Sometimes mwanamke anaweza kutafsiri neno alilolitamka mwanaume tofauti na jinsi mwanaume alikuwa anamaanisha, na hata akipewa ufafanuzi hakubaliani; kwa kosa kama hili mimi siwezi kuomba msamaha kwa sababu sina kosa.
Baadhi ya makosa ni repititve, mwanaume unaona hakuna sababu ya kuomba msamaha wakati unajua kosa utalirudia, na samahani nyingi nazo zina-dilute radha ya samahani.
Ukiomba samahani unakuwa umekubali kwamba umekosa, so kuendelea kushikilia msimamo huombi samahani yoyote; au unasema tu "Samahani kama nimekukosea", hii ni samahani hewa kwa sababu haikubali kosa.
Sio kila kosa lina uzito wa samahani, makosa mengine ni madogo dogo tu, mnatakiwa kusema poa basi yaishe. Na baadhi ya wanawake ukiwa mwepesi sana wa kuomba samahani wanakuona msanii!!!