wakuu wakazi mi ninaswali kidogo hivi kutofauti yoyote kati ya ipad na computer za kawaida
nafkiri unamaanisha tofauti ya ipad na hizi laptop na desktop.
ipad ni simu yenye screen kubwa. haitofautiani sana na simu jinsi inavyorun mambo kama kubrowse, inaingia application sawa na simu, kuangalia video na vyenginevyo.
computer unazosema wewe ni very powerfull tofauti na ipad, zina application ambazo zina nguvu kuliko za ipad na pia unaweza fanya mambo mengi sana kwa computer kuliko ipad.
mfano angalia hizi situation.
1. simu ikiharibika kama inaflashiwa au kuwekwa software mpya computer inatumika ila ipad haiwezi kuflash simu.
2. office kwenye computer ina mambo mengi na inakubali karibia printer zote ila kwenye ipad inataka printer zake tu na haina mambo mengi. (ninaposema office ni ms word, excel, powerpoint, publishe, access nk)
3. unaweza edit video, kutengeneza movie, kutengeneza animation za ukweli na computer ila ni ndoto kwa ipad.
kwa hio umeona hapa kuwa computer ina nguvu kuliko ipad.
reason ya computer kuwa na nguvu ni sababu ya operating system yake. osx au windows ndio zinafanya computer iwe na nguvu. operating system ya ipad yani ios haina nguvu kama za computer.
sasa hivi zipo pc za window za inch 8 tu. hivyo inawezekana computer ikawa ndogo lakini ikawa na power kuliko ipad ya inch 10