Swali la Ugomvi: Mnaounga mkono polisi kupiga raia kwa jina la 'amani na utulivu" jibuni hili...

Mzee Mwanakijiji unachungulia tu, changia mkuu!!!
Mkuu nilivyo ona huu uzi kua umetoka kwa mwanakijiji nimeusoma mbiombio,nakawa siamini kua haya yameandikwa nae,ikabidi niangalie muda duu kumbe ni zamazileee.yeye siku hizi yuko zama mpyaa.amebakia kule fb na matangazo yake ya serikali kugawa kondom 21m.wazungu walipo sema time will tell waliona mbali sanaa.
 
Ndo maana mimi kila mara nasema kwamba ni vizuri kuweka akiba ya maneno! Leo ukimsoma ndugu yangu Mwanakijiji amegeuka nyuzi 360! Kwa lugha nyingine Mwanakijiji haya maneno yake hayaamini tena.

Kazi kweli kweli!
So kuyaamini tu hata kuyaona hatakii,huko aliko analaumu sana jf kutunza huu uzi
 
Njaa imeshampanda kichwani anahitaji tiba MM maana anachokifanya kwa sasa ni zaidi ya mwehu,
Asante sana JF kwa kutunza kimbukumbu minafiki kama MM inaumbuka mchana kweupe
 
Acheni kufukua makaburi jamani ,watu wanabadilika kutokana na mambo mbali mbali ,hivi unawezaje kuweka trust kwa mwanadamu ,kiumbe dhaifu kilichojaa tamaa nk ?
Mkuu kwa hiyo unataka kusema Mwanakijiji ametamani pilau ya Lumumba ndio maana amekengeuka?
 
Mimi nilidhani watu wote wanaotumia jf angalau wana elimu ya msingi. Kama ndivyo ina maana una miaka angalau 13 au 14. Kwa hiyo unadhani ni sahihi kwa polisi kukamata watu hovyo kwa sababu tu watu wameketi kwenye jumba wakikutana kwa amani ndani ya hoteli kujadili kuhusu haki yao ya kufanya siasa na kuwapotezea muda? Na wakati mwingine kupigwa? Ninauliza haya kwa sababu ninashangaa ninapokutana na comments zilizo so careless kama kusema " wacha wapigwe tu". Polisi hatakiwi kupiga mtu yeyote ambaye hana silaha hata kama wanadhania ni mhalifu.
 
Mimi nilidhani watu wote wanaotumia jf angalau wana elimu ya msingi. Kama ndivyo ina maana una miaka angalau 13 au 14. Kwa hiyo unadhani ni sahihi kwa polisi kukamata watu hovyo kwa sababu tu watu wameketi kwenye jumba wakikutana kwa amani ndani ya hoteli kujadili kuhusu haki yao ya kufanya siasa na kuwapotezea muda? Na wakati mwingine kupigwa? Ninauliza haya kwa sababu ninashangaa ninapokutana na comments zilizo so careless kama kusema " wacha wapigwe tu". Polisi hatakiwi kupiga mtu yeyote ambaye hana silaha hata kama wanadhania ni mhalifu.
Easy, Easy, Easy, calm down, JF haiitaji hasira ukija huku control ur temper, huku kuna viumbe akili zao huwa wanazifungia kabatini halafu ndio wanaingia huku.

Be careful waweza kupata strock huku.
 

Nimekutaa hii hapa kwenye facebook page ya Jeshi la polisi.

Tanzania police

September 20, 2012



jamani ninge penda kawafahamisha kwamba kwanini polisi ulazimika kutumia silaha za moto kwa mujibu wa sheria !


-polisi atatumia siraha za moto katika kujilinda na kuwalinda wengine dhidi ya tishio dhahili la la kifo na maumivu makubwa.

-kumzuia mwalifu wa uhalifu mkubwa unaohusisha tukio kubwa la maisha!

-kumkamata anaye sababisha hatali kubwa ya maisha na ambaye anakaidi kutii amri!

-kumzuia mwalifu asitoroke tu pale mabapo njia sisizo za athari kubwa zitakapo onekana kushindwa kufika lengo!
attachment.php


My take:
Mazingira wanayotumia silaha za moto kwenye mazingira ya kisiasa hayaangukii kwenye kifungu tajwa

Pia ameacha kipengele muhimu kuwa wanapolazimika kutumia silaha za moto wanapaswa kulenga miguu!

Duu, aisee kumbe inapaswa walenge mguu/miguu


Sikujua hilo jambo
 
Wenzetu nyinyi mngekuwa upande gani wakati wa mkoloni? Maana wakoloni hawakutaka kusumbuliwa na waliwashtaki wapigania uhuru kadha wa kadha kwa uchochezi na kuleta vurugu. Hata kuundwa kwa Field Force Unit ilikuwa ni kwa malengo ya kuhakikisha hakuna vurugu katika koloni. Wenzetu mngekuwa upande gani?

Au kama mngekuwa mnaishi chini utawala wa kikaburu kule Afrika ya Kusini wenzetu mngekuwa upande gani? Kweli mngekuwa upande wa wapigania uhuru na haki au mngekuwa upande wa serikali kwa sababu serikali inataka kutawala bila kusumbuliwa? Kwenye mauaji ya Sowetto, Sharpeville na kuuawa kwa watu kama kina Chris Hani na Steve Biko wenzetu mngesemaje? Si mngewaambia kwanini hawakusikiliza serikali iliposema wasiandamane au wasiipinge?

Wenzetu mnaoamini kuwa watawala wanatakiwa kutawala bila kuulizwa, kula bila kukatazwa na kufanya watakalo popote, lolote na kwa yeyote hivi kweli si ndio mngekuwa wale vibaraka wa makaburu ambao walikuwa ni weusi walioamini kuwa makaburu watatawala milele na hivyo wakaweka maisha yao mikononi mwao? Na wao weusi wale walipokutana na wanaharakati weusi waliwaambia yale yale - serikali imesema inabidi mtii, na kuwa kupinga serikali ni kujitakia majanga kwani serikali itawapiga tu ni lazima iwapige si ndivyo nanyi mnavyoamini?

Siyo kwamba kama wale waliotetea tawala za kibabe iwe Marekani, Afrika ya Kusini au Kenya walichagua upande mbaya wa historia? Je na nyinyi siyo kwamba mmeamua kusimama upande wa tembo anapomkanyaga siafu na kusema ati nyinyi mko neutral?

Kweli katika historia ya kupigania uhuru na haki za wananchi wenzetu mngekuwa upande gani? siyo kwamba mngekuwa upande ule ule mlio sasa....?

Wa watawala walioshindwa?
Hatuwezi kujibu swali ambalo halina kichwa wala miguu,wanaongoza Tanzanaia ni watanzania wenzetu tulio wachagua kwa uhuru na amani,na ndio maana tulimfukuza mkoroni ili tujitawale wenyewe,tuijenge nchi yetu wenyewe,na sasa mda tunaijenga wanakuja wapuuzi wachache wanataka kutupotezea mda wa kujenga nchi na tuanze kulumbana juu ya upumbavu kamwe hatuwezi kuruhusu,watu hawa wanaojifanya wanaipigania demokrasia wao ndio wamekuwa vinara wa kusigina katiba za vyama vyao leo wanakuja kuhubiri kuhusu katiba,ndio maana naungana na hoja ya kuwa wapigwe tu sababu wanavunja sheria za nchi.
 
INASEMEKANA LEO DAR KUNA KAMATAKAMATA BILA SABABU YOYOTE,WANAKAMATWA WENYE BODA BODA HADI WENYE BAJAJI N'A RAIA WA KAWAIDA,UNAPEWA KIBANO N'A KUPANDISHWA KWENYE DIFENDAAA....

OVA
 
Back
Top Bottom