Taaluma ya Ualimu, isiwe sekta ya kufanyia mzaha.

G.MWAKASEGE

Senior Member
Jun 29, 2007
153
15
Ikunda Erick
HabariLeo; Wednesday,October 10, 2007 @00:01

Hakuna asiyejua umuhimu wa elimu, na ili kuwa na maisha bora yenye mwelekeo ni lazima uwe umepitia ngazi mbalimbali za elimu ambazo zitakuwa zimejengwa na misingi imara ya shule za msingi na sekondari, chini ya uongozi thabiti wa walimu wenye taaluma na wito wa kufundusha na sio wale wanaoangalia bora ajira.Kwa mtazamo wangu, naamini kuwa walimu bora wenye wito na nia ya kufundisha, matokeo yake huonekana mapema na hata wanafunzi wenyewe hufurahia masoma ya walimu kama hao, lakini ikiwa wapo walimu walioingia katika fani hiyo kwa kuwa wamekosa fani nyingine za kusomea ni wazi kuwa taaluma hiyo itawashinda.Hali hiyo hivi sasa inaonekana ambapo baadhi ya wanavyuo kwa kuhofia kukosa nafasi ya kuchaguliwa kujiunga na vyuo mbalimbali vya elimu ya juu, huchagua fani ya ualimu ili kupata nafasi lakini mara waingiapo chuoni wengi wao hufanya jitihada za hali ya juu kubadilisha na kuingia kwenye fani nyingine kama vile sheria, uchumi, Biashara na elimu ya Jamii na Mazingira.Lakini wapo wanaoshindwa kufanya hivyo, na huendelea kusoma ualimu na mara wamalizapo na kupangiwa shule za kufundisha, matokeo yake huanza kuonekana mapema ambapo moja ya mapungufu yao ni pamoja na kushindwa kufundisha ipasavyo hivyo wanafunzi kushindwa kwenye mitihani yao na wakati mwingine, walimu huacha kazi hiyo na kujiunga na shughuli nyingine .Ni wazi kuwa kazi ya ualimu inabaki kuwa ni kazi ya wito kama ilivyo kazi ya udaktari, wauguzi na nyingine na kuwa walimu wenye wito kwa kawaida hufundisha vizuri pamoja na kuwa mazingira ya kazi huwa magumu, lakini nia na kazi yake inabaki palepale, na mifano mizuri ni walimu waliofundisha kwa zaidi ya miaka 30, sasa bado wanaipenda kazi yao, na wengine wamekuwa kivutio kwa watoto nao kuwa na hamu ya kuwa walimu.Hali hiyo ya watu kuingia kwenye fani hiyo kwa wingi imekuja baada ya serikali kutangaza kuongeza nafasi za masomo na ufadhili wa wanafunzi wanaosoma ualimu, ambapo pia mishahara yao imeongezeka na ajira ya uhakika kuwepo, hivyo kwa kohofia kukosa ajira kwenye fani nyingine wengi wamekimbilia fani hiyo, kwa ajili ya kupata maslahi lakini sii wito wao.Chakufurahisha zaidi ni kwamba hata ,Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Margaret Sitta ameliona hilo na kuwaonya walimu wanaojiunga na fani hiyo kwa kufuata maslahi badala ya kazi wajiondoe wenyewe kwenye fani hiyo ili kuepuka kuichafua kwa kujinufaisha badala ya kufundisha kama wafanyavyo walimu wenye wito wa kazi hiyo.Kwa kauli hiyo hata mimi namuunga mkono Waziri Sitta, kwa sababu kama hatua za haraka hazitachukuliwa dhidi wa watu kama hao ambao tunaweza kuwaita wavamizi na wachafuzi wa taaluma yenye hadhi kubwa, ni wazi kuwa kizazi kijacho kitakuwa ni Taifa la watu mbumbumbu wasioweza kujiamini kwa hoja zao au wenye elimu duni na huo Ushirikiano wa Afrika Mashariki unaopiga hodi hatutaweza kushindana na wenzetu.Ni wazi kuwa hatua kali zikichukuliwa za kuwabaini wavamizi kama hao na kuwaondoa kwenye fani hiyo kwani wakiachwa ni hatari kwa ustawi wa elimu nchini kwa sababu badala ya kukuza watididimiza kwa njia mbalimbali kama vile kuwasulubu wanafunzi hata kwa makosa madogo yanayohitaji kuonywa au kuelekezwa kwa ukarimu na wapo wenye kuvunja maadili ya fani hiyo ambapo hufikia hatua ya kuwabaka wanafunzi wao, badala ya wao kuwa mfano wa kuwafundisha maadili mema.
 
Wait a minute...!! This thread was started in 2007..!!!!???
 
Back
Top Bottom