Jidu La Mabambasi
JF-Expert Member
- Oct 20, 2014
- 16,102
- 25,974
Wakoloni pamoja na ubaya wao, walikuwa wanaona mbali.
Kutokana na tabia za watu walitenga wazi wazi, mikoa ya wafugaji na mikoa ya wakulima.
Na wakaenda mbali kuwa sehemu nyingine mifugo isikanyage asilani.
Siye kwa sababu nzuri tu za kuwaridhisha wapiga kura, zile imaginary boundaries zikavunjwa kabisa.
Ng'ombe, punda, mbuzi sasa ruksa kuzurura popote palipo na uoto wa kijani!
Na huwa hawaondoki hapo mpaka uoto wote wa kijani umeharibiwa kabisa.
Nenda leo sehemu za Shinyanga, Mwanza,Tabora, Manyara n Arusha.
Mikoa ya wafugaji.
Uharibifu wa ardhi ni kama hauonekani machoni pa wanasiasa wetu, lakini vile vile hakuna hatua zinzochukuliwa.
Leo mifugo inaleta dhahma Mvomero, Kilosa na na vianzo vya maji huko Ruaha.
Ule uharibifu wa mikoa ya wafugaji unanyemelea kwa kasi mikoa ya wakulima.
Ati sasa yanaatoka maagizo ya nusunusu wafugaji na wakulima watengewe sehemu zao!
Watatengewa vipi kwingine wakati kule kwao walikotengewa walisha fanya uharibifu wa kutisha.
Hivi kwa nini hao wafugaji wasipandishwe mlima Kilimanjaro na Meru, kwenye uoto mzuri zaidi?
Haya matatizo tumeyalea ili watu wapate umarufu wa kisiasa.
Sasa lazima watajwe.
Nani aliruhusu mifugo na wafugaji kuzurura nchi nzima?