Sweden hawana Serikali tangu tarehe 9 Sept,leo imeshindikana kupata Serikali.Wanabembelezana uchaguzi usirudiwe kukwepa gharama,Tanzania je?

britanicca

JF-Expert Member
May 20, 2015
15,636
30,004
Tanzania uchaguzi wa jimbo au kata unaacha majonzi. Wenzenu Sweden hawana serikali tangu tarehe 9 Sept, na leo imeshindikana kupata serikali. Vyama vinabembelezana kuungana ili vifikie column inahitajika ili vishikie dola.

Vyama vikuu ni vitatu: 1. Social demokraterna (ndilo kilichukua dola 2014), 2. Moderaterna (kilishindwa 2014), 3. Sverige demokratena (kimepanda sana na kushangaza ulimwengu, ila hakuna chama kinataka kushirikiana nao). Hivyo ndio vyama vyenye nguvu, pia kuna vingine lakini vilipata chini ya 10%. Point ni kuwa vikubaliane na kugawana viti.....

Lakini Tanzania inatumia bilioni 15.8 kurudia chaguzi lakini inakopa bilioni 46 kujenga mradi wa maji. Tujiulize; sisi Tanzania hatutakaa tuifikie Sweden kwenye suala la maendeleo, na wana uchumi mzuri sana kuliko sisi Tanzania. Swali: Wao wanaona ni mzigo kwa walipa kodi kama uchaguzi utarudiwa. Je, sisi Tanzania tunafikiria kutojifunza toka kwa wenzetu?
 
Tunakubwa la kujifunza hapo mkuu. Tumuombe Mungu sana Atupe ujasiri kudai Katiba na awabadilishe dhamira ccm wawe na fikira kujenga mifumo,mihimili na taasisi imara kuliko MTU kupitia Katiba Bora. Mfano sio siri hata ccm kama taasisi haina nguvu zaidi ya Mwenyekiti wake.
 
Wasweden ndio wanatakiwa kuja kujifunza kwetu sisi tulikataa vyama vingi kupunguza gharama za chaguzi Na figisufigisu kama hizo za vyama vingi wakatulazimisha lazima tuingie vyama vingi tukakubali shingo upande wakati asilimia 80 ya watanzania walikataa vyama vingi.Ona sasa wao wanaojitia vinara wa vyama vingi wamekwaa kisiki.Waje Tanzania watuombe CCM tuwafundishe namna ya kujikwamua kwenye huo mkwamo.
 
Wana lipi la kujifunza kwetu?
 
Uchaguzi Sweden na mataifa mengine yenye mfumo wa democrasia ya kweli huamuliwa na kura za wananchi. DUNIA ya tatu wananchi kura zao ni ushahidi, hazina nguvu.
Marekani Trump mbona walalamika kuwa aliiba kura kwa mtandao akishirikiana Na warusi? Wasweden wangekuwa Na Chama kimoja yasingewakuta
 
Wana lipi la kujifunza kwetu?
Sisi hatujawahi kwama Na kukosa Raisi kama wao baada ya uchaguzi.Kura zikipigwa tu Raisi huyo kapatikana hamna mkwamo watu wazima wanakwamaje? Waje CCM tuwafundishe ili hilo tatizo lisije jirudia miaka ijayo.Taifa dogo tunajua cha kufanya wao taifa kubwa hawajui aibu looo
 
Acha kujidharilisha, umeandika uharo gan hapa?
 
Tanzania uchaguzi wa jimbo au kata unaacha majonzi. Wenzenu Sweden hawana serikali tangu tarehe 9 Sept, na leo imeshindikana kupata serikali. Vyama vinabembelezana kuungana ili vifikie column inahitajika ili vishikie dola. Lakini Tanzania inatumia bilioni 15.8 kurudia chaguzi lakini inakopa bilioni 46 kujenga mradi wa maji. Tujiulize; sisi Tanzania hatutakaa tuifikie Sweden kwenye suala la maendeleo, na wana uchumi mzuri sana kuliko sisi Tanzania. Swali: Wao wanaona ni mzigo kwa walipa kodi kama uchaguzi utarudiwa. Je, sisi Tanzania tunafikiria kutojifunza toka kwa wenzetu?
Yaani chadema wabembelezwe kuunda serikali?,mmh!,huko ni kukosa akili
 
Sisi hatujawahi kwama Na kukosa Raisi kama wao baada ya uchaguzi.Kura zikipigwa tu Raisi huyo kapatikana hamna mkwamo watu wazima wanakwamaje? Waje CCM tuwafundishe ili hilo tatizo lisije jirudia miaka ijayo.Taifa dogo tunajua cha kufanya wao taifa kubwa hawajui aibu looo
Unatutafutia ban humu JF wewe.

Ufala mnaofanya kule bungeni, wabunge wenu kuwapa mikataba ya kijinga wawekezaji, tena kwa kutumia hati ya dharura (Certificate of Urgency) ili ipitishwe kwa haraka haraka, halafu wenyewe mnakuja kuongea kinafiki eti taifa linanyonywa na wawekezaji, nani amaewapa hio mikataba!!!

Saa ngapi mtajua machungu ya kupoteza hela za kodi kila kukicha kurudia uchanguzi? Halafu wa kwanza nyie kuanzisha account za rambi rambi maafa yakitokea.

Ni bora hizo hela za chaguzi za liwale na kata zile 37 nyingine mngepeleka rambi rambi Ukerewe tu, halafu wagombea wenu wapewe ushindi wa bila kupingwa.
 
Acha kujidharilisha, umeandika uharo gan hapa?
Wewe sio mpiga kura wa Sweden pambana Na hali yako Na Chadema wenzio ya kupigwa chini Na CCM Tanzania msitafute Ku steam out frustration zenu kwa chaguzi zao.Ya ngoswe mwachie ngoswe Chaguzi za Tanzania zimewashinda za Sweden mtaziweza? Kanye utakuwa ok frustration Wataalamu husema kama unazo ukinya huwa zinaisha Kanye upunguze political frustration za kubwagwa chaguzi Tanzania
 
Na leo madiwani wengine 4 wameachia ngazi CUF na kujiunga CCM.....tunaendelea hii ni Africa na si ulaya!!
 
Wasweden ndio wanatakiwa kuja kujifunza kwetu sisi tulikataa vyama vingi kupunguza gharama za chaguzi Na figisufigisu kama hizo za vyama vingi wakatulazimisha lazima tuingie vyama vingi tukakubali shingo upande wakati asilimia 80 ya watanzania walikataa vyama vingi.Ona sasa wao wanaojitia vinara wa vyama vingi wamekwaa kisiki.Waje Tanzania watuombe CCM tuwafundishe namna ya kujikwamua kwenye huo mkwamo.
labda waje muwafundishe kuua watu na kutia maiti kwenye maroba
 
Back
Top Bottom