Taarifa kuhusu watumishi wa umma kuuziwa fomu za OPRAS

R.B

JF-Expert Member
May 10, 2012
6,296
2,575
TAARIFA KUHUSU WATUMISHI WA UMMA KUUZIWA FOMU ZA OPRAS
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIAOFISI YA RAIS​


FOMU YA TATHMINI YA UTENDAJI KAZI (OPRAS) HAIUZWI​

Ofisi ya Rais-Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora inawaelekeza waajiri wote nchini kuhakikisha watumishi katika sehemu zao za kazi wanapata Fomu ya Wazi ya Mapitio na Upimaji Utendaji Kazi (OPRAS) kwa utekelezaji bila usumbufu.

Fomu za OPRAS zinapatikana katika Tovuti ya Ofisi ya Rais-Menejimenti ya Utumishi wa Umma yenye anuani, www.utumishi.go.tz. Waajiri wote wanaelekezwa kutembelea tovuti hii na kutoa nakala za kutosha kwa idadi ya watumishi katika maeneo yao ya kazi. Kwa watumishi wanaoweza kutoa fomu hizi wenyewe wanaruhusiwa kufanya hivyo.

Imebainika kuwa katika baadhi ya Taasisi za Umma watumishi wanaelekezwa kununua fomu za OPRAS kutoka kwa watu binafsi. Kitendo hiki ni kwenda kinyume cha Sheria, Kanuni na Taratibu zilizopo na pia ni usumbufu kwa watumishi. Fomu za OPRAS haziuzwi na watumishi hawatatakiwa kuzinunua.

Endapo Mtumishi atashawishiwa au kulazimishwa kununua fomu za OPRAS atoe taarifa Ofisi ya Rais-Utumishi na Utawala Bora ili hatua stahiki zichukuliwe. Waajiri wote wanakumbushwa kuwa ni wajibu wao kuwapatia watumishi walio chini yao fomu hizi na kuzihifadhi baada ya utekekelezaji na si vinginevyo.

Serikali ilianzisha matumizi ya Mfumo wa Wazi wa Mapitio na Tathmini ya Utendaji Kazi (OPRAS) Mwezi Julai 2004, kupitia Waraka wa Utumishi Na. 2 wa mwaka 2004. Hivyo kutoka wakati huo, OPRAS ilifuta mfumo wa zamani wa kupima utendaji kazi wa mtumishi kwa njia ya siri.

Mabadiliko ya kutathmini utendaji kazi wa Watumishi wa Umma kwa uwazi yanakwenda sambamba na Sera ya Menejimenti na Ajira katika Utumishi wa Umma ya mwaka 1998 kama ilivyorekebishwa mwaka 2008 ambazo zote zinasisitiza uwekaji wa mifumo ya menejimenti ya utendaji bora wa kazi inayojali matokeo.

Utekelezaji wa OPRAS katika taasisi za Umma ni hatua muhimu kwa Serikali katika kuboresha utendaji kazi na utoaji huduma kwa Umma. Hivyo ni wajibu wa kila mwajiri kusimamia na kuhakikisha kuwa watumishi wote walio chini yao wanajaza fomu hizo na kuwasilisha taarifa za utekelezaji katika Ofisi ya Rais-Utumishi na Utawala Bora bila kukosa.

IMETOLEWA NA KITENGO CHA MAWASILIANO SERIKALINI Kny: KATIBU MKUU OFISI YA RAIS-UTUMISHI
 
Serikalini kila kitu ni dili, kujaziwa tu hizo fomu vizuri na kwa haki ni dili
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom