeza ulazima wa kufanya hivyo. Tumekuwa tunafanya hivyo hapa nchini na hata nchi za nje kwa nia ya kulinganisha matokeo yetu na kwa vipimo ambavyo sisi hatunavyo. Matokeo ya uchunguzi wetu yameonyesha kuwa Mhe. Rais yuko salama. Hana maradhi ya damu au kisukari, wala ukimwi, au ya wingi wa mafuta (cholesterol), ama ya kiwango cha madini, au ya tezi la kibofu, wala ya tezi la shingo, au ya ini, au ya homoni mbalimbali zilizoko mwilini na mengine n.k. Jambo pekee linalojitokeza ni kwamba Mhe. Rais ana damu nyingi. Hivyo, tumekuwa tunamshauri kupunguza damu kwa kuchangia Benki ya Damu.

  Tunashukuru amekuwa anafanya hivyo karibu kila baada ya miezi sita. Damu nyingi inaweza kuwa na madhara mwilini lakini Mhe. Rais hajafikia kiwango cha kuwa ni tatizo la kiafya. Pia tunamshukuru kwa kuwa mwepesi kukubali kupunguza damu ambayo tunaitumia kuokoa maisha ya watu wengine. Hakuna hofu yoyote.


  Napenda kusema wazi watu wote wasikie na kwa ukweli kwamba mimi na daktari mwenzangu yaani Dr. Mohamed Janabi hali ya afya ya Rais silo jambo linalotutia shaka wala kutusumbua au kutunyima usingizi.

  Tatizo pekee ambalo limekuwa likimsumbua Mhe. Rais mara kwa mara ni maumivu ya shingo yanayotokana na kuumia zamani utotoni na wakati wa ujana. Kuumia huko ni kwa baadhi ya pingili za uti wa mgongo, sehemu ya shingo (cervical spine), kuathirika na kumsababishia maumivu. Mara nyingi matatizo ya namna hiyo huwapata wanamichezo na wanajeshi. Kutokana na shughuli wazifanyazo. Kuumia siyo jambo la kustaajabisha.

  Tutakumbuka kuwa Mhe. Rais amekuwa mwana michezo hususan mchezaji wa basketball, mpira wa miguu na hata riadha wakati wa ujana wake. Pia alikuwa mwanajeshi. Ili kutambua vizuri tatizo la shingo ili tujue namna ya kumpatia tiba tumeshamfanyia vipimo vyote muhimu vya uti wa mgongo toka juu mpaka chini. Tumetumia x-ray, CT – Scan na MRI-Scan. Pia ameshaonwa na madaktari bingwa wa upasuaji wa mishipa ya fahamu hapa nchini na nje. Pamoja na kuwepo athari katika shingo, madaktari hao kwa dhati wameshauri kuwa kwa sasa maumivu yake hayahitaji upasuaji isipokuwa mazoezi ya viungo. Mhe. Rais amefundishwa mazoezi anayotakiwa kuyafanya na amekuwa anayafanya kwa nidhamu ya hali ya juu. Matokeo yake ni kupata nafuu kubwa. Ndiyo maana siku hizo haonekani kunyoosha shingo mara kwa mara kama ilivyokuwa zamani kwa wale wanaokumbuka. Tunafuatilia kwa karibu sana hali ya shingo yake. Tunamfanyia vipimo vya MRI na kuonana na madaktari bingwa mara kwa mara.

  Mwisho
  Napenda kabla ya kumalizia nisisitize tena kwa kusema kuwa mimi na daktari mwenzangu hatuna mashaka na hali ya afya ya Mhe. Rais. Afya yake ni nzuri, hana maradhi yanayotishia maisha yake au kupunguza uwezo wake wa kulitumikia taifa na watu wake. Pia maoni yetu hayo ndiyo maoni ya madaktari wa ndani na wa nje waliowahi kuhusika na uchunguzi wa afya yake.

  Napenda pia kuwahakikishia kuwa, sisi madaktari wake, hatutachoka kufuatilia kwa karibu na kwa umakini mwenendo wa afya ya Mhe. Rais ili tujue mapema kama kuna jambo la kushughulikia. Kwa hili lililotokea, tutaendelea kuchunguza kama jambo lolote lililojificha ambalo hatujalibaini.

  Kwa sasa napenda kurudia kusema kuwa hakuna ushahidi wa kitaalamu wa kusema kuwa kulikuwa na sababu nyingine zaidi ya uchovu. Rais aliondoka New York Septemba tarehe 30 saa nane ya usiku kwa saa ya hapa Dar es Salaam kuanza safari ya kurudi nyumbani. Aliwasili nyumbani saa saba ya usiku wa tarehe 1 Oktoba. Njiani alisimama London na Nairobi kuunganisha ndege. Hivyo basi, alisafiri saa 24 bila ya kulala vizuri. Isitoshe hata kwenye ndege alitumia muda mwingi akifanya kazi. Asubuhi na mapema siku ya Oktoba 2, aliondoka Dar es Salaam kwenda Arusha kufungua mkutano wa Wabunge wa Jumuiya ya Madola saa nne asubuhi. Baadae jioni yake alishiriki kwenye hafla ya chakula cha jioni alichowaandalia wabunge. Rais aliondoka saa sita usiku kwenda kulala. Hatuna hakika alilala saa ngapi kwani najua akiwa na kazi huchelewa sana kulala. Tarehe 3 Oktoba, 2009 alikuwa na mikutano mfululizo na viongozi na wananchi pale Arusha kabla ya kuondoka majira ya alasiri kwenda Mwanza. Alipofika Mwanza alikuwa na mazungumzo na wenyeji wake usiku ule mpaka saa nne ya usiku. Tulipofuatilia tuligundua kuwa hata siku hiyo nayo alichelewa sana kulala kwani walipondoka wageni wake yeye aliendelea kushughulikia hotuba yake mpaka karibu na alfajiri. Katika mazingira hayo kupata matatizo ya mwili kuchoka sana, na hata kukataa kuendelea kutumika, na kutaka kupumzika kama ilivyotokea si jambo la ajabu.

  Mwisho kabisa napenda kuwahakikishia kuwa Rais yuko salama. Afya yake ni nzuri na haina shaka yoyote. Uchovu uliokithiri ndicho chanzo cha yaliyotokea Mwanza siku ile ya tarehe 4 Oktoba, 2009. Mimi na wenzangu katika Ofisi Binafsi ya Rais (OBR) tumejifunza na tumeazimia kuwa waangalifu zaidi katika kupanga ratiba ya kazi ya Rais.


  Dr. Peter Mfisi Ikulu, Dar es Salaam
  Daktari wa Rais 08 Oktoba, 2009
   
 2. S

  Solomon David JF-Expert Member

  #2
  Oct 8, 2009
  Joined: Mar 1, 2009
  Messages: 1,148
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Uongo uongo uongo.

  Mpelekeni atibiwe na msifiche ugonjwa.
   
 3. Asprin

  Asprin JF-Expert Member

  #3
  Oct 8, 2009
  Joined: Mar 8, 2008
  Messages: 50,886
  Likes Received: 23,515
  Trophy Points: 280
  Kumbe inakuwaga hivyoe. Ngoja nami nitafute daktari wangu bana.
   
 4. Mr. Zero

  Mr. Zero JF-Expert Member

  #4
  Oct 8, 2009
  Joined: Jun 5, 2007
  Messages: 9,496
  Likes Received: 2,740
  Trophy Points: 280
  Waswahili husema; Mficha Maradhi Mauti yatamuumbua...............!!!!!!
   
 5. M

  Mdondoaji JF-Expert Member

  #5
  Oct 8, 2009
  Joined: Mar 17, 2009
  Messages: 5,106
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 145
  Waungwana wanasema hasidi hawi bwana hata siku moja sasa wewe nikuulize ulitaka Daktari wa Rais asemeje ashakwambia hana tatizo lolote.

  Mie binafsi nashukuru kwasababu urais ni taasisi hivyo kama mkuu wa taasisi anaumwa then nakuwa na wasiwasi na mwelekeo wa taasisi. Sasa wewe unasema uongo ulitaka wakwambia rais anaumwa kiharusi, sijui uzushi katazame gazeti la udaku kule Global Publishers, mwishoe mtadai rais anaumwa ukimwi (mmungu amuepushie nao mbali).

  Acheni chuki zenu bwana kama hamkumchagua kikwete mie nilimchagua na nitampa kura mwakani mmungu akiniweka hai. But ukweli lazima usemwe na sio majungu tu yasiyo na mpango alaa!!!!
   
 6. N

  Nyauba JF-Expert Member

  #6
  Oct 8, 2009
  Joined: Jul 10, 2008
  Messages: 1,098
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  ni vizurii kuwa na uhakika na afya ya Raisi wetu. Asante Daktari kwa ufafanuzi yakinifuuuuu...ila ni gharama kweli kutambua vyotee hivyooo!!
   
 7. Eeka Mangi

  Eeka Mangi JF-Expert Member

  #7
  Oct 8, 2009
  Joined: Jul 27, 2008
  Messages: 3,182
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  Haya baba tuambie ukweli basi nasi tujue. Wampeleke wapi akatibiwe?
   
 8. NGULI

  NGULI JF-Expert Member

  #8
  Oct 8, 2009
  Joined: Mar 31, 2008
  Messages: 4,812
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 135
  Solo! Unabishana na Dr.? kwanini ww huamnin? umempima ukagundua mgonjwa au ni unasikiliza maneno ya wanasiasa?
   
 9. Bluray

  Bluray JF-Expert Member

  #9
  Oct 8, 2009
  Joined: Mar 25, 2008
  Messages: 3,446
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 135
  I am thinking how honest is the Kikwete Ikulu? Kama Kikwete alipata nervous breakdown na kuzimia wangetuambia au wangetupa story kama hiyo hapo juu?

  Huu uchovu uchovu gani? Jangwani napo? Mwanza I? Mwanza II? The several times he is reputed to have fainted in Ikulu? Mbona Nyerere, Mwinyi na Mkapa walikuwa hawazimiki zimiki hivi?

  Tuambieni kweli jamani, kesho keshokutwa mkiumbuliwa na matatizo haya mtaonekana wajinga sana.
   
 10. Victoire

  Victoire JF-Expert Member

  #10
  Oct 8, 2009
  Joined: Jul 4, 2008
  Messages: 10,445
  Likes Received: 7,182
  Trophy Points: 280
  hahahaha da hata sielewi kabisa
   
 11. Waberoya

  Waberoya Platinum Member

  #11
  Oct 8, 2009
  Joined: Aug 3, 2008
  Messages: 11,570
  Likes Received: 3,863
  Trophy Points: 280
  Cd4???
   
 12. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #12
  Oct 8, 2009
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  Taarifa kwa umma haihitaji majibu!!! Asante Peter na Janabi!!! We take what you have given us and move forward; sould there be anything opposite to this revealed in future, you will bear responsibilities moraly and ethically and most important as people who were given dhamana na nchi yetu nzuri kumuangalia kiongozi wetu mpendwa

  MTM
   
 13. Kandambilimbili

  Kandambilimbili R I P

  #13
  Oct 8, 2009
  Joined: Nov 11, 2008
  Messages: 782
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  CD4 profile sijaona au hakipo kwenye orodha ya vipimo, hiki sio HIV status tu kinaangalia kasi ya uzee inakwenda kwa speed gani ati.......
   
 14. Victoire

  Victoire JF-Expert Member

  #14
  Oct 8, 2009
  Joined: Jul 4, 2008
  Messages: 10,445
  Likes Received: 7,182
  Trophy Points: 280
  kweli bwana maana haya mambo ya kufaint faint bwana mtu kama kikwete ambae mambo yake supa.
   
 15. FirstLady1

  FirstLady1 JF-Expert Member

  #15
  Oct 8, 2009
  Joined: Jul 29, 2009
  Messages: 16,575
  Likes Received: 541
  Trophy Points: 280
  jamani mie nauliza kwani mheshimiwa anaumwa nini ..naona hapo wote hamkubaliani na hiyo report ya Dr wake ..
   
 16. K

  K4jolly JF-Expert Member

  #16
  Oct 8, 2009
  Joined: May 21, 2009
  Messages: 366
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ukisoma hii habari na jinsi alivyopata matatizo mara mbili huko nyuma inaonyesha Rais wetu bado anaumwa. Cha muhimu tumuombee apone haraka kwani majukumu aliyo nayo ni mazito.
   
 17. NGULI

  NGULI JF-Expert Member

  #17
  Oct 8, 2009
  Joined: Mar 31, 2008
  Messages: 4,812
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 135
  uchovu wa kazi hapunziki!!
   
 18. Victoire

  Victoire JF-Expert Member

  #18
  Oct 8, 2009
  Joined: Jul 4, 2008
  Messages: 10,445
  Likes Received: 7,182
  Trophy Points: 280
  KWELI maana majukumu ya kukwea mapipa atleast mara kumi kwa mwezi si mchezo
   
 19. Buchanan

  Buchanan JF Diamond Member

  #19
  Oct 8, 2009
  Joined: May 19, 2009
  Messages: 13,203
  Likes Received: 371
  Trophy Points: 180
  Watanzania lini wakawa wakweli? Any way, kwa sasa madaktari wa Rais tuwape 'benefit of doubt!' Mheshimiwa apone ili mwakani tuone itakuwaje kwenye uchaguzi: kaulimbiu za kasi mpya, maisha bora kwa kila mtz, blah, blah,...blah!
   
 20. Kevo

  Kevo JF-Expert Member

  #20
  Oct 8, 2009
  Joined: Jun 12, 2008
  Messages: 1,332
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Kwani ana Ugonjwa gani Mkuu?
  Labda weye wajua hebu tudokeze na wengine!!
   
Loading...