Taarifa kwa umma

Taarifa kwa umma

SIMBA mtoto

JF-Expert Member
Joined
Jul 13, 2011
Posts
204
Reaction score
100
TAARIFA KWA UMMA

KUKOSEKANA HUDUMAYA MAJI KWA SIKU MBILI JIJINI DAR

Dawasco inawatangazia wakazi wote wa jiji la Dar es salaam na Mji wa Bagamoyo kuwa mtambo

wa kuzalisha Maji wa Ruvu Chini utazimwa kwa wastani wa saa 48 kwa siku za Ijumaa na Jumamosi

ya tarehe 23 na 24 Januari 2015, kuanzia saa kumi na mbili asubuhi, ili kuruhusu mkandarasi
(Sino-hydro Corporation ltd) kuunganisha bomba la zamani na bomba jipya
(Cross-connection) ndani ya Mtambo wa Ruvu Chini , Bagamoyo.

Kuzimwa kwa mtambo wa Ruvu Chini kutasababisha maeneo yafuatayo kukosa Maji; Mji wa Bagamoyo, Mapinga, Bunju, Boko, Tegeta, Kunduchi, Salasala, Jangwani, Mbezi beach na Kawe.

Maeneo mengine ni Mlalakuwa, Mwenge, Mikocheni, Msasani, Sinza,Manzese, Mabibo, Kijitonyama,

Kinondoni, Oysterbay, Magomeni, Upanga, Kariakoo, City Centre, Ilala, Ubungo Maziwa, Kigogo, Mburahati,

Hospitali ya rufaa Muhimbili (MNH), Buguruni, Changombe na Keko.

Wananchi mnashauriwa kuhifadhi maji ya kutosha na kuyatumia kwa matumizi ya lazima.

Au wasiliana na kituo cha huduma kwa wateja namba 022-2194800

Dawasco inaomba radhi kwa usumbufu wowote utakaojitokeza.

Imetolewa na ofisi ya uhusiano,Dawasco
-
Makao Makuu
.
 
tarehe 23-24/january 2015 kwa masaa 48.

hadi leo trh 2/2/015.

kwa maulizo piga namba
022-2194800

au tafuta maji yako
 
...huku sisi, tumejitengenezea visima vyetu.
 
Nimecheka hadi basi yaani hili tangazo limekaa utadhani bongo daslama maji ya bomba bwelelee, kumbe ni usanii mtupu..hamna maji wala nn watu ni maji ya ndoo kwa kwenda mbele miaka 50 ya uhuru ...mazafanta siondoki kwa Obama hata unifungie kwenye sanduku la chuma HAONDOKI MTU HUKU....
 
Back
Top Bottom