Taarifa sahihi za kilimo.

Blank page

JF-Expert Member
May 28, 2015
4,728
3,172
Habari wakuu na wadau wa kilimo?
leo katika pita zangu mtandaoni,nikampitia millardayo...nimekuta akihojiana na wakuvanga mchekeshaji kutoka kundi la orijino komedi...ambaye ameamua kuingia katika kilimo cha kulima mazao ya nafaka kama vile mpunga,mahindi na maharage though hajataja eneo analofanya hiko kilimo....sijatoka patupu nimeweza kuapata mawili matatu naomba kushare nanyi...samahani video sijaweza kuipost but ntasummarize alichokisema then ndiyo itakuwa mada tuijadili hapa.
kwana ameelezea kwamba kabla au ukiwa ndani ya kilimo ufahamu mambo yafuatayo..
1.aina ya ardhi unayoenda kulima
2.hali ya hewa ya eneo
3.wadudu
4.mtaji
5.changamoto zinazokabili wakati sasa na badae
6.soko lako.
sijayapangilia hapo juu ila nimeyataja tu,nadhani itaeleweka.
lakini kingine,ni anasema ukosefu wa taarifa sahihi za kilimo,kwamba kuna wakulima ambao hawapendi kushare au kutoa taarifa kwa wale wanaohitaji kuingia katika kilimo.je hili ni kweli? na kama kweli kwanini wakulima hawa wanafanya hivyo?
lakini kingine ni amezungumzia kuwa tanzania tuna ardhi kubwa sana pamoja na maji ya kutosha,kiasi kwamba eti sehemu zingine unakuta unauziwa shamba au eneo lipo karibu kabisa na maji eka kwa shillingi 10000 (naomba tusizingatie sana hapa ila kama inaweza kuwa kweli unaweza kutoa ushuhuda) hili nalo vp ni kweli tanzania tuna ardhi kubwa kwa ajili ya kilimo?
mwishop kabisa,kazungumzia kuwa vijana waingie kwenye kilimo kwa ajili ya kuepusha malalamiko ya ukosefu wa ajira,vilevile kuchangia [pato la taifa.
imeeleweka sana,naomba tulijadili hili la kilimo kwa mapana na kwa faida au jinsi gani vijana tunaweza kupata hizo fursa.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom