Ombwe kwa Kiingereza ni "Vacuum". Ni kweli kuwa fasihi haitokani ombe(kitu tupu/hewa) bali inatokana na mambo kadhaa yanayomsukuma Mwandishi kuiandikia jamii yake ili kuielimisha, kuionya na kuiasa, kuiadibu, kuifurahisha nk. Mwandishi hupata habari kwenye magazeti, kuona, misibani, matembezini, vilabuni nk. na kupata kung'amua mengi kama vile yaliyo kwenye KILIO CHETU; Athari za mapenzi, Tiba kwa wenye UKIMWI, Athari za marafiki, Dhana potofu. Hivyo basi, hilo swali linahitaji DHAMIRA.