Taarifa Rasmi Kutoka Kwa Meya wa Kinondoni Kuhusu Kukamatwa

Mwanahabari Huru

JF-Expert Member
Mar 9, 2015
14,243
34,903
Nimepigiwa simu kuwa natafutwa na imetolewa hati ya kukamatwa mimi, mstahiki meya manispaa ya Kinondoni.

Ukweli ni kuwa siku ya leo, palikuwa na shauri la kesi, mahakama ya Kisutu, mbele ya hakimu, mheshimiwa Mama Liwa, siku ya 02 May 2016.

Kesi hii nawakilishwa na mawakili wawili, Adv J.malya na Adv F.kiwelo,
Kwa kuwa leo nilikuwa na hudhuru, nimewakilishwa na mdhamini wangu, Mwakatika mtumishi wa CHADEMA makao makuu, baada ya kuomba niweze kuhudhuria mazishi ya aliyekuwa mjumbe wa serikali ya mtaa Ubungo Msewe, katika ratiba ya kumuaga leo 02 May, saa mbili asubuhi ndani ya hospitali ya Lugalo.

Na baada ya mazishi nikiwasikiana na Adv F.kiwelo, aliyekuwapo mahakamani na mdhamini wangu, kuwa kesi imehairishwa mpaka siku ya tarehe 16 may 2016, ikumbukwe kesi imehairishwa zaidi ya mara tano, tunasubiria mashahidi wapatikane.

Mpaka mawakili wanaondoka mahakamani na mdhamini, hakuna maombi ya hati wala hati iliyotolewa ya kukamtwa mimi.

Na baada ya mawasiliano na wakili baada ya mazishi, saa tano nimehudhuria baraza la madiwani jiji la Dar es salaam.

Ambapo kikao kimeisha muda huu wa jioni 12.30 na hapa mtumishi wenu mstahiki meya manispaa ya Kinondoni, niko njiani kwenda Morogoro, kuwahi kesi nyingine 03 May 2016, mahakama ya mkoa wa Morogoro mbele ya hakimu, mheshimiwa E.Rwehumbiza, nawakilishwa na adv. Tarimo.

Kwa kuwa kunataarifa hizo zisizojulikana chanzo chake, nimewaomba mawakili kurudi kesho asubuhi, mahakama ya kisutu, kujua ukweli wa taarifa hizo au kitu chochote kilichojificha nyuma ya pazia, kesi zote ni za kisiasa, wakati na kabla ya uchaguzi.
 
Dah, siku hizi mitandao inapotosha sana mambo.

Watu wanaweza kupika ishu nzito wakaisambaza balaa.

Ngoja tusubiri hiyo kesho tuone nini kinaendelea
 
Kweli kuishiwa marafiki kwaweza kukufanya hata mamako ukamwita mchawi. Kwa nini tumefikia mahali pa kuzuliana uongo mbaya hivi jamani? Tuseme kwa mfano, Mstahiki meya akifungwa, weye mleta mada hii humu jf utapata nini hapo?
Mbona mafisadi hawa waliozoea kuleana wanakasirika hivi kuona upinzani ukiongoza?? Wapeni kanafwasi wajameni tuwapime hawa wapinzani kwa utendaji wao halali si kwa mbinde za mchana hivi. INATIA HASIRAAAAAAAAAAAAAAAA
 
Kweli kuishiwa marafiki kwaweza kukufanya hata mamako ukamwita mchawi. Kwa nini tumefikia mahali pa kuzuliana uongo mbaya hivi jamani? Tuseme kwa mfano, Mstahiki meya akifungwa, weye mleta mada hii humu jf utapata nini hapo?
Mbona mafisadi hawa waliozoea kuleana wanakasirika hivi kuona upinzani ukiongoza?? Wapeni kanafwasi wajameni tuwapime hawa wapinzani kwa utendaji wao halali si kwa mbinde za mchana hivi. INATIA HASIRAAAAAAAAAAAAAAAA
wivu,chuki na ghadhabu zitaimaliza c.c.m!
 
Chapa kazi kaka Lissu yupo na Serikali inajua haiwezi kifua chake ktk sheria.Songa mbele mh.Mstahiki meya wa Watanzania.
 
Ukawa mnahubiri Magufuli afuate utawala Wa sheria ,alafu nyinyi mkiitwa na mahakama hamuendi!!!!


Ukiwa ni janga la taifa.
 
Yaani vijna wa lumumba wanamua kumchafua mheshimiwa meya kwa manufaa yanani?
 
Back
Top Bottom