Swali kwa wanaume: Mnapenda mama wa nyumbani au mwanamke anayefanya kazi?

Paprika

JF-Expert Member
Feb 25, 2017
5,951
9,876
Habari,

Nina jirani yangu ni mwanachuo fulani hapa Dar, anaishi na mpenzi wake. Hii likizo amenitesa sana pua na tumbo kwa harufu nzuri za mapishi zinazotokea chumbani kwake asubuhi, mchana na jioni! Muda mwingine huwa ananiletea sahani imejaa matunda ili na mimi nijumuike nao kwa mbali.

Ninachouliza wanaume ni kwamba mnapenda mwanamke awe mama wa nyumbani na kutumia muda wake mwingi kukutunza wewe na familia na kama kutafuta fedha basi afanye biashara ndogo ndogo tu au mnapenda mwanamke aliye bize kutafuta pesa ili msaidiane majukumu ya kifedha?

Na kama unapenda msaidiane na mkeo kutafuta fedha, ni halali kweli kumtegemea akupikie, akufulie na akufanyie usafi?

Asanteni!
 
Habari!
Nina jirani yangu ni mwanachuo fulani hapa Dar, anaishi na mpenzi wake... Hii likizo amenitesa sana pua na tumbo kwa harufu nzuri za mapishi zinazotokea chumbani kwake asubuhi, mchana na jioni!!! Mda mwingine hua ananiletea sahani imejaa matunda ili na mimi nijumuike nao kwa mbali....

Ninachouliza wanaume ni kwamba mnapenda mwanamke awe mama wa nyumbani na kutumia mda wake mwingi kukutunza wewe na familia na kama kutafuta fedha basi afanye biashara ndogo ndogo tu au mnapenda mwanamke alie bize kutafuta pesa ili msaidiane majukumu ya kifedha?
Na kama unapenda msaidiane na mkeo kutafuta fedha, ni halali kweli kumtegemea akupikie, akufulie na akufanyie usafi??

Asanteni.!
Mimi napenda mwanamke muwajibikaji ili hata siku nikiwa hovyo najua mamii yupo,afu ukimzoesha kukaa hom tu,siku mwanaume anakufa t means lazima atasafa.
Lazima wanaume tuweze kuona nje ya box,km wife anakupenda hata akiwa anafanya kazi lazima atabalance rtb zake ili na we akupe muda
 
Vizuri!!! Ila utakuta mwanamke anafanya kazi za kutoka asubuhi na kurudi jioni na nyumbani hamna msaidizi... Na bado siku kama weekends wanaume wengine wanategemea mwanamke afanye kazi zote za nyumbani peke yake bila kumsaidia! Ni haki kweli?
 
Kitanzania kuna majukumu ya kike na kiume labda uamue kuwa tofauti ni wewe tu.

Kama unataka kuwa na mme atakayekuoshea vyombo, kuchotea maji, kufulia nguo, kupikia, kumtuma sokoni wapo tu ni chaguo lako.

Mimi napenda mwanamke anayejua mipaka yake na mimi niilinde yangu.
 
Tumia vema uwezo wako wa kufikiri,
Kilicho kuchanganya hapo ni sahani ya matunda na harufu ya kukaanga tangawizi na hoho,
Hio sio factor ya kujua kama kuna upendo wa ukweli hapo,
Kuna mengi nyuma ya pazia,

Nikufahamishe tu kuwa HULKA ZA WANACHUO WOTE NI KUCHEZEA TU NA KUPUNGUZA STRESS ZA MASOMO

Roho yangu inaniuma sana kuona wengi wetu tukishindwa kutumia vema uwezo wetu wa kufikiri tuliopewa na MUNGU.
 
Mwanamke kumpikia mumeo na kutunza famila yako au kuchukua majukumu yako kama Mama ni wajibu wako,iwe ni mfanya kazi au mama wa nyumbani,sio rahisi kuyafanya yote yanahitaji moyo na kujua kua wewe cheo chakoo nani sababau mwisho wa siku utabakia kua mwanamke tu, nikupe mfano wangu naafanya kazi,nna watoto 6 siku yangu inaanza 4AM kusali na kuamsha watoto wasali kupika breakfast kuwatayarisha watoto shule by 0600hrs watoto wako tayari,breakfast ya mr kabla sijatoka iwe tayari na 0615hrs natoka home kwenda kazini narudi 1630hrs home work ya watoto chakula cha jioni
by the time nikimaliza kusali 9pm mie sina hadith na mtu watoto nimesha walaza ndio naenda kulala,sio kama sina wafanya kazi
nnao ila mapenzi yangu napenda nipikie familia yangu niwalee ili na wao wajue thamani ya na mapenzi na utu sio kila kitu mfanya kazi no,mfanya kazi atafanya basic sio kila kitu Dada,sasa mkuu sio rahis wengi wana fail na hata mimi kuna time na fail labda kuamka kusali najikuta nimepitiwa lakini daima namuomba mungu aniwezeshe..
 
Tumia vema uwezo wako wa kufikiri,
Kilicho kuchanganya hapo ni sahani ya matunda na harufu ya kukaanga tangawizi na hoho,
Hio sio factor ya kujua kama kuna upendo wa ukweli hapo,
Kuna mengi nyuma ya pazia,

Nikufahamishe tu kuwa HULKA ZA WANACHUO WOTE NI KUCHEZEA TU NA KUPUNGUZA STRESS ZA MASOMO

Roho yangu inaniuma sana kuona wengi wetu tukishindwa kutumia vema uwezo wetu wa kufikiri tuliopewa na MUNGU.
Hujanielewa mkuu!!! Ninachomaanisha ni juhudi za huyo mdada kumpikia mpenzi wake milo yote mitatu kipindi hiki cha likizo tofauti na siku zingine za chuo. Achana na mambo ya upendo kwa sasa!
 
Kitanzania kuna majukumu ya kike na kiume labda uamue kuwa tofauti ni wewe tu.

Kama unataka kuwa na mme atakayekuoshea vyombo, kuchotea maji, kufulia nguo, kupikia, kumtuma sokoni wapo tu ni chaguo lako.

Mimi napenda mwanamke anayejua mipaka yake na mimi niilinde yangu.
Asante mkuu!
Kwa hiyo wewe unapendelea house-wife na vibiashara vidogodogo au full career-wife
 
Habari!
Nina jirani yangu ni mwanachuo fulani hapa Dar, anaishi na mpenzi wake... Hii likizo amenitesa sana pua na tumbo kwa harufu nzuri za mapishi zinazotokea chumbani kwake asubuhi, mchana na jioni!!! Mda mwingine hua ananiletea sahani imejaa matunda ili na mimi nijumuike nao kwa mbali....

Ninachouliza wanaume ni kwamba mnapenda mwanamke awe mama wa nyumbani na kutumia mda wake mwingi kukutunza wewe na familia na kama kutafuta fedha basi afanye biashara ndogo ndogo tu au mnapenda mwanamke alie bize kutafuta pesa ili msaidiane majukumu ya kifedha?
Na kama unapenda msaidiane na mkeo kutafuta fedha, ni halali kweli kumtegemea akupikie, akufulie na akufanyie usafi??

Asanteni.!
Mimi si mwanaume ila naomba nikurekebishe mwanamke mwenzangu
"Mbali na uwajibikaji wa kutafuta pesa na mahitaji mengine kwa familia, lakini mwanamke ni mwanamke tu na ili awe mke ni lazima atimize majukumu yake kwa mumewe na familia kwa ujumla, pesa yaweza kua si lolote si chochote kwenye familia lakini upendo ni nguzo muhimu,na upendo huletwa na mwanamke msikivu, muwajibikaji, muelewa na mchapa kazi" lakini kamwe hauletwi na mwanamke mjuaji, mvivu na kisirani. TIMIZA WAJIBU WAKO
 
Mwanamke kumpikia mumeo na kutunza famila yako au kuchukua majukumu yako kama Mama ni wajibu wako,iwe ni mfanya kazi au mama wa nyumbani,sio rahisi kuyafanya yote yanahitaji moyo na kujua kua wewe cheo chakoo nani sababau mwisho wa siku utabakia kua mwanamke tu, nikupe mfano wangu naafanya kazi,nna watoto 6 siku yangu inaanza 4AM kusali na kuamsha watoto wasali kupika breakfast kuwatayarisha watoto shule by 0600hrs watoto wako tayari,break ya mr kabla sijatoka iwe tayari na 0615hrs natoka home kwenda kazini narudi 1630hrs home work ya watoto chakula cha jioni
by nikimaliza kusali by 9pm mie sina hadith na mtu watoto nimesha walaza ndio naenda kulala,sio kama sina wafanya kazi
nnao ila mapenzi yangu napenda nipikie familia yangu niwalee ili na wao wajue thamani ya na mapenzi na utu sio kila kitu mfanya kazi no,mfanya kazi atafanya basic sio kila kitu Dada,sasa mkuu sio rahis wengi wana fail na hata mimi kuna time na fail labda kuamka kusali najikuta nimepitiwa lakini daima namuomba mungu aniwezeshe..
Uko vizuri mkuu! Mungu akupe moyo na nguvu za kuendelea kua mke na mama bora.
 
Vizuri!!! Ila utakuta mwanamke anafanya kazi za kutoka asubuhi na kurudi jioni na nyumbani hamna msaidizi... Na bado siku kama weekends wanaume wengine wanategemea mwanamke afanye kazi zote za nyumbani peke yake bila kumsaidia! Ni haki kweli?
Inategemea mtu na mtu paprika,mwanamke ni msaidizi wa mwanaume na siyo mfanyakazi wa mwanaume,sema mfumo dume ndo umetuharibu africa
 
Mimi si mwanaume ila naomba nikurekebishe mwanamke mwenzangu
"Mbali na uwajibikaji wa kutafuta pesa na mahitaji mengine kwa familia, lakini mwanamke ni mwanamke tu na ili awe mke ni lazima atimize majukumu yake kwa mumewe na familia kwa ujumla, pesa yaweza kua si lolote si chochote kwenye familia lakini upendo ni nguzo muhimu,na upendo huletwa na mwanamke msikivu, muwajibikaji, muelewa na mchapa kazi" lakini kamwe hauletwi na mwanamke mjuaji, mvivu na kisirani. TIMIZA WAJIBU WAKO
Asante mkuu
 
Kitanzania kuna majukumu ya kike na kiume labda uamue kuwa tofauti ni wewe tu.

Kama unataka kuwa na mme atakayekuoshea vyombo, kuchotea maji, kufulia nguo, kupikia, kumtuma sokoni wapo tu ni chaguo lako.

Mimi napenda mwanamke anayejua mipaka yake na mimi niilinde yangu.
Yap
Mwanamke hata km anafanya kazi lazima ajue wajibu wake kwa mume wake na familia.
Ila mm sipendi goli kipa
 
Ni shida tu tulizonazo watanzania tulio wengi, maana ilipaswa mwanamke akae nyumbani kumsubiria mume, kumfariji baada ya mahangaiko ya kutwa. Kumpikia vizuri, kumuandaa asubuhi, hata kumuohesha, mwanamke yapasa ujue kabisa kesho mume anatakiwa avaaje kuanzia chupi mpaka soksi, na tazama chanzo kikuu cha wanaume kutembea na wadada wa ndani, baba akila chakula kitamu anajua mhusika ni Dada, akivaa Nguo safi na kazini akisiwa hiyo shati umependeza anajua Dada kahusika, malezi ya mtoto Dada kahusika, mpaka wengine kitanda wanaandaa wadada, sasa malipo ya Dada ni nn unadhani, wakuu nimetanguliza kuwa sababu ya umaskini tu, lkn mwanamke ni pambo la ndani
 
Back
Top Bottom