Abdul Nondo
JF-Expert Member
- Oct 28, 2016
- 525
- 2,951
*TAARIFA KWA WANAFUNZI WOTE WALIOOMBA MKOPO TANZANIA 2017/2018*
Mtandao wa Wanafunzi Tanzania, (TSNP), unapenda kuwajulisha wanafunzi wote walioomba mikopo ya kuwa, tunakusanya maoni juu ya changamoto mbalimbali zinazowakumba na zilizowakumba wanafunzi katika zoezi la uombaji wa mikopo ili bodi ya mikopo iweze kuyafanyia kazi haraka iwezekanavyo.
TSNP inaendesha zoezi la kukusanya maoni hayo baada ya leo (tarehe 4 Sepetmba, 2017), kupokea maelekezo kutoka kutoka kwa Mkurugenzi Mtendaji wa bodi ya mikopo(HESLB), Abdulrazaak Badru akiomba tupeleke maoni na mapendekezo ya wanafunzi juu ya changamoto walizopitia katika uombaji wa mikopo.
Mbali na maoni ya wanafunzi, pia taasisi yetu tunaanda maoni yetu ambayo tutayaambatanisha pamoja na maoni ya wanafunzi na kuyapeleka HESLB siku mbili zijazo (6 Septemba, 2017).
Hatua hii ya inakuja baada ya TSNP kupaza sauti kupitia vyombo vya habari, Septemba Mosi, 2017 juu ya dosari na changamoto nyingi zinazowakumba wanafunzi katika uombaji wa mikopo kupitia mfumo mpya.
Katika tamko hilo, taasisi yetu iliiomba Bodi ya Mikopo iweka wazi majina ya waliokosea kuomba ili wanafunzi warekebishe makosa yao, badala ya kutangaza tu kuwa wapo wanafunzi waliokosea bila kuorodhesha majina yao kama ilivyokuwa ikifanyika miaka iliyopita.
Kuhusu hoja ya kutoa orodha ya majina hayo ili wanafunzi warekebisha taarifa zao Mkurugenzi wa Bodi amesema kuwa ingawa wana muda mdogo (fixed timetable)(kufuata Almanac)kuelekea kufunguliwa kwa vyuo lakini wanalifanyia kazi wazo hilo la kutoa nafasi kwa marekebisho.
Katika hatua nyingine, Badru amesema mwanafunzi yeyote ambaye ameomba mkopo na anahisi amekosea sehemu yoyote, aandike barua kueleza amekosea nini, wakati HESLB ikiangalia namna ya kutoa muda wanafunzi kurekebisha taarifa zao, hasa waliokosea.
Tunaipongeza bodi kwa hatua hii ya awali ya kutaka kuchukua hatua katika utatuzi wa changamoto za wanafunzi tulizozibainisha.
TSNP tunaendelea kukusanya maoni ya wanafunzi na hata wazazi, walezi na wadau wa elimu mnaofuatilia kwa karibu mfumo mpya wa uombaji wa mikopo.
Tuma maoni yako kupitia ujumbe mfupi:
Simu:
*0762082783*
*0659366125*
Barua pepe:
tsnp.students@yahoo.com.
Abdulnondo10@gmail.com.
TUNAOMBA USAMBAZE TAARIFA HII NAMNA UWEZAVYO.
Imetolewa na TSNP kupitia kwa;
Abdul Nondo,
Kaimu Mkurugenzi Idara ya Haki na Wajibu wa wanafunzi.
Sent using Jamii Forums mobile app