Nijuavyo mimi, madhehebu yote ya kikristu, ukiondoa Roman Catholic, yanaitwa Protestants. Sasa Ukiwa Mkatoliki (kama mimi) hauwezi at the same time ukawa unaprotest against Catholic church, yaani a protestant. Sana sana utakuwa muhudhuriaji tu kwa upande mmojawapo. Hili jibu ni kwa mujibu wa mimi na linahusu Ukatoliki vs Ulokole. Kuhusu Ulokole vs other protestant churches watakuja wajibu wenyewe
Naomba tujihadhari na mihemko ...
naomba kuuliza kuwa kujua tu niko curious
Naomba wenye kukashifu mkae pembeni..lengo ni kuelimishana tu..
Swali langu ni hili...
Mtu anaweza kuwa mlokole na still mkatoliki au mlutheri?
Je tunaweza sema mtu anasali kwa gwajima au TB Joshua but still mkatoliki au mlutheri?
je Gwajima yeye binafsi anaweza kuwa mkatoliki pia au mlutheri?
Nikirejea mafundisho niliyopata, kama hakuna kanisa la Kikatoliki lililo karibu, Mkatoliki anaruhusiwa kuhudhuria ibada ya kanisa la Anglican, na kama Anglican hawapo eneo hilo, anaruhusiwa kuhudhuria ibada ya Lutheran, na yote hayo with a condition that hatakiwi kushiriki sakramenti zao (kama zipo), bali kusali tu. Other Protestant churches kama za kilokole hairuhusiwi kwani wamekuwa too critical kwa RC kuliko hata waasi wa mwanzo (Lutheran & Anglican)So ni sawa kwa mkatoliki kuhudhuria ibada kwa Gwajima au TB Joshua?
na still akawa mkatoliki?
Hujanijibu swali bado
Katika kusoma kwangu biblia sijawahi kukutana na hayo maneno "Mlokole, mlutheri, mkatoliki, Muanglican, Wa Gwajima nk" kama substitute ya wafuasi wa Yesu. Nimekutana na Neno moja tu kama Subsitute na liko kwenye maandiko ya biblia..."Na wanafunzi waliitwa WAKRISTO kwanza hapo Antiokia." -Matendo ya Mitume 11:26 ... Ukisoma mistari ya nyuma utagundua kuwa Jina hilo walipewa na gentiles likiwa na maana, "Hawa ni wafuasi/watu wa Kristo, au wanatenda kama mkristo." Hivyo basi mtu yeyote ambaye hatendi kama Kristo huyo si Mkristo ... Hizo titles zingine sijui mlokole etc hazina maana, yatosha kuitwa Mkristo kama utafahamu uzito na maana yake...!
Ni kweli; Ni vyema mtu akawa na sehemu ya kukutania na wenzake ktk Imani (Fellowship) & akawa na Mchungaji wa kumlea kiroho. Lakini sio afya kiimani kufungwa katika namna ya kujifunza. Mimi wazazi wangu wote ni Wakristo & walikuwa wanasali ktk denominations tofauti. Mimi naingia popote pale, coz msingi wa Neno/Imani ni mmoja. Lengo ni kujifunza zaidi...! Hao wanaobaguana utafikiri ni Imani tofauti, inabidi warudi wayachunguze maandiko vizuri.Wapo wakristo walokole hawaruhusiwi kuwa na madhehebu mengine...
Kajamaa kanazunguuka, Swali lako ni Dk. Slaa kusali kwa Gwajima kunamuodolea ukatoliki wake?? Idiot
Sijui kama Slaa anasali kwa Gwajima..
nimeuliza baada ya kuona picha za Lowassa na Magufuli kwa TB Joshua
halafu tunaambiwa ni RC na Lutheran...nilifikiri ni walokole