Swali kwa watanzania | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Swali kwa watanzania

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Taifa_Kwanza, Mar 5, 2011.

 1. T

  Taifa_Kwanza JF-Expert Member

  #1
  Mar 5, 2011
  Joined: Sep 3, 2010
  Messages: 443
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Je Kama Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiamuakubadirika, akaacha safari zisizo na lazima nje ya nchi, akaanza kujishughulisha na matatizo yanayotukabiri kwa dhati kabisa na kujielekeza katika kuliendeleza taifa letu kwa haki, usawa, na kuonyesha mapenzi makubwa kwa watanzania kwa vitendo, na akasimama hima na kuanzisha mkakati madhubuti na endelevu wa siasa za vitendo katika kupambana na kudhibiti rushwa na ufisadi uliokisiri na zaidi akaanza kuzitekeleza ahadi zake alizotoa kipindi cha kampeni za uchaguzi n.k

  Imani na Mapenzi yetu kwake binafsi na CCM itajirudia na/ama kuongezeka zaidi??
   
 2. BONGOLALA

  BONGOLALA JF-Expert Member

  #2
  Mar 5, 2011
  Joined: Sep 14, 2009
  Messages: 13,791
  Likes Received: 2,398
  Trophy Points: 280
  Najiuliza inakuaje rwanda sera zao wanatekeleza kwa ufanisi mkubwa sisi tunarudi nyuma badala ya kusonga mbele?
   
 3. FaizaFoxy

  FaizaFoxy JF-Expert Member

  #3
  Mar 5, 2011
  Joined: Apr 13, 2011
  Messages: 58,107
  Likes Received: 22,158
  Trophy Points: 280
  Kutokuwa na mapenzi na Rais eti kwa sababu tu anasafiri sana, ni kukosa kina na mtazamo wa kazi na tija nyingi zinazotokana na hiyo mihangaiko ya Rais.

  Tanzania, kwa mara ya kwanza tumeona japo mvuto wa wawekezaji wakubwa duniani wakionesha nia ya kuwekeza kwenye nyanja tofauti hapa nchini. Hiyo ni moja kwa moja tija ya hizi safari za Rais.

  Kina Bill Gates na wenzake wanakuja kufunguwa kituo kikubwa cha utafiti wa mambo ya teknolojia hapo UDOM. Jee, umeshawahi kujiuliza na kwa jitihada za nani?

  Hilo ni moja tu ya mengi mema yanayotokana ma hizi safari za Rais. Tumeona wimbi la ma-star kutoka Merekani na Uropa likja Tanzania kutalii. Jee, umeshawahi kujiuliza hizo ni jitihada za nani?

  Mema ya JK ni mengi sana kwa Taifa letu lakini chuki na uhassidi usio na msingi kutoka kwa wachache, wajulikanao sababu zao, hujaribu kumpakazia na kuonekana kuwa hana alifanyalo.

  Ukweli unabaki palepale, hakuna Rais aliejituma na mafanikio ya dhahiri kuonekana katika nchi hii kama JK.
   
 4. Omuregi Wasu

  Omuregi Wasu JF-Expert Member

  #4
  Mar 5, 2011
  Joined: May 21, 2009
  Messages: 753
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Heshima yako mkuu.
  Binafsi naona umedanganya sana kupita kiasi au hujui kabisa unachokisema. Nikiwa mdogo kabisa amewahi kuja Marehemu Machel Jakson hapa Tanzania, tumewaona akina Campel n.k ,,, Je, wote waliletwa na safari za nje za Jk? Bill Gates ni investor hivyo hawezi kuwekeza eneo lisilolipa - anawekeza baada ya uchambuzi yakinifu kufanyika na si kwa safari za Rais wa nchi fulani kwenda kwake au kusafiri safari ndefu basi anazawadiwa uwekezaji na Bill Gates. Chukua mfano wa Rais Hu Jintao wa China anasafiri kama mara 10 kwa mwaka lakini Bill Gates amefanya investment za nguvu hapa China kuanzia magari ya BYD hadi compyuta.

  Naomba uwe na mtazamo sahihi wa maisha na si kudanganya au kudanganywa kama huna akili ya kufikiria. JK ameshindwa kutimiza ahadi zake mwenyewe ... well, ngoja nikukumbushe ahadi alizoisha sahau... Geita kuwa mkoa by January 2011, Ujenzi wa barabara ya lami eneo ya mahembe wilaya ya Kigoma vijijini kuanza mara moja aliahidi akifungua mradi wa maji bubujiko (toka mwaka jana april hakuna dalili hata ya dolori la kifusi), Uwanja wa ndege wa Kigma kujengwa kwa lami kuanzia januari 2011 lakina hakuna hata tangazo tu la zabuni. n.k hivi hapo ndo unapomsifu kuwa amefanya mambo mengi kwa watanzania?
   
Loading...