Swali la kujiuliza kuhusu Silaha za moto na Matumizi yake

Phd Hewa

JF-Expert Member
Oct 3, 2016
572
466
Ndugu zangu watanzania sina muda wa kurembesha post yangu nazama moja kwa moja kwenye lengo.

Siku za hivi karibuni tuliona mwananchi wa Tanzania na Mbunge ambae alikua waziri fulani na sasa ni mbunge siyo waziri.

Kwajina munamfahamu mwanachi huyo ambae pia ni mbunge alitishiwa kupigwa bastola hadharani wakati yeye siyo mhalifu.

Jana pia limetokea tukio la kutishiwa kupigwa bastola na mapanga kwa wanachama wa cuf na waandishi wa habari kwenye Conference ya chama cha cuf kilichotaka kuwepo hapo Jana tarehe 22/4/2017.

Na huku tukipata habari kua hilo ni kundi linalotumika na Pro Lipumba linalofahamika kwa jina la Mungiki aliyasema hayo Mtatiro.

mbaya zaidi matukio haya yanafanyika mchana kweupeeeee..!!!
nilisikitika sana nilipoangalia taarifa ya habari na kujionea waandishi wa habari wanavyolalamika kuhusu tukio la kutishiwa kifo kwa kutumia silaha wakati hao siyo majambazi na haikua vitani siamini kama Tanzania yetu imefikia hapa.

Maswali yanakuja hivi
awamu hii na silaha tunazotishiwa wanachi
wanazimiliki ili watutishie tufanye wanavyotaka wao na si kwa kufuata sheria zetu za nchi?

Au na sisi wananchi kwenye matukio kama haya tubebe na silaha zetu za jadi ili kujihami?

Nchi ikiharibika itakua tumeiharibu wenyewe kwa uzembe wetu..!

Ni ngumu sana kuirudisha amani ikishatoweka Mungu ibariki Tanzania.

PhD hewa a.k.a PhD fake
 
  • Thanks
Reactions: 999
Amani ya Tanzania ipo mikononi mwa............. ila inasumbuliwa sana na...................
 
Hili ni tatizo la kumpa mjinga uongozi.
Phd Hewa a.k.a PhD Fake uko sahihi kabisa.
Nchi inaendeshwa na layman wasiojua nini maana ya nchi, kuwaongoza wananchi.
Yaani haelewi lolote zaidi ya kubwabwaja tuuu ili asikike na kuandikwa kwenye vyombo vya habari.

Phd Hewa ni tatizo
 
Back
Top Bottom