Swali la Lazima: Kwanini Mmiliki na Mkuu wa Shule ya Watoto Waliokufa Bado Wako Huru?

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Mar 10, 2006
33,742
40,874
Kati ya vitu vya kwanza ambavyo nilitarajia vingekuwa vimekwishafanyika ni kuhakikisha kuwa mmiliki/wamiliki wa shule ya Lucky Vincent ambayo wanafunzi wake 33, walimu na dereva walikufa kwenye ajali wanatiwa mbaroni mara moja na kushtakiwa kwa criminal negligence (sijui vizuri sheria za Tanzania kosa hili linaitwaje au kama kuna kosa linaloshabihiana na hilo).

Kwa bahati mbaya mara moja watu wameonekana kumlaumu dereva; inawezekana kwa usahihi lakini nadhani ni kutokuwa wa kweli wa kinachoendelea au kilichoendelea.

1. Shule ina mabasi mangapi na kwanini walitumia basi dogo moja kusafirisha wanafunzi wote hao? Hili haiwezekani kuwa lilikuwa ni suala la dereva kujiamulia.

2. Shule ina sera gani katika kusafirisha wanafunzi na katika kuhakikisha wanasafiri salama (labda swali hili linaweza kumhusu Ndalichako pia). Ni vyombo gani vinaruhusiwa kusafirisha wanafunzi na vinatakiwa viwe katika viwango gani? Yanayoitwa "school buses" kwa wenzetu hayako vile kwa sababu ya kupenda tu; kuna sababu yameundwa hivyo ya yanasimamiwa kwa sheria na kanuni mbalimbali za miji na zile za kitaifa. Halmashauri zetu zina kanuni au sheria ndogo gani za kusimamia mabasi ya wanafunzi?

Nakumbuka wakati fulani mabasi yetu ya abiria yaliwekewa zile 'speed governors' a.k.a vidhibiti mwendo; je, mabasi ya yanayobeba abiria yanatakiwa kuwa na vidhibiti mwendo vyovyote? je iko sheria yoyote inayotaka mabasi ya aina hiyo kutokwenda zaidi ya mwendo fulani wakiongozwa na kanuni ya 'kawia ufike'?

3. Ni mpaka lini tutawaacha wamiliki wa vyombo au sehemu mbalimbali huru wakati linapotokea janga ambalo chanzo chake ni uzembe, uvunjaji wa sheria au kutokujali maisha ya watu?

Mifano: Mwaka jana, huko California mmiliki wa mabasi ya utalii alishtakiwa kwa makosa ya uzembe wa kihalifu uliosababisha vifo vya watu.

Mwaka 2013 huko huko California mmiliki mwingine wa mabasi naye alishtakiwa kwa makosa ya kutafanyia matengenezo magari yake na kusababisha ajali iliyoua mtu mmoja.

Mapema mwaka huu huko huko California mmiliki wa pantoni alikamatwa na kushtakiwa baada ya mtoto mdogo kuanguka na kutumbukia majini. Uchunguzi ulionesha pantoni hiyo ya kukodi ilikuwa imejaza watu zaidi na haikuwa na vyombo vya kutosha vya usalama.

Hadi tutakapoanza kuwafunga wamiliki wa vyombo na taasisi mbalimbali ambazo kutokana na uzembe wao watu wanakufa au kujeruhiwa (kama kwenye club za muziki n.k) ndio tutaanza kuona mabadiliko ya tabia. Na siyo kuwafunga tu; kulazimisha bima zao kulipa fidia kwa watu hawa badala ya watu kudai tu fidia. Watu 35 wanakufa na mtu anataka kuendelea na biashara kama kawaida?

Sijali sana nani anazungumza msibani, sijali sana nani anatoa pole na kwa sauti gani ya upole na majonzi! sijali sana nani tena sijali kabisa nani ametoa machozi kwa kuguswa na picha za majeneza zilizorushwa mubashara; sijali sana hata watu kutumiana picha za mishumaa!

Ninachojali ni kuona kuwa kama Bwana ametoa Bwana ametwaa basi na sisi tumsaidie Bwana kuwatwaa hawa wamiliki kutoka kwenye jamii ili na wao wakaone jinsi "Mungu anawapenda zaidi wakiwa jela!".

MMM

Admin: Sikumaanisha kuweka "tetesi" naomba mtu atoe hilo la "tetesi".
 
Mimi ningependa kuona vyombo vyote vya usafiri vikiwekewa 'black boxes'.

Kufanya hivyo itakuwa ni hatua moja kubwa sana ya kutafuta ufumbuzi juu ya hizi ajali za kizembe.

*Sitegemei walio wengi humu wanielewe juu ya hilo*
Kweendraaaa na u.s.a wako hizo gari zenyewe ukiingia ndani zingine zina matobo mpaka unaona lami mimi huwa nawashaangaa sana Traffic wa Tanzania akishakamata gari yeye anasimama nje kuangalia ndani hawaingii yaani ni balaa huku kwetu bado sana
 
Kweendraaaa na u.s.a wako hizo gari zenyewe ukiingia ndani zingine zina matobo mpaka unaona lami mimi huwa nawashaangaa sana Traffic wa Tanzania akishakamata gari yeye anasimama nje kuangalia ndani hawaingii yaani ni balaa huku kwetu bado sana

Niende na u USA wangu eeh?

Haya...na mtaendelea kufa kwa mafungu kama nzi....
 
Hoja kuntu hii, kwani siku ya tukio afisa elimu katika wilaya au jiji la Arusha alinukuliwa na vyombo vya habari akilaumu kutoombwa kibali cha kusafirisha wanafunzi toka wilaya moja hadi nyingine. Pia hili suala ya viwango ni muhimu, juzi sheria ilitaka kutungwa bungeni kuwajumuisha wenye mabasi kwa makosa yanayosababishwa na magari yao siasa iliingia kwa hali ya juu.
 
Back
Top Bottom