​kwa mtu mwenye busara na akili japo ndogo tu,huwa anakuwa na tabia ya kuhisi aibu hasa pale linapozuka suala ama jambo lolote lililo na chembechembe za uhuni, upendeleo na hata dhuluma, na bahati mbaya sana huyo mtu akagundulika na kudhibitika kuhusika kwenye tuhuma hizo zinazomsibu.
Hawa ndugu zetu kiukweli walitumia akili kuokoa familia zao lakini tu walikosea katika kufanya sampling ambayo ndiyo ilitibua mambo mara tu baada ya wazalendo na wenye machungu na nchi yao kuligundua hilo na kuamua kulivalia njuga, mpaka pale mambo yalivyokuwa kama yalivyo; nampongeza sana aliyelifanya hilo.
Lakini vilevile kwa mtazamo wa kawaida tu usiohitaji degree yeyote ile, huenda hata hawa walioko kwenye idara ya Utumishi nao wameoza kimaadili, kwa sababu haiwezekani na wao waruhusu itokee kama ilivyotokea ni hujuma na kutokutumia AKILI katika kufanya mambo yao, kwa hiyo kwa ufupi tu ni kwamba; nao pia HAWAFAI KABISA.
Hebu chukulia mfano tu kwamba ni michakato mingapi hawa watu wameziendesha mpaka sasa na mpaka kufikia kukamatwa ni dhahiri kabisa kwamba huu UHUNI wa aina hii ulianza zamani yaani "
Mtoto wa mtanzania Kabwela aliyesoma kwa mkopo, mkopo ambao pia kila kukicha matangazo yanayosisitiza kurejeshwa kwake hayakatiki kwenye vyombo vya habari, hata kufikia kutaka kuzuiwa kwa utoaji wa VIZA kwa hawa Makabwela ambao hasa ndio walengwa kwa sababu ni wao ndio hawataweza kuurejesha huo mkopo, na istoshe wanatambua wazi kwamba HAWA watanzania makabwela hawajapata ajira kwa sababu hawana mtu wa kuwashika mkono.
Wao utawasikia kwenye vyombo vya habari walivyo na moyo wa kusisitiza vijana kujiajiri,wasitegemee kuajiriwa Hebu muulize yeye anayesema hivyo kama mtoto wake amejiajiri?na kama amejiajiri tayari si kwao pesa zipo?
Je huyu Kabwela yeye atatoa wapi mtaji huo wa kujiajiri? Na wengine watasema kuwa MAKABWELA tukakope pesa benki pale ambapo wanatambua hakika kuwa huyu KABWELA mimi siwezi kutimiza vigezo.
Wamebana kila kona hatuna pa kupumulia, Hajira zikitoka wanazikwapua zote, serikali ikitoa mtaji vigezo lundo ili tushindwe,HIVI huyu mtoto wa maskini anapoangaika kutoka MASUMBWE tena kwa basi lenye hadhi ya daraja la TATU siyo kwa sababu hakuyaona hayo yenye hadhi nzuri ama LUXURY zinaitwa, La hasha! lakini ni kwa sababu tu, hana uwezo huyo.
Huyu Mzalendo kabwela anapakia gari kutoka kijijini kwao BUZIMBWE huko Bunda mkoani Mara, ambaye pia hana ndugu wala pa kufikia Dar es salaam anakoitwa kwenye usaili unaochukua takribani siku kadhaa, WAO wakitambua kuwa huyu mtu anapata mateso na manyanyaso makubwa, wanaendelea kumzungusha ili aendelee kupoteza siku DAR ili awakingie kifua watoto wa vibosile ionekane kwamba usaili ulikuwa wa h- yaani hawa ndio watanzania halisi ambao majina yao yanapitishwa kwa MEMO nitakwambia maana ya memo baadaye.
Ninayo mambo mengi ya kuwaambia watanzania wenzangu lakini kwa sababu hayaishi nadhani nitafungua jarida maalumu kwa ajili ya kutoa elimu japo ya USTAARABU kwa HAO wanaojiita WATANZANIA HALISI ili waweze kuwajali hata hawa ndugu wakambo WAZALENDO MAKABWELA japo kwa likombe cha kahawa.