Symbion Tanzania, TANESCO wabaruzwa kortini wakidaiwa bilioni 560

MsemajiUkweli

JF-Expert Member
Jul 5, 2012
13,171
23,996
KAMPUNI kutoka Falme za Kiarabu, Rental Solutions and Services LLC imeiburuza mahakamani kampuni ya kufua umeme ya Symbion Tanzania Limited na TANESCO, ikidai kulipwa Dola za Marekani 228,070,655.67 ambazo ni zaidi ya Sh bilioni 560 kama fidia na malipo ya ukodishaji wa mitambo ya kuzalishia umeme nchini.

Kesi hiyo Namba 234 ya mwaka 2016 imefunguliwa katika Mahakama Kuu Dar es Salaam mwishoni mwa wiki iliyopita. Mdaiwa wa pili katika shauri hilo ni Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco), ambalo limeunganishwa katika kesi hiyo kama mdau mkuu kwenye sakata hilo ambapo maamuzi yatakayotolewa na mahakama yanaweza kuiathiri.

Katika hati ya madai, Kampuni ya Rental Solutions and Services inadai Symbion Dola za Marekani 28,070,655.67 kama malimbikizo ya gharama za ukodishwaji wa mitambo, ambayo hadi sasa Symbion imeshindwa kulipa na pia katika shauri hilo Symbion itatakiwa kulipa Dola za Marekani milioni 200 ambazo ni fidia kwa kampuni hiyo kula hasara kutokana na Symbion kuvunja masharti ya mkataba na kuchelewesha au kushindwa kufanya malipo hayo.

Kwa mujibu wa hati hiyo ya madai, fedha hizo zinatokana na kazi zilizofanywa na kampuni hiyo ya Uarabuni ya kusambaza, kusimika na kuendesha mitambo ya kuzalisha umeme ambayo ilikodishwa na Symbion kwa matumizi ya miradi mbalimbali ya kuzalisha umeme kwa ajili ya Tanesco ili usambazwe kwenye Gridi ya Taifa kama ilivyokubaliwa kwenye mikataba.

Rental Solutions and Services pia katika kesi hiyo, inaiomba Mahakama kutamka kuwa kushindwa kwa Symbion kulipa gharama hizo za ukodishaji kama ilivyokubaliwa kwenye mkataba na pande zote mbili kumesababisha uvunjifu wa mkataba na hivyo sio halali na haistahili kuendelea.

Inadaiwa kuwa kati ya Septemba 2011 hadi Juni 2013, Rental Solutions and Services iliingia mikataba mbalimbali na Symbion ambapo pale ilipohitajika mikataba hiyo iliongezewa muda ili kukidhi mahitaji kwa mujibu wa mikataba hiyo kwa lengo la kusambaza na kusimika mitambo ya umeme ili kusambazwa kwenye Gridi ya Taifa.

Septemba 21, 2011 kampuni hiyo ya Uarabuni iliingia mkataba na Symbion kwa ajili ya kusambaza na kusimika mitambo ya umeme katika Kituo cha Zuzu cha Tanesco chenye nguvu ya kilovolti 33 kilichoko Dodoma yenye uwezo wa kuzalisha megawati 50.

Katika mitambo hiyo, pande husika zilikubaliana malipo ya Dola za Marekani 1,374,500 kwa mwezi kwa kipindi ambacho kingeishia miezi sita. Inadaiwa kuwa kwa kipindi hicho, Symbion ingepaswa kulipa jumla ya Dola za Marekani 8,247,000.

Hati ya mdai inaonesha kuwa mkataba kama huo uliingiwa na pande zote mbili Februari 12, 2012, kuhusu mitambo ya kuzalisha umeme wa megawati 55 kwa kipindi cha miezi 12 kwa gharama ya Dola za Marekani 1,666,000 kwa mwezi.

Mitambo hiyo ipo katika vituo vya Arusha na Dodoma. Kwa mujibu wa hati ya madai, kulikuwepo na ongezeko wa muda wa matumizi wa mitambo hiyo katika vituo vya Dodoma na Arusha ambapo Rental Solutions and Services ilitimiza matakwa yake kama ilivyo kwenye mikataba na iliwasilisha hati za malipo kwa Symbion ili kukamilisha malipo ya kukodi kitambo hiyo kama inavyotakiwa.

Pamoja na Rental Solutions and Services kutimiza masharti ya mikataba hiyo, kati ya Dola za Marekani 77,667,666.28, Symbion imelipa dola 49,597,010.61 tu. Hivyo, Rental Solutions and Services inadai kuwa hadi sasa, bila uhalali wowote, Symbion imeshindwa kutimiza masharti ya mkataba kwa kutolipa kiasi cha dola 28,070,655.67.

Chanzo:Habari Leo
 
Masuala kama haya ndiyo yaliyopelekea Rais Magufuli kusema mikataba kama hii haina manufaa kwa Tanzania kwa sababu inauweka uchumi wa Tanzania na usalama wa Taifa katika mikono ya wawekezaji kutoka nje ya nchi.

Hii mikataba iliingiwa huku viongozi waliokabidhiwa uhai wa Taifa wakiwa wanaangalia matumbo yao badala ya ustawi wa Watanzania.

Kwa sasa tunajikuta tunaunganishwa kama Taifa kwenye kesi ambazo hazina maslahi kwa taifa. Badala ya Mawakili wa Serikali kuweka nguvu zao kwenye masuala mengine ya kitaifa kwa sasa inawabidi nguvu zao waziweke kwenye kesi ambayo kama viongozi wetu wangeingia mkataba kwa kutanguliza maslahi ya Taifa wala tusingekumbana na kesi za aina hii.

Kinachofanyika ni sawa na msemo unaosema, wapiganapo fahali wawili ziumiazo ni nyasi.

Kumbe Symbion ni madalali tu wanaokopa mitambo nje halafu wanaleta na kuanza kutuuzia umeme kitu ambacho hata sisi kama taifa tungefanya na kupunguza gharama kwa mtumiaji wa umeme

Nchi kama Uingereza ambazo gesi au umeme huuzwa na makampuni ya nje lakini huwezi kukuta kuna kesi kama hizi za kijinga na kipumbavu kwa sababu viongozi waliokabidhiwa dhamana kitaifa walitanguliza maslahi yao katika kuingia mikataba na wawekezaji/wauzaji wa gas na umeme kwa wananchi.

Tusije kushangaa kama Kuna siku wauza umeme wote(wawekezaji) kwa TANESCO watafanya mgomo na kuzimisha mitambo yao mpaka madai yao yatimizwe!

Kweli Tanzania ni shamba la bibi!
 
Masuala kama haya ndiyo yaliyopelekea Rais Magufuli kusema mikataba kama hii haina manufaa kwa Tanzania kwa sababu inauweka uchumi wa Tanzania na usalama wa Taifa katika mikono ya wawekezaji kutoka nje ya nchi.

Hii mikataba iliingiwa huku viongozi waliokabidhiwa uhai wa Taifa wakiwa wanaangalia matumbo yao badala ya ustawi wa Watanzania.

Kwa sasa tunajikuta tunaunganishwa kama Taifa kwenye kesi ambazo hazina maslahi kwa taifa. Badala ya Mawakili wa Serikali kuweka nguvu zao kwenye masuala mengine ya kitaifa kwa sasa inawabidi nguvu zao waziweke kwenye kesi ambayo kama viongozi wetu wangeingia mkataba kwa kutanguliza maslahi ya Taifa wala tusingekumbana na kesi za aina hii.

Kinachofanyika ni sawa na msemo unaosema, wapiganapo fahali wawili ziumiazo ni nyasi.

Nchi kama Uingereza ambazo gesi au umeme huuzwa na makampuni ya nje lakini huwezi kukuta kuna kesi kama hizi za kijinga na kipumbavu kwa sababu viongozi waliokabidhiwa dhamana kitaifa walitanguliza maslahi yao katika kuingia mikataba na wawekezaji/wauzaji wa gas na umeme kwa wananchi.

Tusije kushangaa kama Kuna siku wauza umeme wote(wawekezaji) kwa TANESCO watafanya mgomo na kuzimisha mitambo yao mpaka madai yao yatimizwe!

Kweli Tanzania ni shamba la bibi!
Saa zingine tuwache kuwalaumu wawekezaji ni sisi wenyewe ndio wenye matatizo; hivi wewe una muuzia mtu bidhaa za millioni moja kila mwezi, uwezo wake wa kukulipa ni laki saba halafu hapo hapo anaenda kushusha bei za bidhaa na kujilipa ma bonus ya mabillioni baada ya kupewa sh billioni 70 za serikari huyu kweli ana nia ya kukulipa si ndio dharau zenyewe hizo.

Ukikataa kumuuzia bidhaa serikari inaingilia kati muuzie tutalipa sisi wakati wewe mwenyewe una wadeni wako ambao wanasubiri ulipwe na uwalipe.

Hivi serikari alioni kama management ya TANESCO ni tatizo kubwa sana binafsi bado sijapata majibu uwezo wa kibiashara wa TANESCO kushusha bei ulitokana na mchanganuo upi given their revenue streams and mrejesho wenye mabano kwenye vitabu vyao. Jamani embu tuwe wakweli wawekezaji sio wabaya hivyo mambo mengine tunayoyafanya yanawezekana nchini kwetu tu sio kwingine.
 
Kampuni kutoka Falme za Kiarabu, Rental Solutions and Services LLC imeiburuza mahakamani kampuni ya kufua umeme ya Symbion Tanzania Limited, ikidai kulipwa Dola za Marekani 228,070,655.67 ambazo ni zaidi ya Sh bilioni 560 kama fidia na malipo ya ukodishaji wa mitambo ya kuzalishia umeme nchini.

Kesi hiyo Namba 234 ya mwaka 2016 imefunguliwa katika Mahakama Kuu Dar es Salaam.

Mdaiwa wa pili katika shauri hilo ni Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco), ambalo limeunganishwa katika kesi hiyo kama mdau mkuu kwenye sakata hilo ambapo maamuzi yatakayotolewa na mahakama yanaweza kuiathiri.

Katika hati ya madai, Kampuni ya Rental Solutions and Services inadai Symbion Dola za Marekani 28,070,655.67 kama malimbikizo ya gharama za ukodishwaji wa mitambo, ambayo hadi sasa Symbion imeshindwa kulipa na pia katika shauri hilo Symbion itatakiwa kulipa Dola za Marekani milioni 200 ambazo ni fidia kwa kampuni hiyo kula hasara kutokana na Symbion kuvunja masharti ya mkataba na kuchelewesha au kushindwa kufanya malipo hayo.

Kwa mujibu wa hati hiyo ya madai, fedha hizo zinatokana na kazi zilizofanywa na kampuni hiyo ya Uarabuni ya kusambaza, kusimika na kuendesha mitambo ya kuzalisha umeme ambayo ilikodishwa na Symbion kwa matumizi ya miradi mbalimbali ya kuzalisha umeme kwa ajili ya Tanesco ili usambazwe kwenye Gridi ya Taifa kama ilivyokubaliwa kwenye mikataba.

Rental Solutions and Services pia katika kesi hiyo, inaiomba Mahakama kutamka kuwa kushindwa kwa Symbion kulipa gharama hizo za ukodishaji kama ilivyokubaliwa kwenye mkataba na pande zote mbili kumesababisha uvunjifu wa mkataba na hivyo sio halali na haistahili kuendelea.

Inadaiwa kuwa kati ya Septemba 2011 hadi Juni 2013, Rental Solutions and Services iliingia mikataba mbalimbali na Symbion ambapo pale ilipohitajika mikataba hiyo iliongezewa muda ili kukidhi mahitaji kwa mujibu wa mikataba hiyo kwa lengo la kusambaza na kusimika mitambo ya umeme ili kusambazwa kwenye Gridi ya Taifa.

Septemba 21, 2011 kampuni hiyo ya Uarabuni iliingia mkataba na Symbion kwa ajili ya kusambaza na kusimika mitambo ya umeme katika Kituo cha Zuzu cha Tanesco chenye nguvu ya kilovolti 33 kilichoko Dodoma yenye uwezo wa kuzalisha megawati 50.

Katika mitambo hiyo, pande husika zilikubaliana malipo ya Dola za Marekani 1,374,500 kwa mwezi kwa kipindi ambacho kingeishia miezi sita. Inadaiwa kuwa kwa kipindi hicho, Symbion ingepaswa kulipa jumla ya Dola za Marekani 8,247,000.

Hati ya mdai inaonesha kuwa mkataba kama huo uliingiwa na pande zote mbili Februari 12, 2012, kuhusu mitambo ya kuzalisha umeme wa megawati 55 kwa kipindi cha miezi 12 kwa gharama ya Dola za Marekani 1,666,000 kwa mwezi.

Mitambo hiyo ipo katika vituo vya Arusha na Dodoma. Kwa mujibu wa hati ya madai, kulikuwepo na ongezeko wa muda wa matumizi wa mitambo hiyo katika vituo vya Dodoma na Arusha ambapo Rental Solutions and Services ilitimiza matakwa yake kama ilivyo kwenye mikataba na iliwasilisha hati za malipo kwa Symbion ili kukamilisha malipo ya kukodi kitambo hiyo kama inavyotakiwa.

Pamoja na Rental Solutions and Services kutimiza masharti ya mikataba hiyo, kati ya Dola za Marekani 77,667,666.28, Symbion imelipa dola 49,597,010.61 tu. Hivyo, Rental Solutions and Services inadai kuwa hadi sasa, bila uhalali wowote, Symbion imeshindwa kutimiza masharti ya mkataba kwa kutolipa kiasi cha dola 28,070,655.67.
 
Huku naona ni nishati na madili. Halafu madini yawe sehemu ya mali asili. Yaani toka 1994 kwenye hii wizara na TANESCO wanajitahidi kweli kutandaza umeme lakini madili yao makali balaa. Wawadai wahusika waliokuwepo na si serikali hii.
 
Saa zingine tuwache kuwalaumu wawekezaji ni sisi wenyewe ndio wenye matatizo; hivi wewe una muuzia mtu bidhaa za millioni moja kila mwezi, uwezo wake wa kukulipa ni laki saba halafu hapo hapo anaenda kushusha bei za bidhaa na kujilipa ma bonus ya mabillioni baada ya kupewa sh billioni 70 za serikari huyu kweli ana nia ya kukulipa si ndio dharau zenyewe hizo.

Ukikataa kumuuzia bidhaa serikari inaingilia kati muuzie tutalipa sisi wakati wewe mwenyewe una wadeni wako ambao wanasubiri ulipwe na uwalipe.

Hivi serikari alioni kama management ya TANESCO ni tatizo kubwa sana binafsi bado sijapata majibu uwezo wa kibiashara wa TANESCO kushusha bei ulitokana na mchanganuo upi given their revenue streams and mrejesho wenye mabano kwenye vitabu vyao. Jamani embu tuwe wakweli wawekezaji sio wabaya hivyo mambo mengine tunayoyafanya yanawezekana nchini kwetu tu sio kwingine.
Matatizo ya TANESCO sio ya Management ya TANESCO ndugu, wanasiasa kuingiza siasa zao ndio chanzo cha matatizo ta TANESCO, pili mikataba mibovu kama hiyo ndio inaigharimu TANESCO.

Hapo swala la bonasi halihusiki hata kidogo sana zaidi wivu wa kike unakusumbua ambao ni ugonjwa mkubwa uliowaingia watanzania walio wengi.
 
Hiyo ndio Tanzania ukikosoa tu lazima una wivu wakati watu wanavurunda kila siku hesabu za kampuni zinaonyesha gearing ratio inayofikia 90%, kampuni budget yake over 70% ni donors funded + government top up (nchi nyngine hiyo ni serious risk to national security siku donors wakigoma unaweza aribu uchumi wako kwa sehemu kubwa sana), current liabilities zinazidi current capital assets at any time, balance mabano. Kigezo cha kushusha bei au kujilipa bonus kinatoka wapi?

Some of us do not even care anymore hila kwa mtindo huu Tanzania ya viwanda itakuwa ngumu imechukua Magufuli kuja kutoa hela za Kinyerezi II na bado autotimiza mahitaji ya nchi sasa hawa tena wenye michango yao tunataka kuwawekea mizwenge kuja kuongeza deficit kwenye grid ya taifa halafu unasingizia siasa; we ukiona mtu anapigiwa mizwenge Tanzania ujue ni mwiba Prof Muhongo ana nia njema ya ku-sort TANESCO labda mbinu zake ndio utata hila tatizo halisi ni management decision ata sijui zinaamuliwa vipi kwa ustawi wa kupatikana umeme wa uhakika in the long run hawa jamaa ni matatizo.
 
Masuala kama haya ndiyo yaliyopelekea Rais Magufuli kusema mikataba kama hii haina manufaa kwa Tanzania kwa sababu inauweka uchumi wa Tanzania na usalama wa Taifa katika mikono ya wawekezaji kutoka nje ya nchi.

Hii mikataba iliingiwa huku viongozi waliokabidhiwa uhai wa Taifa wakiwa wanaangalia matumbo yao badala ya ustawi wa Watanzania.

Kwa sasa tunajikuta tunaunganishwa kama Taifa kwenye kesi ambazo hazina maslahi kwa taifa. Badala ya Mawakili wa Serikali kuweka nguvu zao kwenye masuala mengine ya kitaifa kwa sasa inawabidi nguvu zao waziweke kwenye kesi ambayo kama viongozi wetu wangeingia mkataba kwa kutanguliza maslahi ya Taifa wala tusingekumbana na kesi za aina hii.

Kinachofanyika ni sawa na msemo unaosema, wapiganapo fahali wawili ziumiazo ni nyasi.

Nchi kama Uingereza ambazo gesi au umeme huuzwa na makampuni ya nje lakini huwezi kukuta kuna kesi kama hizi za kijinga na kipumbavu kwa sababu viongozi waliokabidhiwa dhamana kitaifa walitanguliza maslahi yao katika kuingia mikataba na wawekezaji/wauzaji wa gas na umeme kwa wananchi.

Tusije kushangaa kama Kuna siku wauza umeme wote(wawekezaji) kwa TANESCO watafanya mgomo na kuzimisha mitambo yao mpaka madai yao yatimizwe!

Kweli Tanzania ni shamba la bibi!
Mbona hatuoni TANESCO wanahusikaje? Huenda hawa watu wameitumia Tanesco ili kupata umakini wa watanzania.
Hii ni mikataba ya kibiashara wanajua waliposhindwana kwani kila mmoja alijua faida ataipataje.
Mbona kesi za kibiashara zipo nyingi tu mahakamani kwa nini hii.
 
Masuala kama haya ndiyo yaliyopelekea Rais Magufuli kusema mikataba kama hii haina manufaa kwa Tanzania kwa sababu inauweka uchumi wa Tanzania na usalama wa Taifa katika mikono ya wawekezaji kutoka nje ya nchi.

Hii mikataba iliingiwa huku viongozi waliokabidhiwa uhai wa Taifa wakiwa wanaangalia matumbo yao badala ya ustawi wa Watanzania.

Kwa sasa tunajikuta tunaunganishwa kama Taifa kwenye kesi ambazo hazina maslahi kwa taifa. Badala ya Mawakili wa Serikali kuweka nguvu zao kwenye masuala mengine ya kitaifa kwa sasa inawabidi nguvu zao waziweke kwenye kesi ambayo kama viongozi wetu wangeingia mkataba kwa kutanguliza maslahi ya Taifa wala tusingekumbana na kesi za aina hii.

Kinachofanyika ni sawa na msemo unaosema, wapiganapo fahali wawili ziumiazo ni nyasi.

Nchi kama Uingereza ambazo gesi au umeme huuzwa na makampuni ya nje lakini huwezi kukuta kuna kesi kama hizi za kijinga na kipumbavu kwa sababu viongozi waliokabidhiwa dhamana kitaifa walitanguliza maslahi yao katika kuingia mikataba na wawekezaji/wauzaji wa gas na umeme kwa wananchi.

Tusije kushangaa kama Kuna siku wauza umeme wote(wawekezaji) kwa TANESCO watafanya mgomo na kuzimisha mitambo yao mpaka madai yao yatimizwe!

Kweli Tanzania ni shamba la bibi!
Richmond aulizwe Lowassa-JM KIKWETE
 
Matatizo ya TANESCO sio ya Management ya TANESCO ndugu, wanasiasa kuingiza siasa zao ndio chanzo cha matatizo ta TANESCO, pili mikataba mibovu kama hiyo ndio inaigharimu TANESCO.

Hapo swala la bonasi halihusiki hata kidogo sana zaidi wivu wa kike unakusumbua ambao ni ugonjwa mkubwa uliowaingia watanzania walio wengi.

Wafanyakazi wa TANESCO mnalipana msichostahiri,maofisini kumejazana watu wasio na kazi,kazi ya kufanywa na mtu mmoja inafanywa na watu wanne hadi watano kutoa LPO's au Qoutations tu.
 
Sasa naanza kuamini kuwa mgao wa umeme Tanzania utabakia kuendelea kuwa historia
 
1.) Dollar milioni 28 inakuwaje shilling Billion 560?!
2.) TANESCO ilishindwa kwenda kwa huyo supplier moja kwa moja hadi wamtumie huyo dalali symbion?
3.) TANESCO haidaiwi chochote hapo, kwanini ameshtakiwa kwenye hiyo kesi? Mwishowe watz tukamuliwe service charge kulipa deni la symbion!
 
Bongo sanaa haziishi kumbe symbion hana mitambo nae anakodi kwa nini kama ni ivyo tusikodi wenyewe kwa hao jamaa au kununua Mitambo hata kwa kukopa kuriko huu Ujambazi unaofanyika kila siku huko Tanesco...

Mkuu uko sahihi.Kwa ufupi niseme hivi.Mwenyezi MUNGU awalaani wote walioingia hii mikataba ya kinyonyaji ya kukwapua hela za walipa kodi maskini wa Tanzania.Wafe kwa maradhi ya mateso ya muda mrefu mno wao na familia zao.Asiwepo atakayeishi bila kuumwa katika familia zao.Walaaniwe waamkapo na walalapo.Asiweko atakayeona raha ya maisha.Maisha yao yawe uchungu siku zote.
 
Hii nchi ina shida kama mnakumbuka symbion wanaidai TANESCO na wakati huo huo TANESCO wakashusha bei ya umeme; sasa inakuaje mtu una madeni kibao uku unashusha bei ya umeme?
 
Back
Top Bottom