Taanzia ya mashambulizi ya Sep. 11, 2001 USA

Yericko Nyerere

JF-Expert Member
Dec 22, 2010
16,987
20,271
Makala hii ni mswaada wa kitabu changu kiitwacho “Vita dhidi ya Ugaidi”.

Yote haya yalikuwa yamefanywa wakati wa kipindi cha Cliton, “kitu gani kinakusumbua sana siku hizi? Boren alimwuliza Tenet asubuhi hiyo. “Bin laden,” Tenet alijibu akimanisha kiongozi wa ugaidi Osama Bin laden raia wa Saudi Arabian aliyekuwa akiishi ukimbizini Afghanistan ambaye alikuwa ameanzisha mtandao wa Al Qaeda dunia nzima neno ambalo kwa kiarabu linamaanisha “ Kituo kikuu”. “Oh, Tenet!” Boren alisema kwa muda wa miaka miwili iliyopita alikuwa akisikiliza wasiwasi wa rafiki yake kuhusiana na Bin laden, je, mtu mmoja binafsi angewezaje bila ya kutumia utajiri wa serikali ya kigeni akawa tishio kubwa kama hili? aliuliza, “huwezi kufahamu uwezo na kiwango cha yale wanayoyapanga”, Tenet alisema. Boren alikuwa na wasiwasi kwamba rafiki yake alikuwa ameamua kuwa na chuki za ajabu dhidi ya Bin laden.

Karibu miaka miwili hapo nyuma muda mfupi tu kabla ya sherehe za kutimia kwa mwaka 2000 Tenet alikuwa amechukua hatua ambayo haikuwa ya kawaida kwa kumwonya binafsi Boren asisafiri au kutokea kwenye matukio makubwa ya wazi katika mkesha wa mwaka mpya kwa sababu alitegemea kungekuwa na mashambulizi makubwa. Na siku za karibuni zaidi, Tenet alikuwa na wasi wasi kwamba kungekuwa na mashambulizi wakati wa sherehe za tarehe 4 Julai 2001. japokuwa hakuyafichua hayo kwa Boren, kulikuwa na matukio 34 ya habari zilizonaswa miongoni mwa washirika wa Bin laden zikielezea matamshi kama vile “siku ya kiama ni kesho” au “ “tukio la ajabu ni kesho” Kulikuwepo na unaswaji mkubwa wa habari kama hizi katika mitandao ya ujasusi na ripoti nyingi zilisema kulikuwa na shambulio kubwa dhidi ya balozi za marekani au dhidi ya makundi ya watalii wa marekani nchi za nje, lakini habari za kijasusi hazikuweza kufahamu ni lini wapi na kwa njia gani. Hapakutokea chochote, lakini Tenet alisema kwamba suala hilo lilikuwa linamfanya akose usingizi.

Ghafla mara walinzi wa Tenet walikuja mbio kuelekea mezani alikokuwa.Uh-oh, Boren aliguna moyoni “Bwana Mkurugenzi”, mmoja wao alisema “kuna tatizo kubwa”. “Ni nini”” Tenet aliuliza akionyesha kwamba kwake ilikuwa ni vyema kumpa mtu uhuru wa kuzungumza bila woga . “mnara wa kituo cha Biashara umeshambuliwa.” Mmoja wao alimpa Tenet simu ya mkono na akapiga simu makao makuu. “Kumbe wameigongesha ndege kwenye jengo lenyewe?” Tenet aliuliza akiwa haamini. Aliamuru watu wake muhimu kukutana katika chumba cha mkutano kwenye makao makuu ya CIA, Akaagiza kuwa angekuwa amefika huko katika kipindi cha dakika 15 hadi 20. “Yote haya siku zote yamekuwa ni Bin Laden,” Tenet alimwambia Boren. “Lazima niondoke” pia alifahamu kwamba uwezekano halisi ni kwamba CIA na shirika la upelelezi la Marekani (FBI) havikufanya yote yanayotakiwa ili kuzuia shambulio hilo la kigaidi.” 25 “Nashangaa,” Tenet alisema, “iwapo hii inahusiana na jamaa huyu ambaye anachukua mafunzo ya kurusha ndege.” Alikuwa akizungumza kuhusu Zacarias Moussaoui raia wa Ufaransa mwenye asili ya Morocco ambaye FBI ilikuwa imemtia kizuizini huko Minnesota mwezi uliopita baada yakuonyesha tabia za ajabu wakati akiwa katika shule ya mafunzo ya kurusha ndege. Tukio hilo la Moussaoui likiwa bado liko katika mawazo yake.

Mnamo Agosti, FBI ilikuwa imeomba CIA na wakala wa Usalama wa Taifa kufuatia simu zote ambazo Moussaoui alikuwa amezipata nchi za nje. Mtu huyo alikuwa tayari faili lake limetuna makaratasi ya unene wa inchi tano katika ofisi hiyo ya ujasusi wakati Tenet anaingia katika gari lake kwenda kwenye makao makuu ya CIA ambayo yana eneo la hekta 258 huko Langley Virginia, juhudi zake za kupigana dhidi ya ugaidi wa siku za nyuma zilikuwa zikipishana kichwani mwake. CIA ilikuwa inamwinda Bin laden kwa zaidi ya miaka mitano na juhudi hizo zikazidi baada ya ulipuaji mabomu wa mwaka 1998 wa balozi wa Marekani nchini Kenya na Tanzania ambao ulisimamiwa na Bin laden na kuacha watu zaidi ya 200 wakiwa wamekufa. Wakati huo, Rais Clinton alielekeza jeshi la Marekani kufyatua makombora 66 katika kambi za magaidi ambako Bin laden anasadikiwa kuwa alikuawa akifanya mkutano muhimu . Lakini ni wazi alikuwa ameondoka masaa machache kabla ya makombora hayo kufika sehemu hiyo. Mwaka 1999, CIA ilianzisha harakati za siri za kutoa mafunzo kwa makomandoo 60 kutoka katika shirika la ujasusi la Pakistan ili kuingia Afghanistan kumteka Bin laden. Lakini harakati hizo zilikwama kutokana na mapinduzi ya kijeshi yaliyotokea nchini Pakistan. Njia nyingi zaidi na za hatari zilikuwa zimepangwa katika mfululizo wa mikutano na maofisa wa ngazi za juu wa usalama wa taifa katika utawala wa Clinton.

Moja ya chaguo ambalo lilikuwa limefikiriwa lilikuwa ni shambulio la usiku kutoka kwenye helikopta dhidi ya Bin laden kwa kutumia kikosi kidogo maalum cha Marekani chenye watu wapatao 40, shambulio hilo lingehitaji ndege kupatiwa mafuta zikiwa angani kwani helkopta hizo zingelazimika kusafiri kiasi cha maili 900. Lakini mpango huo ulivurugika kutokanaka na oparesheni “Desert One” ya mwaka 1980 ambayo Rais Carter aliamuru ifanywe ili kuwaokoa mateka wa Marekani waliokuwa wanashikiliwa nchini Iraq ambapo ndege kadhaa zilianguka jangwani na kuangushwa, kama helikopta mbili aina ya “Black hawk” nchini Somalia mwaka 1993 na kusababisha vifo vya Wamarekani 18. Jeshi lilisema kwamba shambulio dhidi ya Bin Laden lingeweza kushindwa na kusababisha hasara kubwa kwa askari wa Marekani, Habari za kijasusi pia zilionyesha kwamba Bin Laden alikuwa akifuatana na familia yake, na Clinton alikuwa anapinga oparesheni yoyote ambayo ingeweza kuua wanawake na watoto.

Kikosi maalum cha Marekani na askari wa jeshi la maji wenye uwezo wa kurusha makombora aina ya ‘cruise’ waliwekwa katika tahadhari lakini walihitaji masaa sita hadi kumi kuweza kupata tahadhari ya mahali alipokuwa Bin Laden. Moja ya siri zenye kulindwa zaidi katika CIA ilikuwa ni ile ya mawakala 30 wa kijasusi wa Afghanistan waliokuwa wakiendesha shughuli zao chini ya maneno ya siri GE/SENIORS, ambao walikuwa wamepewa fedha kwaajili ya kufuata nyendo za Bin laden nchini Afghanistan. Katika miaka mitatu iliyopita kundi hilo ambalo lililipwa dola 10,000 kila mwezi liliweza kusafiri pamoja au kugawanyika katika vikundi vidogo vya watu watano. CIA kila siku ilikuwa na vyombo salama vya mawasiliano “the Seniors” kama walivyokuwa wakiitwa, na walikuwa wamenunuliwa magari na pikipiki lakini kuzifuatia nyendo za Bin laden likawa jambo gumu zaidi kwani aliweza kusafiri bila mpangilio na kila mara akiondoka nyakati za usiku au kuwalamba chenga za visigino akipita milimani.

Kitu cha ajabu ni kwamba seniors hao waliweza kujua wakati wote mahali alipokuwa lakini kamwe hawakuweza kutoa habari thabiti za vitendo yaani kusema kithibiti kwamba angeendelea kukaa mahali hapo kwa muda unaotakiwa ili kuweza kulenga makombora ya ‘cruise’ mahali hapo. Na CIA ilishindwa kupata mtu wa kuaminika ili kufanya ujasusi miongomi mwa watu wa Bin laden ambaye angeweza kuwadokeza kuhusu mipango yake. Kulikuwa na watu katika utawala wa Clintoni na vyombo vya usalama wa taifa walikuwa hawana imani na seniors kwa vile kuna wakati kulikuwa na habari za kupingana kuhusiana na mahali alipokuwa Bin laden. Na nchini Afghanistan watu hususani wenye kuleta habari za kijasusi walikuwa wananunuliwa na kutoa habari kwa watu wengine .Hadi sasa, si Clinton au Bush waliokuwa wametoa madaraka kwa CIA kutuma seniors au mawakala wengine wenye kulipwa kwenda kumuua Bin laden. Amri ya kirais kupiga marufuku mauaji ambayo ilisainiwa kwanza na Rais Gerald Ford , ilikuwa na nguvu ya kisheria. Katika kipindi kimoja kiongozi wa Seniors wa Afghanistan alikuwa amekutana mara kadhaa na mkuu wa kituo cha CIA kutoka Islamabad, Pakistan, ambaye alikuwa anawapa maelekezo na kuwalipa. Kiongozi huyo wa seniors alidai kwamba walikuwa wameurushia risasi msafara wa Bin laden katika matukio mawili katika kujihami, jambo ambalo lilikuwa linaruhusiwa lakini alitaka kuufuatilia msafara huo kwa njia nyingine akiwa anapendekeza kuvamia kwa kushitukiza ambapo kitu chochote kilicho karibu kitapigwa risasi, kuua kila mtu na kisha kukimbia.Mkuu wa kituo cha CIA alisema, Hapana hamuwezi kufanya hivyo jambo hilo litavunja sheria za Marekani. Kwa kutilia maanani fedha iliyokuwepo, vitengo mbali mbali vya siri na mazingira yaliyokuwepo, Tenet aliona kwamba CIA ilikuwa imefanya kila kitu kilichotakiwa kufahamika.

Lakini kamwe hakuomba kubadilishwa kwa sheria alikuwa hajamwambia Clinton kuwepo kwa mfumo wa kijasusi ambao ungewaruhusu Seniors kumvamia kwa kumshambulia Bin laden. Mwanasheria kwenye Wizara ya sheria Ikulu aliamini wangekataa na kusema kwamba hali hiyo ingekuwa imevunja sheria ya kupiga marufuku mauaji ya 27 watu. Tenet aliona amefungamanishwa na msimamo wa Clinton na washauri wake. Kila kitu kimefungiwa “sheria ya kufa”, alikuwa akisema lakini na yeye pia alikuwa amechangia katika hali hiyo katika kipindi chake cha miaka mitano na nusu akiwa kama mkuu wa habari za Ujasusi wa Clinton na Naibu wa idara hiyo. Sheria ilikuwa inasema kwamba CIA ingeweza kumkamata Bin laden na kumfikisha katika vyombo vya sheria.

Operesheni kubwa ya kufanya kazi hiyo iliwekwa katika ratiba za njama siri za idara hiyo. Tenet alikuwa ana amini kwamba Bin laden asingekubali kuchukuliwa akiwa hai, hivyo operesheni kama hii, iwapo ingefanikiwa, ingepelekea katika mauti yake. Lakini wataalam wote wa CIA katika kurugenzi ya Uendeshaji walifikiri isingefanya kazi na kwamba ingesababisha watu wengi kuuawa na si lazima awemo Bin laden. Na Tenet alikubali Mpango huo kamwe haukuendelea zaidi ya hapo. Pendekezo la Saudi Arabia kwamba CIA iweke silaha maalum katika mizigo ya mama wa Bin laden ambaye alikuwa anasafiri kutoka Saudi Arabia kwenda kumwona mwanaye nchini Afghanistan, pia lilikataliwa kwa vile lingekuwa la hatari na kwamba lisingefanikiwa.

CRAIG KELLY AMPA UJUMBE POWELL.

Huko mjini Lima, Peru, asubuhi hiyo, waziri wa mambo ya Nje Colin L. Powell alikuwa ndiyo kwanza ameanza kupata kifungua kinywa na rais mpya Alejandro Toledo. Powell alikuwa anahudhuria mkutano wa nchi za umoja wa Nchi za Amerika. .Alikuwa na mategemeo ya mawasiliano mema na mawaziri wa nchi za nje au viongozi 34 wa nchi 35 za eneo hilo.Cuba ilikuwa haikukaribishwa, Toledo alikuwa anasisitiza kuhusu mgao wa soko wa nguo kutoka Marekani . Alitaka kuondolewa kwa kodi katika pamba ya hadhi ya juu ambayo alidai isingeweza kushindanishwa na pamba ya hadhi ya chini iliyokuwa inazalishwa katika mataifa ya kusini ya Marekani ambayo ilikuwa inataka pawepo mgao huo katika soko. Ghafla mlango ukafunguliwa na Craig Kelly, msaidizi mtendaji wa Powell, aliingia haraka akiwa na ujumbe uliokuwa umeandikwa katika kipande cha karatasi kilichokuwa kimechanwa kutoka katika kitabu cha kumbukumbu .Ndege mbili zimejibamiza katika kituo cha Biashara cha kimataifa . Ndege mbili, si tukio la ajali, Powell alitambua .ujumbe wa pili ulisema kwamba ndege hizo zilikuwa ni za injini ya “jet” .Powell akafikiri, nilazima niende nyumbani. Hata kama kimetokea nini, hali ilikuwa ni mbaya mno kwake kuendelea kukaa katika mkutano wa mawaziri wa mamboya nje mjini Peru. “Hebu tayarisha ndege, alimwambia Kelly, Nenda kawaambie tunasubiri”. Ingechukua kiasi cha saa moja kuitayarisha ndege, hivyo Powell aliueleza mkutano huo. Mawaziri wengine walitoa hotuba za kumpa pole. Powell alizungumza kwa ufupi, akiwashukuru wajumbe wa mkutano huo kwa pole zao na kuahidi kwamba Marekani inachukua hatua mara moja “Mkasa mkubwa sana umeikumba nchi yangu,” alisema “Lakini….lazima mfahamu kwamba Amerika itapambana na wakosaji watafikishwa mbele ya haki. Mfahamu kwamba pamoja na siku hii kuwa mbaya kwetu, nilazima tutashinda kwani sisi ni taifa lenye nguvu na linalo jiamini duniani’ Wajumbe wengine walisimama nakupiga makofi.

Mara tu baada ya ndege kuondoka Powell alifahamu kwamba asingezungumza na mtu yeyote kwavile vyombo vyake vya mawasiliano vilikuwa vimeunganishwa na mfumo wa mawasiliano nchini Marekani ambao ulikuwa umejaa habari mbalimbali za ma wasiliano. Bila yasimu au barua pepe, alikuwa ni sawa na mtu ambaye hakuwa na nchi. Baada ya dakika kadhaa alikwenda mbele ya ndege kupiga mawasiliano ya radio. Hiyo ilimaanisha mawasiliano hayo hayakuwa na usalama. Alimpata Richard L Armitage, naibu waziri wa mambo ya nje na rafiki yake mkubwa, walizungumza mara kadha, lakini mazungumzo ya maana hayakuwezekana. Armitage ambaye alihitimu chuo cha jeshi la maji mwaka 1967 alikuwa ametumikia jeshi mara nne nchini Vietnam na baadaye akawa Naibu waziri wa ulinzi katika utawala wa Reagan. Alikuwa ni mtu mwenye kupenda kusema ukweli mwenye tambo kubwa na kifua kipana ambaye hakupenda kuzungumzia diplomasia yenye kujificha.

Hata kabla hawajawa wakuu wa wizara ya mambo ya nje Powell na Armitage walikuwa wakizungumza mara kadhaa kila siku. “Mtu huyu ninamwamini kuhusu uhai wangu, watoto wangu, hadhi yangu, kila kitu ambacho ninacho,” alikuwa akisema Powell kuhusiana na Armitage. Katika mambo yote ambayo Powell alikuwa anayachukia, ni kushindwa kuchukua hatua yoyote wakati wa tatizo ndilo jambo lililokuwa linashika nafasi ya kwanza. Jambo kuu katika upangaji wa sera za usalama wa taifa, na timu ya Ikulu au ya usalama wa taifa ingetaka kuweka msimamo gani katika upangaji wa sera kulikuwa kuna utaratibu wa kipekee katika nyakati za matukio makubwa. Hali ya migogoro ndiyo ilitoa fursa ya kuwepo hatari kubwa zaidi na fursa kubwa zaidi za utendaji wa kazi.

Ni mmarekani wa kwanza mweusi kuweka historia ya kuhudumu katika ngazi za juu za utawala wa Marekani Akiwa na umri wa miaka 64 katika kipindi cha mgogoro Powell alikuwa tayari amekaa katika viti vitatu vya chumba cha dharura vya Ikulu ambavyo ni mshauri wa kitaifa kwa Rais Regan kwa muda wa mwaka mmoja, kisha akawa mwenyekiti wa Muungano wa Wanadhimu kwa Rais Bush wa kwanza wakati wa vita vya Ghuba, na wakati mgogoro alikuwa ni Waziri wa mambo ya nje kwa rais George W. Bush. Ripoti nyingine ilifuata ikisema kwamba makao makuu ya jeshi yalikuwa yameshambuliwa, na kulikuwa na ripoti na uvumi usioaminika kwamba kulikuwa na ndege nyingine zikiruka kila mahali. Powell alianza kuandika notisi kwa ajili ya matumizi yake, aliandika hivi, “Watu wangu watakuwa na majukumu gani”? Je, ulimwengu na Marekani zitajibu vipi tukio hili? Je, hali itakuwa vipi kwa Umoja wa Mataifa? Je, Umoja wa kujihami wa NATO? Je, nitaanzaje kuwaita watu mbali mbali wakusanyike? Masaa saba kutowasiliana na mtu yeyote yalionekana kama miaka isiyohesabika kwa mtu huyo ambaye angekuwa mkuu wa majeshi.


Mnamo 1995, miaka miwili Powell akiwa amestaafu kutoka jeshini, alikuwa amefikiria kugombea urais. Aliandika kitabu cha simulizi ya maisha yake kiitwacho My America Journey (Safari yangu ya Amerika) ambacho kilishika nafasi ya kwanza kitaifa katika idara ya mauzo. Alikuwa amejichimbia katika siasa za Marekani akiwa katika kiwango cha makadirio ya juu kiumaarufu ambacho uteuzi wa chama cha Repblican ulikuwa ni wa kutaka aseme tu, na urais alikuwa karibu sana kuufikia. Armitage alikuwa amekipinga kitu hicho kwa nguvu “hapana haja. “Achana nacho” alimshauri rafiki yake huyo, “sidhani kama uko tayari kwa kitu kama hicho”. Shughuli ya kuendesha kampeni ni jambo ambalo Powell alikuwa halipendi, “inajumuisha kila kitu kibaya unachoweza kukifikiria.” Powell alikuwa anapenda mipango iliyotayarishwa vyema utaratibu mwema wenye kuweza kutabirika, na kiwango cha uhakika jambo ambalo halikuwa ni sehemu ya siasa za haraka haraka za Marekani.

Ilikuwa inafahamika wazi kwamba mkewe, Alma, alikuwa hapendi jaribio hilo kugombea nafasi hizo. Kilichokuwa siri ni kwamba Alma alikuwa amemwambia wazi kwamba iwapo angegombea urais angemwacha. “Ukigombea tu naondoka”, alisema. Alma alikuwa anaogopa kwamba (mumewe) angeshambuliwa au kupingwa risasi. Mumewe kugombea urais, “akishinda” na yeye kuwa mke wa rais ni mambo ambayo mwanamke huyo alikuwa hayataki maishani mwake . “Itabidi uyafanye mambo hayo peke yako,” alisema. Baada ya Bush kushinda uteuzi wa kugombea urais wa chama cha Repblican mwaka 2000, Powell alisaini makubaliano ya kutoa msaada, lakini Karl Rove aligundua kwamba kampeni hiyo ilikuwa ifanye juu chini kumwezesha aonekane katika tukio lolote sambamba na Bush. Karibu wafuasi wote muhimu wa Repblican walikubaliana kwamba chaguo la kugombea urais siyo Powell. Watu wake walitaka kufahamu ni nani mwingine ambaye angekuwepo kwenye tukio muhimu la chama hicho, kitu gani kingesemwa, nani wangehudhuria, na lengo la kisiasa lilikuwa nini. Yote haya yalikuwa yamepangwa kuelekeza mgawanyiko dhidi ya Powell na si Bush.

Isitoshe ni nyenzo za kumweka Bush katika siasa za mlengo wa kati na baadaye akawa ndiye chaguo kuu la kuwa waziri wa mambo ya nje iwapo Bush angechaguliwa kuwa rais. Katika sura ya nchi zaidi kulikuwa na hisia kubwa kuwa walifahamu kuwa walikuwa wanachagua timu si Bush na makamu mgombea mwenza wake, Waziri wa ulinzi wa zamani Dick Cheney, pia Powell. Wakati mahakama kuu ilipomtangaza Bush kuwa mshindi kwa kura 537 katika mkanganyiko wa uchaguzi huko Florida washauri wa Powell walikuwa na imani kwamba bosi wao alikuwa amesaidia kwa kiwango kikubwa sana katika ushindi huo. Katika miezi yake ya kwanza akiwa waziri wa mambo ya nje Powell alikuwa hajaliziba pengo la uhusiano wake na Bush ambalo halikuwafanya wawe karibu zaidi kama alivyokuwa na uhusiano wa karibu na watu wengine.

Kulikuwa na pengo kati ya watu hao wenye kuunganishwa na maelewano ya kirafiki. Bush na Powell walikuwa wanataniana wakiwa na watu wengine lakini walifanya hivyo mara chache sana wakiwa wawili. Rove alihisi kwamba Powell alikuwa anajidukiza mno kisiasa na kuendesha shughuli zake nje ya cheo chake. “Lazima ufahamu siku zote kwamba vyote hivi ni siasa na mimi ndiye nitaushinda mchezo huu wa kisiasa,” Rove alimwambia kwa faragha Powell. Kila mara Powell alipokuwa katika mandhari ya mbele kuhusiana na suala fulani na kuonekana kuwa ndiyo sura ya utawala, shughuli za kisiasa na mawasiliano huko Ikulu zilihakikisha zina mweka pembeni mwa mandhari na mwanga wa kisiasa. Rove na Karen P. Hughes mkurugenzi wa muda mrefu wa mawasiliano wa Bush ambaye wakati huo alikuwa ni mshauri Ikulu waliamua nani miongoni mwa viongozi angetokea katika kipindi cha mazungumzo cha jumapili kipindi maarufu cha televisheni kuhusu habari za jioni na asubuhi. Iwapo Ikulu isingetoa taarifa kupendekeza kwamba akubali mwaliko wa kutokea kwenye kipindi hicho Powell alikuwa anafahamu utaratibu mzima. Aliwaambia watayarishaji wa kipindi hicho.

Mnamo Aprili 2001 wakati ndege moja ya ujasusi wa kijeshi ya Marekani aina ya EP-3E ilipokingamwa na ndege za kivita katika pwani ya China, ikalazimishwa na serikali ya China kutua na kukamatwa mateka wote 24 waliokuwa katika ndege hiyo. Ikulu ilikuwa imedhamiria kuona kwamba Bush hajihusishi na suala hilo ili rais huyo asionekane kuwa mzungumzaji katika mgogoro huo. Ilikuwa ni kama vile hapakuwepo na mgogoro wa mateka, hii ilikuwa ni kwa kutia maanani jinsi mgogoro wa mateka huko Iran ulivyomdhoofisha Rais Carter na jinsi mgogoro wa mateka huko Lebanon ulivyokuja kumwathiri Rais Reagan katikati ya miaka ya 1980. Suala hilo lilipelekwa kwa Powell ambaye alifanikisha kuachiliwa kwa mateka hao baada ya siku 11. Ulikuwa ni ushindi mkubwa lakini hata hivyo, Ikulu haikutaka atokee kwenye televisheni kupata sifa alizostahili.

Powell na Armitage walikuwa wanataniana na kusema kwamba Powell alikuwa amewekwa katika kisanduku cha barafu au kwenye friji ambapo alikuwa anatumiwa tu wakati akitakiwa. Muda mfupi kabla ya mashambulizi ya September 11, jarida la times lilikuwa limeandika habari moja kuu kuhusiana na Powell ikiwa na kichwa cha habari “Umekwenda wapi Colin Powell”? Habari hiyo ilisema kwamba alikuwa akiacha nyoyo zikiwa kwenye kina kirefu kuhusiana na sera mbali mbali na kuonekana kuwa amemezwa na watu wenye msimamo mkali katika utawala uliokuwa madarakani. Habari hiyo ilitoa changamoto kubwa kwa Ikulu ambako maofisa kadhaa walikuwa wamewashikilia waandishi kuthibitisha kwamba Powell alikuwa akifanya kazi kama kawaida wakati mwingine akiwa amekata tama. Mara nyingi akifanya kazi kwa upweke akiwa amejikita pembeni na utawala huo mpya. Rove akiwa miongoni mwa maofisa hao alikuwa akisema chini chini kwamba alikuwa anahisi Powell alikuwa ameteleza sehemu fulani na kwamba ilikuwa si kawaida kumwona akiwa katika hali isiyoonyesha furaha akiwa na Rais.


TUNAINGIA VITANI.

Powell na watu wengine miongoni mwa washiriki wake walikuwa wametumia masaa mengi na waandishi wa jarida la Times wakijaribu bila mafanikio kuwajulisha kwamba habari waliyoandika haikuwa ya kweli. Lakini Powell na Armitage walifahamu nguvu iliyokuwepo Washington ambako kuibuka na kuanguka kwa umaafuru wa mtu ni jambo jepesi. Tatizo lilikuwa kwamba msimamo huo wa habari hiyo ungeonekana kuwa ndiyo ukweli hata kama haikuwa hivyo. Tatizo kubwa zaidi lilikuwa kwamba habari hiyo kwa sehemu fulani ilikuwa ni kweli. Powell alikuwa haanzishi sera mpya ya nchi za nje alikuwa akipangiwa majukumu ya kufanya na alikuwa akikabili migogoro midogo mmoja bada ya mwingine.

Lakini kama alivyowahi kusema mara moja katika faragha, “ili kuweza kuendelea bila matatizo katika ngazi za juu lazima uwe mjanja katika mchezo wako.” Alipokuwa mwenyekiti wa jopo la Wakuu katika jeshi aliwahi kuandika baadhi ya misemo aliyokuwa anaipenda zaidi na kuipenyeza chini ya kioo kilichokuwa juu ya deski lake katika makao makuu ya Wizara ya Ulinzi. Moja ya misemo hiyo ilikuwa “kamwe usiwaruhusu wakwambie kwamba unatapa tapa”. Rais Bush alikuwa akiwahutubia wanafunzi katika shule ya Emma E. Booker Elementary School huko Sarasota Florida wakati Rove alipomjulisha kwamba ndege moja ilikuwa imeubamiza Mnara wa Kaskazini wa kituo cha biashara cha kimataifa mwanzoni ilionekana kuwa tukio hilo lilikuwa ajali au labda kosa la rubani ambaye huenda alikuwa na mshitulo wa moyo, Bush alifikiri. Alikuwa amekaa kwenye stulu darasani akiwa amevaa suti yenye rangi nyeusi shati la bluu na tai nyekundu, Ubao mdogo wa ukutani uliokuwa nyuma yake ulikuwa na maandishi yasemayo “ Kusoma kunaifanya nchi istawi”.! Andrew H. Card Jr mnadhimu wa Bush na msaidizi wa zamani wa Reagan na Bush mkubwa aliingia na kumnong’oneza rais huyo moja kwa moja sikioni mwake “ndege ya pili imeubamiza mnara wa pili, Marekani inashambuliwa”. Picha ya hali iliyotokea wakati huo imebakia katika historia, mikono ya rais huyo ilikuwa imekunjwa juu ya miguu yake wakati anageuka kusikiliza maneno ya Card.

Uso wake ukawa na sura tulivu kwa mbali japokuwa kulikuwa na mshituko pamoja na kuchanganyikiwa. Bush anakumbuka vizuri kabisa alivyokuwa, ‘nafikiri watu hawa wametangaza vita dhidi yetu, na nimeamua wakati huu kwamba tunaingia vitani.” Alisema Bush. Bush aliamua kwamba alihitaji kuwaeleza wananchi wake mambo kadhaa. Saa 3.30 asubuhi alitokea mbele ya kamera za televisheni katika kituo cha habari cha shule hiyo ya Booker ili kutoa taarifa yenyewe. “kwa nini niliyarudia maneno hayo hayo labda huo ulikuwa ni mwangwi wa matukio ya nyuma” rais huyu alisema baadaye. “Sifahamu ni kwa nini nitakueleza ukweli kwamba hatukukaa kuyapanga maneno haya. Nilisimama na kujikuta nikiyasema. “Mlichokiona ndiyo hasa mimi mwenyewe nimeonyesha hulka yangu.”

Msururu wa magari ya rais huyo kwa kasi ulielekea kiwanja cha ndege cha kimataifa cha Sarasota Bradenton. Alichepuka haraka akipanda ngazi na kuingia katika chumba cha ofisi yake ya faragha ya ndege yake ya serikali ya Air Force One. “hakikisheni mke wangu na mabinti zangu wanalindwa” hiyo ndiyo ilikuwa amri yake ya kwanza kwa maofisa wa vyombo vya upelelezi. “Bwana Rais alisema mmoja wa maofisa hao kwa unyonge, “tunataka ukae haraka iwezekanavyo.” Bush alikaa kitini na kujifunga mikanda na ndege ikaanza kuondoka taratibu na muda si mrefu ikapaa angani kwa kasi. Mke wa Rais huyo Laura Bush akiwa amevaa suti nyekundu na mikufu miwili ya mapambo ya lulu shingoni mwake alikuwa katika chumba cha Caucus katika jengo la Ofisi ya Seneti la Russe mjini Washingtoni akiwa tayari kutoa hoja kuhusu watoto kuanza elimu mapema mbele ya kamati ya Seneta Robert M. Kennedy mara wakapata habari kuhusu ajali hiyo na bibi Bush, Seneta Kennedy na watu wengine wakaondoka kupitia mlango wa pembeni.

Baada ya maelekezo ya tukio hilo Bibi Bush alifanya juu chini kujituliza. Uso wake ulipauka mara moja machozi yakimlenga na midomo yake ikitetemeka kwa woga. Kisha makao makuu ya jeshi la Marekani yakashambuliwa, na wapelelezi na polisi wa kamzingira. Walimweleza nia ya kumpeleka katika eneo lenye usalama. Kundi hilo mara moja likaondoka haraka. Saa 3.50 Bibi Bush alikuwa akisubiri watu wa kumsindikiza katika msongamano wa magari kutoka jengo la bunge la Seneti (Capito), ilichukua dadika 45 kumfikisha kwenye makao makuu yake na alipelekwa katika chumba cha Mikutano cha Wood. Saa 4.51 ndipo vyombo vya usalama vilipoamua Kend kumficha katika Ofisi ya New Havana mtu mmoja aliyejuliakana kwa jina la Turquoise ambalo lilikuwa jina la siri la Barbar Bush Bint wa rais huyo aliyekuwa na umri wa miaka 19 akisoma huko . Twinkle jina jingine la siri la binti mwingine pacha wa Rais Bush. Akiwa anasoma Chuo kikuu cha Texas huko Austtin alipelekwa kufichwa katika Hotel ya Driskill dakika sita baadaye. Ilikuwa saa 3.39 asubuhi ambapo ndege ya America Air lines Safari namba 77 aina ya Boeing 757 ilipobamizwa katika jengo la makao makuu ya jeshi la Marekani. Dakika tano baadaye aliweza kuwasiliana kwa simu na makamu wake wa rais Dick Cheney ambaye alikuwa amekimbizwa kutoka katika ofisi yake ya upande wa magharibi na maofisa wa usalama na kupelekwa katika kituo cha shughuli za Dharura cha Rais (Presidential Operations Center - POC) ambacho ni handaki maalum la dharura lililo chini ya viwanja vya Ikulu.

LAZIMA TUWAOKOE WATU WETU,


“Uko sahihi kabisa” Tenet hatimaye alimwambia Black nafikiri sheria zote zimebadilika asubuhi hii. Maelfu ya watu walikuwa tayari wamekufa katika jiji la New York na makao maku ya jeshi (Pentagon). Black aliona kulikuwa kuna badiliko muhimu. Watu, akiwemo mkurugenzi wake, walikuwa wakipata wimbi la busara mbele ya macho yake katika muda mfupi sana wakijitoa katika kanuni za urasimu na kukubali matukio yaliyokuwa yamejaa hatari, hata kifo. Black hakushangaa sana na shambulio hilo lakini alishituliwa na kiwango cha mauaji hayo. Katika nafasi yake ya miaka mitatu akiwa mkuu wa idara ya kupiga vita ugaidi alikuwa amefikia imani kwamba iwapo mkuu wa CTC hakuwa mwenye msimamo mkali zaidi ya wakuu wake bali kazi hiyo ilikuwa haimfai. Alikuwa ameendesha harakati dhidi ya Al Qaeda alipokuwa mkuu wa kituo mjini Khartoum Sudan, alikuwa na lengo la shambulio la kushitukiza na jaribio la kumuua la mwaka 1994.

Alikuwa amepanga mipango kadhaa ya siri na ya nguvu na ya mauaji ili kumpata Bin Laden, lakini ilikuwa imekataliwa. Alifikiri na kuona kwamba kutokana na mazingira, hali hiyo ilikuwa ni lazima iwe hivyo. Hivi sasa yote hayo yaliku wa yamebadilika. Tenet alitoa amri ya watu wote kuondoka katika jengo hilo,isipokuwa wale tu waliokuwa katika idara ya GRC. Kwenye saa 3.50 asubuhi, Tenet alikuwa katika ofisi yake iliyokuwa katika ghorofa ya saba. ndege mbili za abiria tayari zilikuwa zimebamizwa kwenye minara yote miwili ya jengo la kituo cha Biashara cha kimataifa (World Trade Center) na ya tatu ikabamizwa kwenye makao makuu ya jeshi la Marekani (Pentagon) ndege ya nne iliyokuwa imetekwa ilikuwa katika anga la jimbo la Pennsylvania ikiwa moja kwa moja inaelekea eneo la Washington. Ripoti mbali mbali zilikuwa zimeenea katika mizunguko ya kijasusi kwamba malengo ya siku za baadaye yalikuwa ni pamoja na Ikuli, Bunge, Wizara ya mambo ya nje, Makao makuu ya CIA, eneo linaloonekana vyema na kufahamika karibu na mto Potomac lilikuwa moja wapo ya malengo dhahiri.

Wachunguzi walifahamu kwamba Ramzi Yousef gaidi wa kundi la Al Qaeda aliyeendesha shambulio la kwanza kwenye kituo hicho mwaka 1993 alikuwa na mipango ya kurusha ndege iliyokuwa imejaa mabomu na kuibamiza kwenye majengo ya CIA. “Ni lazima tuwaokoe watu wetu”, Tenet aliwaambia viongozi wake wa ngazi za juu. “Ni lazima tuwahamishe watu.” Alitaka kila mtu aondoke sehemu hiyo hata mamia ya wafanyakazi kutoka katika kituo cha kupiga vita Ugaidi (CTC) kilichokuwa katika sehemu ya chini ya jengo hilo ambako hapakuwa na madirisha. Cofer Black, mkuu wa CTC, aliiona amri yake hiyo kuwa haikuwa na msingi, na alifanya hivyo akikaribia kutingisha kichwa chake. Akiwa na umri wa miaka 52, Black alikuwa mkongwe wa kuendesha shughuli za siri na mmoja wa wafanyakazi hodari wa shirika hilo, Alikuwa amesaidia katika kukamatwa kwa gaidi wa kimataifa (Carlos) the Jackal ambaye labda alikuwa ndiye gaidi mwenye sifa mbaya zaidi duniani kabla ya Bin laden. Black alikuwa na nywele ambazo zilikuwa zinazidi kupungua na alikuwa akivaa mawani makubwa alikuwa anafanana sana na Karl Rove, mpangamikakati mkuu wa kisiasa wa Rais Bush. Alikuwa ni mtu mashuhuri sana wakati shirika hilo lilipokuwa na watu wenye mvuto na wale wa ajabu. Wakati karibu kila mmoja katika CIA alimwita Black nidhamu ya kizamani ya shuleni, ambapo alikuwa anapenda kuita “Bw. Mkurugenzi” au “Bwana” “Bwana,” Black alisema itabidi CTC tuwaache katika mpango huo kwa vile tunataka watu wetu wafanye kazi kwenye kompyuta.” alisema “je, watu wa kituo cha kupokelea majina Duniani (Global Response Center) Alikuwa akimaanisha watu wanane waliokuwa katika sehemu ya uchunguzi katika ghorofa ya sita karibu sehem wakipokea na kufuatilia habari mpya za ujasusi kuhusu ugaidi duniani kote “watakuwa katika mazingira ya hatari.” waendelee kukaa sehemu hiyo kutoka sehemu hiyo ,” Tenet alisisitiza .“Hapana, bwana ni lazima tuwaache pale kwani wana kazi muhimu ya kufanya katika mgogoro kama huu.

Ndio maana tuna kituo cha GRC.” lazima wafe.”Tenet alikaa kimya. Mkurugenzi huyo wa CIA alikuwa ni kama baba mlinzi wa maelfu ya watu waliokuwa wakifanya kazi hapo. Katika imani ya watu wengine kwa watu wengi mjini Washington, CIA ilikuwa taasisi iliyomegeka n maneno ya wazi zaidi ilikuwa ni chombo ambacho kilikuwa kinakaribia kutoweka. George Tenet mkurugenzi wa CIA (kulia) akiwa sambamba na G. Bush na Condolezza Rice katikati Mwaka 2002 Black alikuwa na nywele ambazo zilikuwa zinazidi kupungua na alikuwa akivaa alikuwa anafanana sana na Karl Rove, mpangamikakati mkuu wa kisiasa wa Rais Bush. Alikuwa ni mtu mashuhuri sana wakati shirika hilo lilipokuwa na watu wenye mvuto na wale wa ajabu.

Wakati karibu kila mmoja katika CIA alimwita Black kwa jina lake hilo la kwanza, Black alikuwa na nidhamu ya kizamani ya shuleni, ambapo alikuwa anapenda kuita “Bw. Mkurugenzi” au “Bwana” “Bwana,” Black alisema itabidi CTC tuwaache katika mpango huo kwa vile wafanye kazi kwenye kompyuta.” “Ndiyo, lakini”, Tenet alisema “je, watu wa kituo cha kupokelea majina Duniani (Global Response Center) Alikuwa akimaanisha watu wanane waliokuwa katika sehemu ya uchunguzi katika ghorofa ya sita karibu sehemu ya juu ya jengo hilo, ambao walikuwa wakipokea na kufuatilia habari mpya za ujasusi kuhusu ugaidi duniani kote “watakuwa katika mazingira ya hatari.” “Hilo ndio suala lenyewe itabidi kukaa sehemu hiyo.” “Sawa, lakini ni lazima tuwaondoe watu hao hiyo ,” Tenet alisisitiza .“Hapana, bwana ni lazima tuwaache pale kwani wana kazi muhimu ya kufanya katika mgogoro kama huu.

Ndio maana tuna kituo cha GRC.” “Wanaweza kufa.” “Mheshimiwa kama ni lazima wafe.”Tenet alikaa kimya. Mkurugenzi huyo wa CIA alikuwa ni kama baba mlinzi wa maelfu ya watu waliokuwa wakifanya kazi hapo. Katika imani ya watu wengine kwa watu wengi mjini Washington, CIA ilikuwa taasisi iliyomegeka na isiyokuwa ya lazima kwa maneno ya wazi zaidi ilikuwa ni chombo ambacho kilikuwa kinakaribia kutoweka.
 
H
Juzi kuna mtu kaongea kiswahili katikati ya wageni , kaonekana anakienzi , leo umeandikiwa kiswahili hichohicho na Yericko hutaki !
Ahahaa mkuu hawa ndio waswahili, yupo mwingine alikuja akaseme nimekopi kwake habari za dp cooper
 
FB_IMG_1535209536475.jpg
 
Back
Top Bottom