Taarifa kuwa Bugando wamesitisha mgomo ni za uongo

drgeorge

Member
Jun 22, 2009
99
23
Taarifa iliyotolewa na TBC kuwa madaktari wa bugando wamesitisha mgomo kwa kile walichokiita kuchoka kuburuzwa si za kweli, ni propaganda ya watu fulani kwa lengo la kujisafisha na kuupotosha umma wa watanzania.

Madaktari hawafanyi propaganda wana madai ya msingi ambayo wanayasimamia, na mgomo bugando upo.

Kilichotokea ni kwamba, kuna wajinga fulani walibandika kijitangazo usiku wa manane kuwa eti hawataki kuburuzwa na wakajiita G25, nadhani walikuwa wanakumbushia ile ya wabunge waliojiita G55 enzi nzileee. sasa wakati kinajadiliwa hicho kijiujumbe asubuhi kumbe waandishi wameitwa na kupewa kuwa ndo news ya kuripoti hiyo.

Hakuna hata mtu mmoja aliyejitokeza kuhusika na kijitangazo hicho. Ni upuuzi wa hali ya juu.

Viongozi waongo ndo wataiangusha hii serikali maana wataipotosha nayo itapotoka na kuchukua maamuzi mabovu na mwisho mpotoko huo unaweza kuzaa mengine

Chanzo cha habari ni mimi mweneywe, nipo bugando
 
Wakati nchi zingine na serikali zao wakiwekeza kupunguza vifo na kutafuta namna ya kuongeza umri wa kuishi, sisi ndo kwanza tunazidi kujitenganisha kati ya wananchi na serikali. Serikali haiko kwa nia ya kulinda wananchi na uhai wao bali ipo kwa ajili ya kikundi fulani cha watu fulani fulani wenye maslahi yao binafsi.!! Too sad!
 
Taarifa iliyotolewa na TBC kuwa madaktari wa bugando wamesitisha mgomo kwa kile walichokiita kuchoka kuburuzwa si za kweli, ni propaganda ya watu fulani kwa lengo la kujisafisha na kuupotosha umma wa watanzania.

Madaktari hawafanyi propaganda wana madai ya msingi ambayo wanayasimamia, na mgomo bugando upo.

Kilichotokea ni kwamba, kuna wajinga fulani walibandika kijitangazo usiku wa manane kuwa eti hawataki kuburuzwa na wakajiita G25, nadhani walikuwa wanakumbushia ile ya wabunge waliojiita G55 enzi nzileee. sasa wakati kinajadiliwa hicho kijiujumbe asubuhi kumbe waandishi wameitwa na kupewa kuwa ndo news ya kuripoti hiyo.

Hakuna hata mtu mmoja aliyejitokeza kuhusika na kijitangazo hicho. Ni upuuzi wa hali ya juu.

Viongozi waongo ndo wataiangusha hii serikali maana wataipotosha nayo itapotoka na kuchukua maamuzi mabovu na mwisho mpotoko huo unaweza kuzaa mengine
Chanzo cha habari ni mimi mweneywe, nipo bugando

Nlitarajia hili tangu nlipoanza kusikia mara sijui mahakama,mara wazee...hili gvt wamezoea kulitumia kama njia ya kupata cha kuadress kwa umma kuwafeva....
 
naomba kujua hivi HBEVDNA test ni bei gani?. Muhimbili wanazo Gastroscope?...Nasikia wanapeleka kupimia Agakhan sijui...Hatari kama ndiyo hivyo kweli doctors wanahaki ya kudai uboreshwaji wa mazingira ya kazi. As a doctor sitapenda kupokea wagonjwa and at the end of the day sina vitendea kazi vya kuwatibia, then I just watch them dying.
 
Ndiyo maana madokta walitoa onyo mapema juu ya upotoshaji wa habari za namna hii.
 
ni imani yangu kwamba Serikali huwa ndipo pahala ambapo yeyote anaweza kupata ukweli wa kitu chochote. Lakini sio hapa kwetu maskini ukitaka kudanganywa basi nenda serikalini. Mungu tusaidie
 
Back
Top Bottom