Swali la Kimantiki: CCM wamuue Alphonce Mawazo kwa sababu zipi hasa?

We Msumari wa Moto acha kujiapiza kijinga hivyo kwamba Arusha itakuwa ya Chadema milele nadhani hujui na huamini kuwa siasa ni mchezo mchafu sana kwani una vitu ambavyo at any time waliokuwa wakikubeba kwenye kiti cha machela kama Kabaila watakubwaga ktk masanduku ya kura,vile vile waliokuwa wakikudekia barabara ya lami kuwa usije ukapata mafua ndiyo hao hao watakaokunyima kura na kumpa mwingine,nadhani mpaka hapo utakuwa umenielewa.Vicent Nyerere alikuwa akibeza kila kitu toka kwa mpinzani wake na kumfananisha na mtoto mdogo anayehangaika na baiskeli ya mbao,yaliyompata na Chama chake ni AIBU NA MUSOMA AMEIKIMBIA HAJULIKANI ALIKO,YASEMEKANA KATOKOMEA KANDA YA KASKAZINI.
 
Mtoa post,

Humu JF siku hizi tumeingiliwa na wanywa viroba wa Ufipa sasa sijui kama hoja zako zenye mashiko hivyo kama wataweza kuzijadili.

Ila kwa upande wangu nakubaliana na wewe kwenye maeneo mengi sana. Mfano hiyo ya motive, sioni nia ovu ya CCM dhidi Marehemu Mawazo. Mawazo pale kanda ya ziwa hakuwa hata na mtaa mmoja. Hakuwa hata na kijiji. Hakuwa hata na kitongoji. Sasa mtu wa hivyo atakuwa ni tishio kwa CCM!?! Tuwe tu wakweli hapa.

Kwa ninavyoona na elimu ndogo niliyoipata kwenye criminology. Naamini kabisa motive kubwa inaweza ikawa kwa wafanyabiashara wa madini wa kanda ya ziwa. Maana inajulikana kuwa marehemu alikuwa mtu wa matifutifu yaani kwa maneno mengine mtata. Hivyo huenda wale ma-big fish wa biashara ya madini wakaona wamuweke nje ya picha kwa kumtumia wahuni wamuue. Huko kwenye madini ndio polisi wachunguze zaidi.

Ikiwa kweli ndugu, jamaa na marafiki wa marehemu Mawazo wanataka kuwapata wauaji wa huyu ndugu yetu na sheria ichukue mkondo wake, basi waache kuegemea na kuamini kuwa ni CCM inahusika. Kufanya hivyo kutawaweka wauaji halisi salama na kuna uwezekano mkubwa wasikamatwe kabisa na haki ya marehemu wetu ikapotea.

Ni hayo tu.
 
Lema anaposema polisi wamehusika ni kwa sababu matukio kama haya yametokea sana na polisi hawajachukua hatua.
 
lema alitoa taarifa za msiba wa mawazo kabla hata kabla mawazo hajakata roho Huyu lema achunguzwe matamshi maana ndo anajitia kimbelembele cha kuwasingizia polisi..Something is behind
 
Mimi nadhani hoja kubwa hapa ni WAPI HUYU NDUGU YETU ANAYEJIITA MWANASHERIA ALISOMA?

Ishu siyo kwamba alisoma au lah? Ishu ni aliwezaje kutoka chuoni na hilo jina analojiita, yaani MWANASHERIA. Ikiwa mtu huyu atathibitisha kwa vyeti kuwa yeye ni kweli mwanasheria, na vyeti hivyo vikawa si vya kufoji......aliyempa anapaswa kuchunguzwa.
 
threat unazoongelea hapa ni mhusika mwenyewe dhidi ya mahasimu wake rejea kuwa mawazo alikuwa ccm hivyo anawajua weakness zao anapopanda jukwaani anamwaga sumu ya kutosha hivi upande mmoja kukosa raha hivyo ukiangalia kwa juu juu utaona weakness za upande mmoja ndio zilizaa threat hii ambayo haipo kwa sasa hivo kuleta strength upande mwingine

Kuna msululu wa watu kibao waliotoka ccm kwenda chadema,tena vichwa vya nguvu ,mawazili,wabunge,madiwani na wabiga domo kama kingunge ambao hawakuwa theat, sasa hiyo threat wako aliyepata unaarufu baada yA kufa alikuwa na jipya gani
 
kama ndo wanasheria tulionao mnaandika hivi, I'm sure tuna safari ndefu ya kufika nchi ya ahadi!!!

Hahahahahaha! Na pia km tutaendelea kulazmisha mambo yawe km tunavyotaka na kukataa yalivyo kwa sababu tuuu upande unaouhitaj unaona umeelemewa au uko chin kiuwezo hatutafka mbali
Nchi ya ahad kwa kuzusha mambo ,,bila ya kutafuta chanzo na kutazama mazingira ya tukio,,, tutaendelea kuwa wabebaji wa jazba za wenzetu wakat wao wanapunguza uwezekano wa ulcers kwa kutoa jazba zao na kukutwisha ww ambae umeamua kuwa unameza kila unachotapikiwa,,,,,
 
Amani ya Bwana iwe nanyi wadau,

Kwanza kabisa napenda kuanza kutoa pole kwa wale wote walioguswa na kifo na ndugu Alphonce Mawazo. Kifo chochote sio jambo la kawaida kwa hiyo hata iweje lazima pole itolewe hasa kwa wale walioguswa kwa dhati na kifo hiki.

Nikiwa natafakari kifo hiki kumekuwa na maneno mbalimbali yamekuwa yakiendelea humu mitandaaoni kwa watu kurushiana maneno hasa wakihusishana na kifo hiki. Watu hawa kwa kifupi ni wafuasi wa CHADEMA wakisema kuwa CCM wanahusika na kifo hiko, wengine wanadai kuwa ni polisi na huyu si mwingine bali ni mgombea ubunge wa jimbo la Arusha mjini ambaye ameenda mbali zaidi hadi kuwataja polisi kuwa wanahusika na kifo hicho.

Nikiwa mwanasheria na mdau wa mambo ya kisheria hapa napenda nishirikiane na wenzangu jambo hili, nalo ni kama nilivyoandika kwenye kichwa cha thread husika kuwa CCM WAMUUE MAWAZO KWA SABABU ZIPI HASA?

Hili swali linaweza kuonekana la ajabu kwa watu ambao sio critical thinkers ila kwa critical thinkers ni swali la msingi na la muhimu sana kwa sababu hata upande kwa upelelezi unapoanza kuchunguza tukio ili kumuhusisha mtuhumiwa na mauaji kwanza wanaanzaga kuangalia MOTIVE YAANI KWA LUGHA NYINGINE INTENTION.

Kwa wale msioelewa maana ya motive ni nia au dhamira ya mtenda kosa. Sasa kwenye hili tukio ili kuwahusisha CCM napenda kuuliza kuwa Je kuna sababu zipi hasa kwa CCM kumuua ndugu Mawazo ili tu kuweza kutengeneza au kupata motive yao?

Sijaandika ili kuwatetea CCM ila as long as taarifa za kipelelezi hazijatoka napenda tujiulize kwa pamoja kuna sababu gani za msingi kwa CCM kama chama kupanga au kutekeleza mauaji ya ndugu Mawazo?

Nimefikiria sana hata sijaweza pata hata moja kwa sababu hata kwa Geita mawazo hakuwa threat kwa chama kwa kusema kuwa hali ya upinzani kwenye uchaguzi huu kwa Geita imeonyesha kuwa haikuwa nzuri yaani hata ushawishi wao haujaonekana kwa sababu robo tatu ya mkoa tena kama sio wote kwenye uchaguzi uliomalizika imeenda CCM sasa kulikuwa na threat gani kwa CCM hadi waseme wamuue ndugu mawazo? kwa sababu ili iweze kuihusisha CCM na mauaji ya ndugu Mawazo lazima narudia ni lazima ili motive ipatikane tuweze kujiridhisha kiwango cha threat ambacho ndugu mawazo alikiweka kwa CCM. Kama hakijapatikana basi hapo hatuwezi kuihusisha CCM na mauaji ya ndugu Mawazo.

Jambo la pili ni kuhusiana na Polisi kwa sababu ndugu LEMA amejaribu kuwahusisha polisi, swali lilelile napenda kuli impose hapa Je, ndugu Mawazo alikuwa na threat gani kwa polisi hadi polisi wahusike na mauaji yake? Hadi sasa swali hili halijaweza kujibiwa popote pale.

Napenda kumaliza kwa kusema ingawa haturuhusiwi kuongelea upande negative wa marehemu ila hapa lazima tuseme kitu. Marehemu alikuwa anajulikana vizuri sana kuwa ni mtu mtata sana hasa kitabia na hulka na hata kuna thread humu ndani alizokuwa akimsema vibaya kwa vitisho ndugu Zitto Kabwe zinaonekana humu ndani. Naomba tusiondoe nadharia hii kwenye kifo cha marehemu kuwa inawezekana marehemu alikuwa kwenye ugomvi na wauaji wake na kwenye huo ugomvi ndo yakatokea yaliyotokea. Na pia inawezekana yeye ndo alikuwa mgomvi kwa sababau hadi sasa hivi hatujaweza kuelezwa kuwa marehemu alikuwa na nani na kitu gani kilitokea hadi kusababisha mauti yake.


MUNGU IBARIKI TANZANIA NA WATANZANIA.

Mkuu mwanasheria

Mimi natofautiana na wewe kidogo. Nadhani umetumia sehemu ndogo sana ya uelewa wako wa criminology.

Kwa Mtazamo wangu, sidhani kama primary intention ilikuwa kumuua (refer timeline btn yeye kushambuliwa na mda aliofariki). ideally waliomshambulia walitaka kumuadhibu/kumkomoa/harm ila sidhani kama walipanga afariki. So ishu ya motive of murder hapo sio strong point maana scenario kama hii. ,, Lakini bado ni mauaji be it murder or manslaughter
 
Akili yangu inaniambia Chadema wamemuua ili wapate la kuongelea kwny kampeni za majimbo yaliyobaki! Kubali au kataa ila hili jambo linapossibility kubwa sana
 
watu wa geita wapi! wale ni vijana wenu mliokaa mkawalisha maneno wa lopoke hovyo hovyo kwa faida za kisiasa, kila jambo likitokea kosa lenu kubwa ni kufanya mtaji wakisiasa angalia tukio la bomu la arusha mkajifanya mnaushaidi mwisho wa siku hadi leo hakuna kilichofanyika

Tuambie.....nani kamuua mwenyekiti wetu? kwa nini? manake inaonekana unajua kuliko mashuhuda
 
Back
Top Bottom