Swali la Ufahamu kwa hawa Celebrities Wetu hasa Wasanii

ESPRESSO COFFEE

JF-Expert Member
Sep 6, 2014
6,170
7,662
Leo nina swali,Wasanii hapa Bongo ni wengi sana na hawa wasanii ni wachache sanaa ambao hawana Management! Diamond ndo nahisi anaongoza kwa kuwa na management kubwa na huwa sijui wote wanafaidika vipi kwa msanii mmoja,sijuagi kama DIAMOND akafanya show ya millioni 20 sijui yeye anapata shilingi ngapi,Sijui babu tale hapo anafaidika vipi au Sallaam anafaidika vipi au mkubwa fela anafaidika vipi toka kwenye hiyo helaa!! Anyway hayo ni mambo ya Management ambayo sina uelewa nayo

Lakini swali langu la msingi ni hili kwanini hawa mamanager wa kibongo wanakuwa wanafahamika sawa na msanii na wengine wanawazidi wasanii wao kwa kuwa maarufu huwa sielewi hapa inakuwaje

Mfano babu tale,Sallaam,Mkubwa Fela,ostadhi Juma, na Mamaanager wengine wengi tuuu naona wanakuwa maarufu kuliko wasanii ambao wana wamanage sasa nini maana ya kuwa na Hiii kitu? Ni nani ambae anastahili kuwa maarufu manager au msanii? Naombeni mnieleweshe

Hii ipo hadi kwenye soka,Msemaji wa club anakuwa maarufu kuliko Kocha wa timu husika.......Sasa mimi huwa sielewi sisi wabongoo hii inakaaje na ni Tanzania tuuu ndo naona maManager ndo maarufu kuliko msanii!

Tuangalie nchi za wenzetu zilizo endelea ambazo mara nyingi huwa tunajifunza toka huko, huwezi kuona Manager wa Just bieber ana umarufu kuliko Bieber!! Hope nimeeleweka naomba nieleweshe kuhusu management za kibongooo!!
 
Kuna yule wakala wa Sterling Raheem,alikuwa anaongea kuhusiana na uhamisho wa jamaa kuliko mchezaji mwenyewe.
Aliweza kusema kuwa Raheem hawezi kusign mkataba mpya liverpool hata wampe kiasi gani cha pesa.
Huyu alikuwa kama Muro ama Manara tu.
YNWA
 
Kufahamika hapa dar tu maybe lkn sio kwel kwamba wanafahamika kuliko wasanii mfano mimi kuwajua hao
mameneja ni via social network lkn kwamtu ambaye hayupo karibu na mitandao ya kijamii atabak kumsikia tu msanii kwenye redio,,bar,tv,,matamasha na kwenye vyombo vya usafir
 
danya umebugi huu utafiti wako hauko sawa,na kama alivyosema mchangiaji mmoja hapo juu,kwanza hiyo ipo kwa baadhi ya wasanii na pili ni kwa hapa mjini tu na tena kwa wale wanaingia mitandaoni ndio wanawajua hao (mameneja) lakini si watu wengi wanaowajua. Lakini tukirudi ni jinsi gani mapato ya DIAMOND na Mameneja wake anayagawanya ni KWA MTINDO WA ASILIMIA FULANI NI YA MAMENEJA NA KIASI FULANI NI CHA DANCERS,DJ, BAUNSA NA WENGINE WAPO KWENYE MISHAHARA YA MWISHO WA MWEZI. ( kumbuka hata hawa mameneja alionao DIAMOND bado ni wachache sana kwani alitakiwa awe nao si chini ya 5-7 hawa wawe wanamuhusu yeye tu na si timu nzima ya WCB )
 
Back
Top Bottom