Sympathy for Wema Sepetu

Troll JF

JF-Expert Member
Feb 6, 2015
7,804
12,237
Wakuu nilikua nimepigwa ban hasa na watu wasionitakia Mema. (Mwanachama wa Chama Cha Mapinduzi).

Binafsi nimehudhunishwa na kitendo cha huyu binti kutuacha Chama Cha Mapinduzi (CCM) and the beauty Queen deserved some respect.

Wema Sepetu Mchango wake ulikua mkubwa sana kwenye kampeni za mwaka 2015. Wema Sepetu ndiye alikua anazunguka na Makamo wa Rais Bibi Samia Suluhu baada ya wanawake wengi kwenye chama kugawanyika baada ya kuamini kuwa huenda UKAWA wakachukua Nchi.

Ipo wazi wanajamii Forums kuna Viongozi wandamizi ndani ya chama kwa wakati kama Sophia Simba, Hawa Ghasia ni kama walikua wamemsusia yule mama zile kampeni amefanya kampeni zake kwa Upweke huku akiwa na Wema Sepetu hata Mimi nilikua nawasiwasi sana juu ya kumtumia Wema lakini alijitahidi Mwanzo hadi mwisho.

Hivyo CCM ilitakiwa kumjali Dada huyu hapa si maanishi kumpa Uongozi au Cheo la hasha hata kumlipa tuu pesa zake alizokua anadai Mimi binafsi nilishangaa kuwa alikua anakidai chama.

Wema ana mambo mengi lakini Yale ni personal life yake amekisaidia chama na pia mwanachama wa chadema naomba mumuoneshe ushirikiano nilishangaa wiki iliyopita kuna Mtu alileta thread kuwa Wema Sepetu hatajiunga CHADEMA mwanachama mmoja wa CHADEMA akacomment "Ana Msaada gani huyo break pumb.u?'" Nilihuzunishwa sana.

Mimi sitaondoka Chama Cha Mapinduzi ila namtakia kila laheri Wema Sepetu Chadema kama mkimpa Jimbo mwaka 2020 Na Umri wake utakua umesogea kidogo Nina uhakika anaweza kushinda Jimbo.

Namtakia mafanikio mema.
 
Wema anaweza kuingia bungeni kupitia ukawaa maana alikokuwa hakuna msanii maarufu kashinda jimbo tofauti na huku
Sugu
Prof jay
 
Hivi hii ishu ya madawa, imekuwaje ya ki CCM??
 
Huyu binti ataweza kweli kuvumilia dhahama za Upinzani? Maana kwa nchi zetu hizi za kiafrika hasa apa kwetu Upinzani unaonekana kama uadui dhidi ya sirikali. Anyway Muda utaongea
 
Interesting! Tangu hizi mada za bangi, Wema na Nyerere zikolee nimekuwa msomaji tu wa JF. Manake kwa watu kama sisi Tanzania ni zaidi ya uijuavyo! Sikutarajia ma"celebrity" hawa wa uswazi wanaweza kuwa na kilo ndefu hivyo kwenye siasa za bongo.

Inaelekea CCM ilipitia kipindi kigumu sana uchaguzi wa 2015 ikalazimika kuingia gharama kubwa kusajili kila aina ya nyenzo ili kumgonga Lowassa. Sasa nimeanza kuelewa kujaa kwa mada zinazotetea kila ujinga kwa kuhitimisha na obsession ya "almuradi Lowassa hakuiona Ikulu"! Yaani chama kilikuwa radhi kuzoa chochote kwa gharama yoyote kumzuia mtu mmoja asiingie Ikulu!

Kinachonishangaza sasa ni iweje chama kishindwe kuwalipa hela zao na kuwakamata kwa kuvuta bangi? Kwani wanadai hela ngapi hawa hadi tusikilizishwe porojo zao za kimtaa? Bora kuendelea kuwa msomaji tu.
 
Huo ndio ukweli

Halafu CCM sasa haina mwenyewe
 
Mjirekebishe mliokua mnamwita Break Pumb.u

Kama kuna mtu alimuita hivyo basi akili yake anaijua mwenyewe.Cha msingi Wema whether yuko CCM au CHADEMA bado anazo haki zake za msingi kama RAIA wa Tanzania,anzohaki za kupewa heshima zote hata kama ni msanii.Bado anazohaki za kutokupewa hukumu kwenye media hata kama alimkataa Mkuu wa Mkoa.

Na mwisho anayohaki kama mtanzania kulingana na sheria zetu kutetewa na wakili kwenye kesi zake.

Hongera bora umeona haki za Wema awepo CCM au upinzani bado anazo haki ya kuheshimiwa utu wake
 
Sasa atapewaje jimbo na wakati kesi yake ya kukutwa na bangi anapigwa mvua 30?
 
Namtakia maisha mema ndani ya cdm, ccm ya sasa haitaki ujanjaujanja, wala ngada wapika puli na wacheza vigodoro hawana nafasi, nilazima tujenge taifa lenye nidhamu.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom