MwanaFalsafa1
JF-Expert Member
- Feb 26, 2008
- 5,564
- 849
As for me sina haja ya kuwa mwanachama wa chama chochote, kwanza haina maana ni kupoteza fedha yangu kulipia kadi wakati tayari wanakula ruzuku kutokana na kodi ninayokatwa. Na kwa hali ya sisi ni maana ya kuwa na wanachama? labda kama unataka kugombea uongozi kwenye hicho chama ni sawa lakini vingenevyo ni bora kukaa pembeni na kuwa mshabiki tu.
Watu wengi si kwamba wanaipenda sana Chadema, bali wamechoshwa na usanii wa CCM ndio wanaona labda Chadema inaweza wasogeza mbali. Hivyo kama Chadema nao wakiingia na kufanya kama wanavyofanya CCM dawa ni ile ile, piga chini angalia wengine wanaoweza kutupeleka and may be by that time CCM watakuwa wameshajifunza kinaweza tena kuwa chama kizuri!!
hatushabikii uanachama wa chama flani bali tunakubali chama kinachotetea maslahi ya watanzania sio maslahi ya 10%...kwa sasa mimi naona cdm ndio chama pekee kinachojua watanzania maskini wanataka nini sio hawa mafisadi wa magamba..
Ni kweli mkuu si lazima uwe mwanachama. Ila unaweza ukawa mshabiki ila mwenye mapenzi ya kweli. Mfano ni mtu uwe shabiki wa Simba. Unaweza usiwe mwanachama ila unaipenda timu na siku zote upo nae aidha iwe juu au iwe chini. Ndicho haswa mimi ninacho ongelea.
Na unacho sema kwamba si kwamba wanaipenda Chadema bali wamechoshwa na CCM ina maana lengo kubwa haswa la watu ni CCM ijirekebisha kwa hiyo ikisha fanya hivyo Chadema itasahaulika?
Lengo kubwa la watanzania ni kuboreshwa kwa maslahi ya maisha na maendeleo ya nchi yetu iwe kupitia Chadema, CCM, NCCR, PPPT n.k. Lakini kwa hali halisi ya sasa, CCM haiwezi kujirekebisha bila kwanza kupigwa chini vinginevyo ni kujidanganya. Maana mle wamejificha watu wenye "madhambi" na madudu kibao na ili waendelee kuwa salama ni lazima waendelee kufanya madhambi mengine waweze kujilinda.
Alisema mwalimu Nyerere CCM imekuwa chaka ambalo watu wenye madudu yao wanakimbilia kujificha ili mambo yao yaende sawa, na hawa watu hawatakubali watolewe peupe ili wahukumiwe, wenyewe mnaita magamba. Kiukweli zaidi ya asilimia 80 ya viongozi ndani ya CCM ni magamba, angalia mfano tu rahisi jinsi wabunge wa CCM wanavyosema Polisi kuuua raia Arusha, Tarime etc ni sawa!! Kweli mtu mwenye akili anaweza kushabikia kitu kama hiki?
Nimefuatilia post yako na naona umetaja tu Chadema..inamaana chadema ndicho chama pekee cha upinzani TZ?
Chadema hii hii nayoijua ya Ubinafsi, majigamo, utemi, ukabila, udini na utabaka,kwa mawazo yako chama kama hiki kitakaa kipate majority support na kiongoze nchi?
Kweli mkuu nakubaliana na wewe. Ili Tanzania kuwa na demokrasia halisi ya vyama vingi ni lazima chama kilicho kaa madarakani tangia uhuru kianguke. Hii itajenga utamaduni wa kupokezana madaraka kati ya vyama na vyama na pia itajenga nidhamu ya vyama kuheshimu wananchi kwani wanajua hawawezi kufanya upumbavu wowote tu na waendelee kufaiidi madaraka. Kwa sasa kiburi kikubwa cha CCM ni kwamba bado hakuna ile kuamini kwamba ipo siku wanaweza angushwa.
kama mmoja wa wataka mabadilko ndani ya mwaka wakishika madaraka naweza kujua kama nao CDM watakuwa adui. na vigezo ni hivyo hivyo vinavyofanya CCM iwe adui leo.Binafsi sitegemei chama chochote kitachoiangusha CCM ifanye miujiza miaka ya mwanzo. Kazi kubwa itakuwa ni clear mess ya CCM kuweka mfumo na utaritibu itayochochea utawala wa sheria moja kwa wote. utengansha Utendajina siasa ( Eg TAKUKURU, Polisi)
Sasa swali langu ni je mashabiki wa Chadema ambao si wanachama bado wataendelea kuwa mashabiki pindi Chadema itakapo bahatika kushika madaraka? Je CCM ikisha anguka adui atakua nani?
Enheee si unaona CCM inajipanga na kureform ikiwa madarakani. CCM itakuwa reformed vizuri na tarudi kuwa chama izuri kikikaa nje ya system japo kwa miaka mitano au kumi . Jibu hapa kimbilio laweza kuwa tena CCM au chama kingine chocote inategema na wakati hou hali itakuwaje. Haya mambo hayako static. But ni ukweli ulio wazi CCM ikiwekwa bench basi itazaliwa upya na itakuja ile CCM ya wananchi.
Je kama Chadema ikibahatika kushika madaraka na waka chemsha na wao kimbilio litakua lipi?........
Nauliza hivi kwa sababu kuna tofauti kati ya kuwa pro-Chadema na anti-CCM. Kuwa pro-Chadema ina maana wewe umeiva uana Chadema na upo nacho kwa hali yoyote. Kuwa anti-CCM ina maanisha wewe haufuati itikadi zozote bali lengo ni kuiona tu CCM ikiondoka na hata kesho kikitokea chama kingine cha upinzani chenye nguvu basi utahamia huko........
nadhani nami pia naangukia kwenye kundi la wanaotaka mabadiliko.i admit few weeks ago nimechukua kadi ya chadema,lakini baada ya kufikiria kuwa maybe kuna siku nitaihitaji nitakapoamua ku-koki hii bunduki. japokuwa for the past 2 yrs nimekuwa niki-contribute here and there kwa chama. ninachotaka mimi ni badiliko na uwajibikaji. obviliously ccm imeshindwa kunipa ninachotaka, hopefully chadema can. ila na chadema pia ikishindwa, wala sitaona aibu kuitaliki! unakumbuka excitement iliyokuja na ccj? lakini baada ya kuonekana ccj haikidhi kiu ya wengi,well.. niseme kuwa chadema imeweza kuleta matumaini kiasi hichi hata kwa wanachama wa ccm pia. ndo maana hata kwenye uchaguzi kuna majimbo yalichagua mbunge wa chadema na rais wa ccm and vice versa. so kuwa mwanachama ama kutokuwa haina uhusiano directly na kuwa na imani na chadema.
Inabidi ifike wakati tuwe kama Marekani au Uingereza, chama kinapewa nafasi ya kuongoza kutokana na sera zake then kikishindwa kutekeleza uchaguzi unaofuata kinawekwa pembeni wanapewa wengine. Lakini hii itahitaji tubadilishe Katiba yetu ile watu kama Wakuu wa Mikoa na Wilaya aidha waondolewe maana ni Makada wa vyama au wawe civil servants ambao hawaruhusiwi kuwa wanachama wa vyama vya siasa, maana hawa ndio wanatumika hasa na serikali ya CCM kuua demokrasia nchini.
Mkuu Mtazamaji,
..............Ila alicho kua ana maanisha ni kwamba tusikimbilia kuchukua option ya pili kabla hatuja tafakari na kuona ni bora zaidi. Je Watanzania wame tafakari na kujiaminisha kwamba kweli Chadema ni tofauti na CCM na kweli kikipata madaraka kuna nafasi ya kuwa tofauti (siyo lazima kuleta mabadiliko makubwa) na CCM?
Cha pili ni kwamba muda si mrefu wazee wa CCM wenye makamo ya JK na kwenda juu karibia wata staafu au kuwa wachache. Je vijana wanao chipukia CCM wanaweza kutoa changamoto kwa kujionesha kuwa wao ni tofauti na "the old guard"?