Syndicate: Mahakama, serikali, CCM | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Syndicate: Mahakama, serikali, CCM

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mundali, Feb 21, 2012.

 1. Mundali

  Mundali JF-Expert Member

  #1
  Feb 21, 2012
  Joined: Sep 16, 2010
  Messages: 749
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 35
  Wana JF salaam.
  Ninashangazwa sana na mwenendo mzima wa mahakama zetu hapa nchini. Baada ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2010, kesi nyingi za kupinga matokeo zilifunguliwa. Wagombea kupitia CHADEMA walifungua kesi nyingi tu mahakama kuu kupinga matokeo ya majimboni mwao.

  Lakini kinachonishangaza kesi hizo hazisikiki kabisa mwendelezo wake, lakini zile zilizofunguliwa na CCM, kama ile ya jimbo la Arusha mjini maelezo ya ushahidi wa upande wa mashtaka karibu utamalizika.

  Sasa je, kuna urafiki kati ya mahakama, serikali na CCM wenye muelekeo wa kutoa haki kwa upendeleo?
  Inakuwa vipi kesi ya kupinga matokeo ya jimbo la ukonga, ambalo mgombea ubunge kupitia CCM alikamatwa na masanduku ya kura yapatayo sita kwenye gari lake, kusuasua? Mahakama haina hela kwa kesi za CCM tu?
  Nawasilisha.
   
 2. Chali wa Moshi

  Chali wa Moshi JF-Expert Member

  #2
  Feb 21, 2012
  Joined: Feb 12, 2012
  Messages: 258
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  sheria yetu ya uchaguzi aijakaa vizuri kabisa
   
 3. t

  tenende JF-Expert Member

  #3
  Feb 21, 2012
  Joined: Jan 10, 2012
  Messages: 6,560
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Bila kelele haya yote yatawekwa kapuni. Ndiyo maana mie nasema 2015 hakuna kwenda mahakamani. Akichakachua mtu zaa naye!
   
 4. P

  PapoKwaPapo JF-Expert Member

  #4
  Feb 21, 2012
  Joined: Jun 5, 2008
  Messages: 380
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  napenda wote tuwe na moyo kama huu
   
 5. Calnde

  Calnde JF-Expert Member

  #5
  Feb 21, 2012
  Joined: Oct 7, 2008
  Messages: 1,373
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  bajeti hamna. Pesa ikipatikana tutaharakisha zile ambazo chadema wanapingwa. C unaona ya Arusha?
   
 6. O

  OPTIMUS TZ JF-Expert Member

  #6
  Feb 21, 2012
  Joined: Jan 30, 2012
  Messages: 391
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mzazi mahakama huna! huko kumwekwisha kabisa hao wanao endesha mahakama wajikomba serikalini waziwazi' .Sheria ya uchaguzi inasema kesi ifanyike ndani ya mwaka, wanajifanya hawana pesa mbona kesi nyingine zinaendelea ;kama kesi haiamishi mahakama huhitaji pesa kuendesha watumishi ni wale wale wako kituoni kwao;mbona kesi ya Zombe na Babu Seya zilizokuwa na mashaidi kibao zilifanyika;hii kusema hakuna hela ni uongo wa mchana watanzania tuamke maana nchi isiyokuwa na mahakama huru na zinazotenda haki amani haiwezi kudumu.
  Alipo ondoka Jaji Smata ndio kilikuwa kifo cha uhuru wa mahakama

  CDM inapaswa kuitisha maandamano kupinga uonevu huu wa wazi wazi take it form me Lema atapigwa chini Mzazi
   
 7. r

  rodrick alexander JF-Expert Member

  #7
  Feb 21, 2012
  Joined: Feb 12, 2012
  Messages: 4,112
  Likes Received: 1,499
  Trophy Points: 280
  leo jaji mkuu amesema pesa zimeshatoka na kesi zinatakiwa ziwe zimeisha mwezi wa tano sasa kigugumizi cha kunza kuzisikiliza ni nini jaji mkuu aache siasa afanye kazi yake yeye akilalamika na sisi wengine tufanyeje ndio maana walimtosa The Hague
   
Loading...