Taarifa muhimu juu ya maendeleo ya CHAWADE

Taarifa muhimu juu ya maendeleo ya CHAWADE

chawade

Member
Joined
Nov 21, 2014
Posts
21
Reaction score
3
CHAMA CHA WANANCHI NA DEMOKRASIA
CHAWADE



Phone: +255 789113534, +255 715 039991
Mw/Chai – Matombo na Gombero (house No 28)
chamachawade@yahoo.com


Taarifa kwa Umma

Ndugu wanachama wa CHAWADE, napenda kuchukuwa fursa hii adimu kwa heshima kubwa kuzungumza nanyi kupitia WARAKA huu, mambo muhimu juu ya maendeleo ya chama chetu kitukufu CHAWADE.

Jambo la kwanza ambalo napenda kuzungumza nanyi ni hili la maendeleo ya taratibu za usajiri wa chama chetu. Hadi sasa, taratibu zote zinaendelea vizuri juu ya USAJIRI WA KUDUMU hata hivyo kuna changamoto kadhaa ambazo natumaini tutaweza kuzikabili na hatimaye kupata usajiri wa KUDUMU.

Matarajio yetu ni kuwa kama hapatakuwa na mizengwe kwenye tarehe 20/06/2015 tunaweza kuwa tumepata usajiri wa KUDUMU.

Ndugu wanachama, jambo la pili ambalo napenda kuwafahamisha ni juu ya idadi ya wanachama hadi sasa. Kwa juhudi kubwa ambazo viongozi wa chama chetu wamekuwa wakizifanya juu ya kupata wanachama wapya, hadi sasa ninapowaandikia waraka huu, chama chetu kimefikisha wanachama elfu nane na thelathini na tatu (8,033).

Ndugu wanachama, jambo la tatu ambalo napenda kuwafahamisha ni juu ya ushiriki wetu kwenye UCHAGUZI wa mwaka 2015. Katika uchaguzi wa mwaka huu napenda kuwajulisha kuwa tutashiriki kikamilifu kwa kuweka wagombea kwa nafasi za ngazi mbali mbali (URAIS, UBUNGE NA UDIWANI) katika maeneo yote ndani ya nchi yetu.

Ndugu wanachama, endapo itatokea chama chetu kikawa bado hakijapata usajiri wa kudumu hadi kipindi cha uchaguzi, uongozi wa chama chetu utatoa TAMKO juu ya chama gani na wagembea wepi CHAWADE itawaunga mkono kwa mantiki hiyo tuwe na subira muda ukifika tutafahamishana.

Kwa kumalizia, ndugu wanachama, napenda kuwaomba kuendelea kuwa na SUBIRA pamoja na uvumilivu maana chama chetu bado kipo kwenye mchakato wa kupambana na kuhakikisha tunapata usajiri wa KUDUMU.

Nawashukuru sana kwa ushirkikano wenu katika kukijenga chama chetu.

Asanteni sana na Mungu awabariki.

CHAWADE!!! KWA PAMOJA TUTASHINDA!!!


Shabiri Mpaka
Mwenyekiti Chawade Taifa.

 
Ccm wamewatuma mlinganishe majina na chadema kusudi muwape wananchi utata ,majina mlikosa ccm mna kazi mwaka huu mpaka mtaugua kuhusu Chadema!!
 
Ha ha ha! Wallahi kuelekea uchaguzi mkuu tutashuhudia mengi. Yaani mmetumwa na magamba mchote kajineno kamoja kamoja kutoa vyama vikuu (CUF & CHADEMA) halafu mfinyange-finyange ili kaendane-endane na CHADEMA. Eti Chama cha "Wananchi" na "Demokrasia". Kweli ujinga ni mzigo.
 
Ccm wamewatuma mlinganishe majina na chadema kusudi muwape wananchi utata ,majina mlikosa ccm mna kazi mwaka huu mpaka mtaugua kuhusu Chadema!!

Nipo apa mwembe chai sijui ata izo ofisi zao zipo wapi...pia si USAJIRI ni USAJILI.....
 
Hahahahahahahahahahaha duh,izo kura bora muwape ACT wazalendo na sio ile saccos
 
Huu ni upuuzi uliopitiliza, hata kama ndo demokrasia,this is too much now.

Kuna haja ya kuwa na utaratibu hata wa kisheria kudhibiti ama kuzuia uanzishwaji wa vyama vya siasa wakati kama huu.

Haiwezekani watu waibuke tu from no where eti wanaanzisha CHAMA miezi mitano kabla ya uchaguzi na kujipanga kushiriki general election.
HUU NI UTAPELI MKUBWA.
 
Haaaaahaaaa baada ya ngoma ya ACT kubuma sasa ccm wameamua kushabihisha majina ili kuwaghilibu wananchikweli nimeamini kuwa ccm kinafariki mwaka huu
 
Ccm wamewatuma mlinganishe majina na chadema kusudi muwape wananchi utata ,majina mlikosa ccm mna kazi mwaka huu mpaka mtaugua kuhusu Chadema!!

Mkuu Rabuor asante kwa kunisemea,hyo ni mbinu zaifu mno
 
Last edited by a moderator:
Hii nchi inabidi iweke kwenye maajabu ya dunia
 
Mbinu zilezile na makosa yaleyale. Mlikosea rangi ya gwanda na mkamvisha berreti na matokeo ya impact yake ikawa negligible.

Sasa mnakosea jina na timing, angalau jina lingekuwa chadewa. Chama cha demokrasia na wananchi.

Utawala huu umefitinika mbele za Mungu na ulimwenguni pia kwa kujawa na tamaa za mali na kuwasahau wananchi wengi walio maskini na wenye maisha duni kabisa. Kilio chao kimesika mbele ya Mungu na utawala huu unaenda kuanguka tena kwa kishindo kikubwa.
 
​Mkuu hawa ni wahuni na wasaliti wengine ambao hawakuona umuhimu kwa kuunda chama muda wote uliopita mpaka miezi minne kabla ya uchaguzi. Hawa ni wa kuwapotezea tu hawana maana yoyote.

MANI lusungo BAK tpaul na wengineo, huyu mgeni Chawenge sorry Chawade mshakutana nae? Hahahahhahaa zumbemkuu lete miguu yako hapa
 
CCM wanahangaika sana kipindi hiki maana litawi lao ACT limekauta halichipuki tena
 
​Mkuu hawa ni wahuni na wasaliti wengine ambao hawakuona umuhimu kwa kuunda chama muda wote uliopita mpaka miezi minne kabla ya uchaguzi. Hawa ni wa kuwapotezea tu hawana maana yoyote.

Halafu chama kinasajiliwa ndani ya miezi 6 tu ili kiwahi uchaguzi.
 
Back
Top Bottom