Swali pendwa kwa mjasiriamali

MSDK pj

Member
Jul 17, 2021
10
29
Funzo la siku ya leo👇🏽

Nataka Nifanye Biashara Unanishauri Nifanye Biashara gani inayolipa🤷🏽‍♂️🤷🏽‍♂️ Swali hilo ndilo swali linaloongoza kwa kuulizwa na watu wengi kuliko swali lolote lile. Mara Nyingi huwa nawajibu "HAKUNA"

Kuna kitu cha mwanzo kabla ya kitu BIASHARA.

Biashara ni Kitu cha Pili! Kitu cha kwanza ni kujenga ujuzi kwanza. Watu wote waliofanikiwa katika Biashara kitu cha kwanza walijenga ujuzi sio hiyo Biashara bali ni UJUZI (Skills)

Swali la kujiuliza sio Nifanye Biashara gani? Jiulize hivi "Nina uwezo wa kutatua Changamoto gani?" Usifanye Biashara bali tatua Matatizo ya watu.

Usifanye Biashara bali towa hitaji fulani kwa watu. Usifanye biashara unayosikia inalipa bali fanya biashara unayoijua vizuri sana na kuielewa inavyofanywa. Biashara ni Wewe sio kile unachokiuza. Bidhaa ni ile hisia mteja anayoondoka nayo baada ya kutoka katika sehemu yako ya Biashara

Jenga ujuzi unaotatua matatizo ya watu kwanza na biashara itatokea hapo. Biashara yako sio kile unachokiuza aidha ni bidhaa/huduma bali ni lile Tatizo unalolitatua au ni lile hitaji unalopeleka kwemye jamii wanohitaj hitaji hilo. Biashara sio kile unachokiuza Bali ni Jinsi unavyokiuza (It's not the WHAT you sell it is the HOW you you sell)

Ukifikiria kwanza Biashara ya kufanya utaingia katika mtego unaoitwa "Product centric " unawaza kuuza bidhaa badala ya kuwawaza wale unaotaka kuwauzia Hiyo bidhaa

Huwa nashauri usikipende kile unachokiuza bali wapende wale unaowauzia watakwambia jinsi wanavyotaka kuuziwa (Never fall in love with your product, fall in love with your customers)

Kuwa aina ya mjasiriamali anaeitwa "Customer Centric " Unawasikiliza walengwa wa kile unachokiuza na kuwasaidia kutatua matatizo yao. Kuwa mtaalamu na mshauri wa kile unachokiuza (Expert &Consultant)

Watu huwa hawapendi kuuziwa ila Wanapenda kununua suluhisho au hitaji. Wateja huwa hawajali kile unachokijua mpaka pale utakapojali kuhusu wao (They don't care how much you know until they know how much you care)

Je, wewe ni Mjasiriamali wa aina gani?
 
Back
Top Bottom