Swila na Bundi

Swila na Bundi

Hussein J Mahenga

JF-Expert Member
Joined
Mar 5, 2012
Posts
751
Reaction score
656
SWILA NA BUNDI.
Na.
Uncle Kaso
__________
Nakumbuka vizuri siku nikiwa porini, mara ya kwanza nilipokutana na swila, nikajikuta nipo kwenye mgongo wa ng'ombe pasi na kujua nimepandaje, na viatu vyangu vya matairi vikiwa vimejaa mkojo.

Mara ya pili, nilimuona mjomba akihangaika huku na huku kupambana na swila hadi jasho likimtoka. Mama yangu pia aliwahi kuniambia kuwa, swila ni nyoka mbaya sana. Kwanza ana jeuri. Hasikilizi kelele, ila hupambana na kelele mpaka mwisho.

Meno ya swila ni mfano wa sindano ya kudungia dawa, yenye mrija ambao hupitisha mate yenye sumu kali ambayo humsaidia katika mashambulizi yake na adui. Ukilinganisha na koboko, swila hana aibu wala kuogopa kiume, ila hukabiliana nacho mpaka dakika ya mwisho hata kama amezidiwa.

Mama yangu aliponiita siku moja SWILA kama utani, nilifurahi sana, kwani nilijipa ushujaa kuwa, mimi ni mwanaume nisiyeogopa kama swila. Mimi ni swila.

Nasema kweli ya Mungu kuwa mimi ni swila. Nakumbuka vizuri kabisa yule mgeni aliyekuja akadai kuwa eti biashara yangu na yeye ilikuwa ni kwa faida ya familia yangu. Nilisimama nikasema kwa kujiamini kabisa kuwa, "kama ufinyanzi huu hautakuwa na uhitaji na wafinyanzi, tuuache hivyohivyo". Mama yangu alisimama tena na kuniita kwa sauti kubwa, SWILA!. Siku hiyo nilijiamini kabisa kuwa mimi ni shujaa. Jina la Kaso halikuvuma tena na hata majirani zetu wakapendelea kuniita kwa jina la utani alilonipatia mama yangu.

Kijijini kwetu watu hupendelea sana biashara ya vyungu, kwani mara nyingi wengi wao husema kuwa, mtungi kwa mfano, hupoza maji vizuri zaidi kuliko hata jokofu. Kwa hiyo, vijana wengi tulijiajiri na uchimbaji wa mfinyanzi; shughuli ambayo hata baba yangu aliifanya mara nyingi.

Miaka kadhaa baadae, ule mfinyanzi ulipata thaman sana, hivyo kila mtu akaona kuwa, ni sahihi na inalipa zaidi kujiajiri katika uchimbaji wa mfinyanzi. Licha ya hilo, hata biashara yake pia, biashara ya vyungu ililipa sana hasa ukipeleka kwenye vijiji jirani. Hivyo, vijana wengi tuliokuwa rija moja tulijiajiri kwa shughuli hii.

Biashara hii haikuishia hapa tu. Ilikuna hadi vichwa vya uongozi wa kijiji ambapo wakaona ni bora waifanye kama sehemu ya mapato ya kijiji ambayo ingeweza kusaidia katika maendeleo ya kijiji.

Siku moja mwenyekiti wa kijiji alitembelea kijiji jirani kwa ajiri ya kujionea biashara hiyo. Akiwa huko, aliona biashara hiyo inalipa kila sehemu, lakini hawakuwa na pa kuchimba mfinyanzi huo, hivyo akadhani kuwa ilikuwa ni fursa nyingine kwa vijana wa kijiji chake kwamba, si tu wangejipatia mali kwa kuuza vyungu kule, bali pia wangefanya ushirika wa kuchimba mfinyanzi na kuuza kule. Kwa hiyo, kwa busara zake akaonelea kuwa, ingekuwa vizuri zaidi endapo angefanya ushirika wa kubadilishana hata wafinyanzi. Kiukweli kijiji kil!e kilikuwa kimeendelea kidogo, kwani kilikuwa na sululu nyingi, majembe mengi na mapanga ambayo yalikuwa mazuri kuchimbia kuliko ambayo tulikuwa tukiyatumia hapo awali.

Katika mazungumzo yake na mwenyekiti wa kijiji kile, kijiji cha Mogwa, Mzee Matola, mwenyekiti wetu aliamini kuwa ushirika ule ungekuwa na manufaa makubwa.

Mzee Uwezo, mwenyekiti wa kijiji hicho, alikuwa ni rika la Mzee Matola. Nywele zake zilikuwa kama katani iliyokunwa kwa ustadi mkubwa. Macho yake yalikuwa yamejaa janja nyingi. Mzee Uwezo alipendelea sana kuvaa saa ambayo hakumaliza hata dakika bila kutazama muda. Kwa upande mwingine, Mzee Matola alikuwa ni mzee ambaye hakupendelea sana kujishusha akiwa ugenini. Uso wake ulikuwa wa namna ya pekee ambao ukiuangalia mara moja tu inatosha kumjua Matola ni nani.

Wakati huo, mimi nilikuwa msagula wa karibu sana na Mzee Matola. Kwa hiyo hata safari hiyo nilikuwa naye.

Tukiwa kwenye kikao, nilisikia mzee Matola akisema kwa hasira, lakini nilipomwangalia usoni alikuwa na tabasamu.

"Kama mfinyanzi huoza, acha uozee chini. Sipo tayari kabisa kufanya biashara ya kuchumia tumbo". Yalikuwa ni maneno yake na wala sikujua ilikuwa ni nini chanzo.

Tulipotoka pale kijijini siku hiyo usiku, nikamuuliza mzee Matola, kwani shida ilikuw nini? "Yeye ana vijana wa kazi, ana vifaa vya kuchimbia mfinyanzi. Sasa anataka awe anachukua madebe nane kwenye kila madebe kumi yanayotoka shimoni. Siiwezi kabisa biashara hiyo".

Baada ya kifo cha mzee Matola, wapo waliolia kwa hisia kali wakidai kuwa hakika alikuwa mtu wa watu. Wengine wakasema kuwa, watafuata nyayo zake ili kumuenzi.

Yapata miaka thelathini iliyopita, waliosema wanataka kumuenzi Mzee Matola, walirudi kwenye kile kijiji na kukubaliana na Mzee Dunga, mwanaye mzee Uwezo juu ya biashata ya mabebe mawili katika kila madebe kumi yatokayo shimoni. Yaan, wakichimba debe kumi, kijiji chetu kinapata madebe mawili tu, nane yote yanakwenda kijiji cha Mogwa. Ndiyo, kwa nini unashangaa?

Biashara hii niliichukia sana. Hakika sikula nikashiba nilipoiwaza biashara ile. Cha ajabu sasa, mpaka vyungu vikawa vinachomewa Mogwa na kurudishwa kuuzwa Kalitu, kijijini kwetu. Kwa hiyo, wataalamu wote wa kufinyanga vyungu wakawa wanakia njaa. Niliapa ipo siku nitakuwa mwengekiti wa kijiji chetu, kijiji cha Kalitu.

Miaka ishirini baadae, Mungu amesaidia nimepata kuwa mwenyekiti wa kijiji hiki. Mama yangu ananiita SWILA. wanakijiji wote wananiita SWILA. Nilipoikataa biashara ile, jina la Swila lilichukua sura mpya.

Siku moja mama yangu akaniambia kuwa, "wakatu mwingine mate ya swila huwa hayafiki mbali. Mwanangu, watu wote humuogopa Swila, lakini Swika humuogoa zaidi bundi!".

Nilipokataza biashara ile, sikutaka kabisa kuonana na wajumbe wa Mzee Dunga; nilichokitaka ni mfinyanzi wetu urudi.

Masalale! Niliposhikilia mfinyanzi, nilisahau kuwa tulishauza vyungu vingi kule Mogwa na tayari vilikuwa vinaendelea kusafirishwa! Na biashara hii ilikuwa imeshapitishwa na rafiki yangu wa karibu sana, aliyewahi kuwa mwenyekiti wa kijiji pia, Mzee Marekana.

Wanakijiji walipotaka Mzee Marekana apigwe masumle, niliwaambia kuwa, mzee Marekana alifanya kazi kubwa mno. Wamuache aendeleze kilimo chake cha njugu salama.

Mimi ni Swila, hata mama yangu anajua. Ninao mpango wa kumtemea sumu kali bundi pale kwenye kiota chake. Nitahakikisha Mzee Dunga na marafikize hawachukui tena mfinyabzi wetu, ila vyungu wasafirishe tu. Nguvu ya swila, bundi haiwezi!

Uncle Kaso
 
Back
Top Bottom