Swali kwa wanaotaka UKAWA warudi bungeni

daniel merengo

JF-Expert Member
Joined
Aug 19, 2011
Posts
277
Reaction score
98
Kuna watu watu wengi wamekuwa wakisema UKAWA warudi kujadili serikali 2 kisha wananchi wataamua. swali kwao ni kwa nini hao walio bungeni wasikubali kujadili serikali 3 zilizopendekezwa na wananchi halafu wakati wa kupiga kura ukifika wananchi waamue wenyewe? kwani hao wanaokomaa ikajadiliwe serikali 2 wanaogopa nini kujadili serikali 3 halafu wananchi waamue?
 
Kazi ya BMK ni kujadili na kuamua namna ya KUTEKELEZA maoni ya wananchi.

Kuamua serikali 3 ziweje na sio kuyakataa.

Wananchi wanataka serikali 3.
 
Kuna watu watu wengi wamekuwa wakisema UKAWA warudi kujadili serikali 2 kisha wananchi wataamua. swali kwao ni kwa nini hao walio bungeni wasikubali kujadili serikali 3 zilizopendekezwa na wananchi halafu wakati wa kupiga kura ukifika wananchi waamue wenyewe? kwani hao wanaokomaa ikajadiliwe serikali 2 wanaogopa nini kujadili serikali 3 halafu wananchi waamue?

Wanachotakiwa ni kwenda kujadiliana pia ni kwa nini serikali tatu? Kwa nini zisiwe mbili au kwwa nini isiwe moja? waliotoa maoni ya serikali tatu ni watu 17,000 kati ya watu laki tatu waliohojiwa unadhani kwa hesabu hayo ya 17000 ambao ni maoni ambao ni asilimia sita tu ya watu waliotoa maoni kwenye rasmu ndiyo yachukuliwe kuwa ndio final? Jamani hata hesabu za kawaida tu haikubali.

HIvyo UKAWA warudi bungeni warumbane tani yao kuhusu serikali mbili,tatu,nne,moja au kuvunja muungano halafu watoke na jibu.Kukaa nje na kukataa kwenda kulumbana kwa hoja ni kukimbia hoja.Na katiba haiwezi patikana nje ya bunge hata siku moja.Ni delaying tactics.Inavyoelekea vyama vya siasa kuanzia chama tawala na UKAWA hawataki katiba mpya ipatikane kabla ya uchaguzi wa mwakani.Kila mmoja ana ajenda ya siri ambayo wananchi tunafichwa machoni wanaonekana kama wanagombana lakini ukweli ni kuwa wote hawataki katiba mpya ipatikane kabla ya uchaguzi.

Wanasiasa kama masingasinga wanajuana kwa vilemba.Wananchi tuendelee na shughuli zetu wanatupotezea muda na hela zetu tu hawa wanasiasa.
 
serikali tatu ni mhimili na msingi wa rasimu.. Bunge halina mamlaka ya kuondoa isipokuwa wananchi.. Bunge linatakiwa tu kujadili hizo serikali tatu ziwe za namna gani basiiiiiii.... Na syo serikali mbili.. Ambyo ni maoni ya baadhi ya viongozi wa ccm
 
Mkulima hahitaji serikali tatu anachotaka ni serikali moja itakayompa uhuru wa kumiliki ardhi na kulima popote na kuuza popote

Mfanyabiashara anachotaka ni serikali moja yenye sheria za biashara na kodi za aina moja na taratibu za aina moja zinazomwezesha kufanya biashara popote bila bughudha ya aina yoyote

Mfanyakazi angependa kuwe na serikali moja ambapo yuko huru kufanya kazi popote na kwa viwango sawia vya mishahara na marupurupu

Mvuvi angependa serikali moja inayomwezesha kuvua popote na kujiuzia popote

Kiongozi wa dini angependa serikali moja yenye sheria moja ambayo inamwezesha yeye kutangaza dini yake na kuabudisha popote bila vikwazo

Mwanafunzi angependa awe huru kusoma popote na kupata mkopo wa kusoma popote

Lakini wanasiasa ndio wanataka serikali tatu ili wawe na nyimbo zao,majeshi yao,balozi zao,na vyeo vyao vya kisiasa na mafungu yao ya kugawana mapato yatokanayo na kukamua kodi wanyonge

Wakili wa kujitegemea angependa serikali moja ya kumwezesha kufanya kazi zake popote bila vikwazo ndani ya nchi moja.

Mfugaji wa kuhama hama angependa serikali moja inayoruhusu yeye kujichungia mifugo yake popote penye malisho mazuri ya mifugo yake

Hivi hiyo tume ya Warioba ina uhakika kuwa wananchi ndio wanataka serikali tatu?

Mimi baada ya kuwahoji wanachi wa kawaida wengi wameruka kuwa hilo la serikali tatu anayelijua vizuri ni huyo warioba na tume yake na hao wanasiasa wa UKAWA.

Wataka serikali tatu wanaotoa hadi mapovu ni wanasiasa ambao wanaishi kwa kutegemea siasa tu na wanaofaidika na ulaji kodi za wananchi ila wanajaribu kutumia wananchi kama ngao ya ubaradhuli wao.

Chadema na CUF wanajua kuwa si rahisi wao kushika nchi ikiwa moja kwa sababu CUF ina nguvu sana Zanzibar lakini bara haina nguvu hivyo nchi ikiwa moja wanajua hawatapata kura bara na CHADEMA wanaona kukiwa na serikali moja watakwama kwa kuwa wana nguvu sana Tanzania bara lakini Zanzibar hawana nguvu hivyo kukitokea uchaguzi kukiwa na serikali moja wanajua watakwama. Hivyo makundi haya mawili ya CUF na CHADEMA yanapigania serikali tatu kwa kuota ndoto za Alnacha kuwa zikipatikana basi CUF itashika Zanzibar CHADEMA tashika BARA na CCM itaambulia hako kaserikali ka muungano kasikokuwa na NGUVU wala raslimali bali kanategemea michango ya washirika.

Ukweli ndio huo wanasiasa ndio wanataka serikali tatu na warioba akaona muhimu kuwasikiliza hao na akayaita eti ndio maoni ya wananchi sio kweli.

Katika vitu vya aibu ambavyo tume imefanya ni kuchukua maoni ya wanasiasa kuhusu serikali tatu na kuyaita maoni ya wananchi .Ni aibu kwa tume. Najisikia vibaya tume kwa hili imekula posho ZA KODI ZA WANANCHI bure kabisa.
 
Wanachotakiwa ni kwenda kujadiliana pia ni kwa nini serikali tatu? Kwa nini zisiwe mbili au kwwa nini isiwe moja? waliotoa maoni ya serikali tatu ni watu 17,000 kati ya watu laki tatu waliohojiwa unadhani kwa hesabu hayo ya 17000 ambao ni maoni ambao ni asilimia sita tu ya watu waliotoa maoni kwenye rasmu ndiyo yachukuliwe kuwa ndio final? Jamani hata hesabu za kawaida tu haikubali.

HIvyo UKAWA warudi bungeni warumbane tani yao kuhusu serikali mbili,tatu,nne,moja au kuvunja muungano halafu watoke na jibu.Kukaa nje na kukataa kwenda kulumbana kwa hoja ni kukimbia hoja.Na katiba haiwezi patikana nje ya bunge hata siku moja.Ni delaying tactics.Inavyoelekea vyama vya siasa kuanzia chama tawala na UKAWA hawataki katiba mpya ipatikane kabla ya uchaguzi wa mwakani.Kila mmoja ana ajenda ya siri ambayo wananchi tunafichwa machoni wanaonekana kama wanagombana lakini ukweli ni kuwa wote hawataki katiba mpya ipatikane kabla ya uchaguzi.

Wanasiasa kama masingasinga wanajuana kwa vilemba.Wananchi tuendelee na shughuli zetu wanatupotezea muda na hela zetu tu hawa wanasiasa.

Kwa hiyo hao wajumbe 600 wa BMK ni wengi kuliko wananchi 17,000! Hata wapima Ukimwi au Malaria kwenye damu huwa wanachukua vitone havizidi viwili na kati ya lita 4-5 za damu ya binaadamu, hawachukui lita nzima kama mnavyotaka? Ukiwa CCM lazima akili ifikiri kinyumenyume.
 
Hao 17,000 ni watu binafsi waliotoa maoni yao ambao hawakuchaguliwa wala kutumwa na yeyote kusema hicho walichosema.Bunge limebeba watu milioni 45.Hao waliomo humo ndani wanawakilisha hao milioni 45.Wako 600 lakini wamebeba nyuma yao wananchi milioni 45!

Hiyo rasimu kwa sasa ni private document kwa sababu kuanzia mwanzo hadi mwisho imejaa maoni ya watu binafsi sasa kuifanya iwe public document ndio hao 600 wawakilishi wa watu milioni 45 waenda ijadili na kupitisha ili iwe public document yenye sauti ndani za wale wanaowawakilisha.nASEMA HAO 600 waweza ona wadogo kwa namba lakini ni wengi kwa idadi kwani wamebeba umati wa mtume wakiwemo mashehe na viongozi wa dini,viongozi wa vyama,makundi n.k Lazima waipitie na kujadili.
 
Mkulima hahitaji serikali tatu anachotaka ni serikali moja itakayompa uhuru wa kumiliki ardhi na kulima popote na kuuza popote

Mfanyabiashara anachotaka ni serikali moja yenye sheria za biashara na kodi za aina moja na taratibu za aina moja zinazomwezesha kufanya biashara popote bila bughudha ya aina yoyote

Mfanyakazi angependa kuwe na serikali moja ambapo yuko huru kufanya kazi popote na kwa viwango sawia vya mishahara na marupurupu

Mvuvi angependa serikali moja inayomwezesha kuvua popote na kujiuzia popote

Kiongozi wa dini angependa serikali moja yenye sheria moja ambayo inamwezesha yeye kutangaza dini yake na kuabudisha popote bila vikwazo

Mwanafunzi angependa awe huru kusoma popote na kupata mkopo wa kusoma popote

Lakini wanasiasa ndio wanataka serikali tatu ili wawe na nyimbo zao,majeshi yao,balozi zao,na vyeo vyao vya kisiasa na mafungu yao ya kugawana mapato yatokanayo na kukamua kodi wanyonge

Wakili wa kujitegemea angependa serikali moja ya kumwezesha kufanya kazi zake popote bila vikwazo ndani ya nchi moja.

Mfugaji wa kuhama hama angependa serikali moja inayoruhusu yeye kujichungia mifugo yake popote penye malisho mazuri ya mifugo yake

Hivi hiyo tume ya Warioba ina uhakika kuwa wananchi ndio wanataka serikali tatu?

Mimi baada ya kuwahoji wanachi wa kawaida wengi wameruka kuwa hilo la serikali tatu anayelijua vizuri ni huyo warioba na tume yake na hao wanasiasa wa UKAWA.

Wataka serikali tatu wanaotoa hadi mapovu ni wanasiasa ambao wanaishi kwa kutegemea siasa tu na wanaofaidika na ulaji kodi za wananchi ila wanajaribu kutumia wananchi kama ngao ya ubaradhuli wao.

Chadema na CUF wanajua kuwa si rahisi wao kushika nchi ikiwa moja kwa sababu CUF ina nguvu sana Zanzibar lakini bara haina nguvu hivyo nchi ikiwa moja wanajua hawatapata kura bara na CHADEMA wanaona kukiwa na serikali moja watakwama kwa kuwa wana nguvu sana Tanzania bara lakini Zanzibar hawana nguvu hivyo kukitokea uchaguzi kukiwa na serikali moja wanajua watakwama. Hivyo makundi haya mawili ya CUF na CHADEMA yanapigania serikali tatu kwa kuota ndoto za Alnacha kuwa zikipatikana basi CUF itashika Zanzibar CHADEMA tashika BARA na CCM itaambulia hako kaserikali ka muungano kasikokuwa na NGUVU wala raslimali bali kanategemea michango ya washirika.

Ukweli ndio huo wanasiasa ndio wanataka serikali tatu na warioba akaona muhimu kuwasikiliza hao na akayaita eti ndio maoni ya wananchi sio kweli.

Katika vitu vya aibu ambavyo tume imefanya ni kuchukua maoni ya wanasiasa kuhusu serikali tatu na kuyaita maoni ya wananchi .Ni aibu kwa tume. Najisikia vibaya tume kwa hili imekula posho ZA KODI ZA WANANCHI bure kabisa.

Hiyo Ardhi unayoizungumzia ni ipi ambayo mkulima anaitaka kupitia Serikali Moja? Mbona hata hizi serikali mbili zilizopo hata Wazungu na Wachina wanamiliki ?
 
Ardhi ya Zanzibar kwamba mkulima wa Tanzania bara awe na haki ya kupata shamba na hati miliki ya shamba zanzibar kama ambavyo mkulima mzanzibari ana haki ya kupata shamba na hati miliki ya shamba tanzania bara.Kusiwe na sheria za ardhi tofauti.
 
Mkulima hahitaji serikali tatu anachotaka ni serikali moja itakayompa uhuru wa kumiliki ardhi na kulima popote na kuuza popote

Mfanyabiashara anachotaka ni serikali moja yenye sheria za biashara na kodi za aina moja na taratibu za aina moja zinazomwezesha kufanya biashara popote bila bughudha ya aina yoyote

Mfanyakazi angependa kuwe na serikali moja ambapo yuko huru kufanya kazi popote na kwa viwango sawia vya mishahara na marupurupu

Mvuvi angependa serikali moja inayomwezesha kuvua popote na kujiuzia popote

Kiongozi wa dini angependa serikali moja yenye sheria moja ambayo inamwezesha yeye kutangaza dini yake na kuabudisha popote bila vikwazo

Mwanafunzi angependa awe huru kusoma popote na kupata mkopo wa kusoma popote

Lakini wanasiasa ndio wanataka serikali tatu ili wawe na nyimbo zao,majeshi yao,balozi zao,na vyeo vyao vya kisiasa na mafungu yao ya kugawana mapato yatokanayo na kukamua kodi wanyonge

Wakili wa kujitegemea angependa serikali moja ya kumwezesha kufanya kazi zake popote bila vikwazo ndani ya nchi moja.

Mfugaji wa kuhama hama angependa serikali moja inayoruhusu yeye kujichungia mifugo yake popote penye malisho mazuri ya mifugo yake

Hivi hiyo tume ya Warioba ina uhakika kuwa wananchi ndio wanataka serikali tatu?

Mimi baada ya kuwahoji wanachi wa kawaida wengi wameruka kuwa hilo la serikali tatu anayelijua vizuri ni huyo warioba na tume yake na hao wanasiasa wa UKAWA.

Wataka serikali tatu wanaotoa hadi mapovu ni wanasiasa ambao wanaishi kwa kutegemea siasa tu na wanaofaidika na ulaji kodi za wananchi ila wanajaribu kutumia wananchi kama ngao ya ubaradhuli wao.

Chadema na CUF wanajua kuwa si rahisi wao kushika nchi ikiwa moja kwa sababu CUF ina nguvu sana Zanzibar lakini bara haina nguvu hivyo nchi ikiwa moja wanajua hawatapata kura bara na CHADEMA wanaona kukiwa na serikali moja watakwama kwa kuwa wana nguvu sana Tanzania bara lakini Zanzibar hawana nguvu hivyo kukitokea uchaguzi kukiwa na serikali moja wanajua watakwama. Hivyo makundi haya mawili ya CUF na CHADEMA yanapigania serikali tatu kwa kuota ndoto za Alnacha kuwa zikipatikana basi CUF itashika Zanzibar CHADEMA tashika BARA na CCM itaambulia hako kaserikali ka muungano kasikokuwa na NGUVU wala raslimali bali kanategemea michango ya washirika.

Ukweli ndio huo wanasiasa ndio wanataka serikali tatu na warioba akaona muhimu kuwasikiliza hao na akayaita eti ndio maoni ya wananchi sio kweli.

Katika vitu vya aibu ambavyo tume imefanya ni kuchukua maoni ya wanasiasa kuhusu serikali tatu na kuyaita maoni ya wananchi .Ni aibu kwa tume. Najisikia vibaya tume kwa hili imekula posho ZA KODI ZA WANANCHI bure kabisa.

Hao wote ulowataja wakulima wanafunzi wavuvi wafanyabiashara kwa mujibu wa maoni yaliyoratibiwa kitaalam na tume makini walitaka serikali tatu maoni ya kuja na serikali yameratibiwa na nani .? acha kukariri
 
Hao 17,000 ni watu binafsi waliotoa maoni yao ambao hawakuchaguliwa wala kutumwa na yeyote kusema hicho walichosema.Bunge limebeba watu milioni 45.Hao waliomo humo ndani wanawakilisha hao milioni 45.Wako 600 lakini wamebeba nyuma yao wananchi milioni 45!

Hiyo rasimu kwa sasa ni private document kwa sababu kuanzia mwanzo hadi mwisho imejaa maoni ya watu binafsi sasa kuifanya iwe public document ndio hao 600 wawakilishi wa watu milioni 45 waenda ijadili na kupitisha ili iwe public document yenye sauti ndani za wale wanaowawakilisha.nASEMA HAO 600 waweza ona wadogo kwa namba lakini ni wengi kwa idadi kwani wamebeba umati wa mtume wakiwemo mashehe na viongozi wa dini,viongozi wa vyama,makundi n.k Lazima waipitie na kujadili.

Nina wasiwasi na uelewa wako tume hawakuwa wajinga kiasi hicho wao walijikita kwenye hoja na sio idadi ya watoa maoni kumbuka ukitaka kujikita kwenye takwimu unapaswa kupigia kura tume hawakuendesha zoezi la kupiga kura bali waliangalia uzito wa hoja na kama ukitaka kuangalia takwimu mwenyekiti wako wa chama amejipachika tu kwenye urais kwani watu mil tano walompigiakura hawatoshi ukilinganisha na watanzania mil 45
 
Nyongeza ni kuwa hii ilikuwa qualitative research na siyo quantitative kama wanaouliza idadi wanavyofikiri.Unapofanya qualitative research kuna point of saturation inafikiwa ukiwa field inakuwa hupati tena majibu mapya kwa topic inayoongelewa i.e kila mtu anajibu hivyohivyo- majibu ya mtoa hoja wa Mtwara na alie Shinyanga, Arusha etc at that point yanafanana ingawa hawakukaa pamoja.
 
Kama ni quality iliyozingatiwa hivi hoja ya serkali moja ambayo walikiri kuwa waliipokea kwao ilikuwa haina quality kuliko ya serikali tatu waliyopendekeza? Hivi kipi hapo kiko kwenye kiwango cha quality hata ukikipeleka kwa wananchi ukitaka wakipigie kura ni serikali moja au tatu?
 
Wanachotakiwa ni kwenda kujadiliana pia ni kwa nini serikali tatu? Kwa nini zisiwe mbili au kwwa nini isiwe moja? waliotoa maoni ya serikali tatu ni watu 17,000 kati ya watu laki tatu waliohojiwa unadhani kwa hesabu hayo ya 17000 ambao ni maoni ambao ni asilimia sita tu ya watu waliotoa maoni kwenye rasmu ndiyo yachukuliwe kuwa ndio final? Jamani hata hesabu za kawaida tu haikubali.

HIvyo UKAWA warudi bungeni warumbane tani yao kuhusu serikali mbili,tatu,nne,moja au kuvunja muungano halafu watoke na jibu.Kukaa nje na kukataa kwenda kulumbana kwa hoja ni kukimbia hoja.Na katiba haiwezi patikana nje ya bunge hata siku moja.Ni delaying tactics.Inavyoelekea vyama vya siasa kuanzia chama tawala na UKAWA hawataki katiba mpya ipatikane kabla ya uchaguzi wa mwakani.Kila mmoja ana ajenda ya siri ambayo wananchi tunafichwa machoni wanaonekana kama wanagombana lakini ukweli ni kuwa wote hawataki katiba mpya ipatikane kabla ya uchaguzi.

Wanasiasa kama masingasinga wanajuana kwa vilemba.Wananchi tuendelee na shughuli zetu wanatupotezea muda na hela zetu tu hawa wanasiasa.

hoja ya selikali 2 kwa takwimu zipi?
 
Kama ni quality iliyozingatiwa hivi hoja ya serkali moja ambayo walikiri kuwa waliipokea kwao ilikuwa haina quality kuliko ya serikali tatu waliyopendekeza? Hivi kipi hapo kiko kwenye kiwango cha quality hata ukikipeleka kwa wananchi ukitaka wakipigie kura ni serikali moja au tatu?

Hapo logic ndio ilizingatiwa:Ukiangalia uwezekano wa Wazanzibari kubadili katiba na kujivua hadhi (nchi)waliyojivika ndani ya muungano ni ngumu kuliko kuitambua status ya Tanganyika kama nchi ndani ya muungano.Kuna vitu ambavyo si wingi wa watu huamua ila hekima na logic.Hilo wamelikosa wabunge wengi wa chama chetu ndio maana wanajiita maoni ya walio wengi wakati wakijua kabisa wanachosimamia maslahi ya wachache-msimamo kikundi kidogo ndani ya chama.
Kifupi ni kuwa approach ya tume ya mzee Warioba ikizingatiwa iliundwa na wajumbe wenye itikadi tofauti ilikuwa ya logic na consensus na sio wingi. Sita angeitumia bungeni katiba ingekuwa tayari tusingekuwa hapa. Tutaumiss sana unyenyekevu wa kificho katika kudeal na issues.
 
Nashangaa sana, kama elfu 17,000 waliotoa maoni ya serikali tatu ni wachache sana. Je wabunge wa ccm na washirika wao walioko bungeni hawazidi 500. wao wankuaje wengi kuwaamulia watanzani serikali 2. je 17,000 na 500 wepi wengi????
 
Kuna watu watu wengi wamekuwa wakisema UKAWA warudi kujadili serikali 2 kisha wananchi wataamua. swali kwao ni kwa nini hao walio bungeni wasikubali kujadili serikali 3 zilizopendekezwa na wananchi halafu wakati wa kupiga kura ukifika wananchi waamue wenyewe? kwani hao wanaokomaa ikajadiliwe serikali 2 wanaogopa nini kujadili serikali 3 halafu wananchi waamue?
Fumbo mfumbie mjinga, Mwerevu ..............................
 
Wanachotakiwa ni kwenda kujadiliana pia ni kwa nini serikali tatu? Kwa nini zisiwe mbili au kwwa nini isiwe moja? waliotoa maoni ya serikali tatu ni watu 17,000 kati ya watu laki tatu waliohojiwa unadhani kwa hesabu hayo ya 17000 ambao ni maoni ambao ni asilimia sita tu ya watu waliotoa maoni kwenye rasmu ndiyo yachukuliwe kuwa ndio final? Jamani hata hesabu za kawaida tu haikubali.

HIvyo UKAWA warudi bungeni warumbane tani yao kuhusu serikali mbili,tatu,nne,moja au kuvunja muungano halafu watoke na jibu.Kukaa nje na kukataa kwenda kulumbana kwa hoja ni kukimbia hoja.Na katiba haiwezi patikana nje ya bunge hata siku moja.Ni delaying tactics.Inavyoelekea vyama vya siasa kuanzia chama tawala na UKAWA hawataki katiba mpya ipatikane kabla ya uchaguzi wa mwakani.Kila mmoja ana ajenda ya siri ambayo wananchi tunafichwa machoni wanaonekana kama wanagombana lakini ukweli ni kuwa wote hawataki katiba mpya ipatikane kabla ya uchaguzi.

Wanasiasa kama masingasinga wanajuana kwa vilemba.Wananchi tuendelee na shughuli zetu wanatupotezea muda na hela zetu tu hawa wanasiasa.

Hizi ni hoja mufilisi za watu waliochoka kufikiri na wanaotaka kulazimisha mambo. hivi mnavyosema kwamba waliotoa maoni ya serikali 3 ni wachache ,Je rais kikwete alichaguliwa na watanzania wangapi? mbona hili hamjalihoji hata siku moja?
1) naomba uniambie rais kikwete alichaguliwa kuwa rais 2010 na wapiga wangapi kati ya waliojiandikisha kupiga kura?
baada ya hapo utuambie uhalali wake kuwa rais kwa sababu alipata kura mil 5 kati ya wapiga kura mil 19
2) utuambie ni katika mkoa gani alipata kura nyingi kuliko mikoa mingine? kisha utuambie uhalali wake kuwa rais kwa sababu alipata kura nyingi toka mkoa huo utakaotuambia? ninakuuliza haya maswali kwa sababu ya siasa nyepesi zinazofanywa na watu wa aina yako

Kama kweli watu wanajiamini na wanajua maoni ya serikali 3 ni maoni ya warioba na sio ya wananchi ni KWA NINI MSIKUBALI KUJADILI SERIKALI 3 HALAFU WANANCHI WATAAMUA?

Vile vile hizo serikali mbili mnazojadili bungeni haya maoni mliyakusanya lini? kutoka kwa nani? na kwa sheria ipi? kupitia tume ipi?

Na ninachokisema kwamba wanaokataa rasimu ya warioba hawana hoja ni kutokana na kitendo cha SAMWELI SITTA kutaka ITV ifungiwe kisa wamerusha mdahalo ulioongozwa na wajumbe wa tume. na mkasahau kwamba UDASA,TBC,STAR TV,na chama cha serikali 2 waliandaa mdahalo kabla ya huu wa tume na wajumbe wake. mbona sitta hajaituhumu star tv,tbc kwa kurusha mdahalo wa chama chako?

WALIOZOEA VYA KUNYONGA HAWAWEZI VYA KUCHINJA
 
Mkulima hahitaji serikali tatu anachotaka ni serikali moja itakayompa uhuru wa kumiliki ardhi na kulima popote na kuuza popote

Mfanyabiashara anachotaka ni serikali moja yenye sheria za biashara na kodi za aina moja na taratibu za aina moja zinazomwezesha kufanya biashara popote bila bughudha ya aina yoyote

Mfanyakazi angependa kuwe na serikali moja ambapo yuko huru kufanya kazi popote na kwa viwango sawia vya mishahara na marupurupu

Mvuvi angependa serikali moja inayomwezesha kuvua popote na kujiuzia popote

Kiongozi wa dini angependa serikali moja yenye sheria moja ambayo inamwezesha yeye kutangaza dini yake na kuabudisha popote bila vikwazo

Mwanafunzi angependa awe huru kusoma popote na kupata mkopo wa kusoma popote

Lakini wanasiasa ndio wanataka serikali tatu ili wawe na nyimbo zao,majeshi yao,balozi zao,na vyeo vyao vya kisiasa na mafungu yao ya kugawana mapato yatokanayo na kukamua kodi wanyonge

Wakili wa kujitegemea angependa serikali moja ya kumwezesha kufanya kazi zake popote bila vikwazo ndani ya nchi moja.

Mfugaji wa kuhama hama angependa serikali moja inayoruhusu yeye kujichungia mifugo yake popote penye malisho mazuri ya mifugo yake

Hivi hiyo tume ya Warioba ina uhakika kuwa wananchi ndio wanataka serikali tatu?

Mimi baada ya kuwahoji wanachi wa kawaida wengi wameruka kuwa hilo la serikali tatu anayelijua vizuri ni huyo warioba na tume yake na hao wanasiasa wa UKAWA.

Wataka serikali tatu wanaotoa hadi mapovu ni wanasiasa ambao wanaishi kwa kutegemea siasa tu na wanaofaidika na ulaji kodi za wananchi ila wanajaribu kutumia wananchi kama ngao ya ubaradhuli wao.

Chadema na CUF wanajua kuwa si rahisi wao kushika nchi ikiwa moja kwa sababu CUF ina nguvu sana Zanzibar lakini bara haina nguvu hivyo nchi ikiwa moja wanajua hawatapata kura bara na CHADEMA wanaona kukiwa na serikali moja watakwama kwa kuwa wana nguvu sana Tanzania bara lakini Zanzibar hawana nguvu hivyo kukitokea uchaguzi kukiwa na serikali moja wanajua watakwama. Hivyo makundi haya mawili ya CUF na CHADEMA yanapigania serikali tatu kwa kuota ndoto za Alnacha kuwa zikipatikana basi CUF itashika Zanzibar CHADEMA tashika BARA na CCM itaambulia hako kaserikali ka muungano kasikokuwa na NGUVU wala raslimali bali kanategemea michango ya washirika.

Ukweli ndio huo wanasiasa ndio wanataka serikali tatu na warioba akaona muhimu kuwasikiliza hao na akayaita eti ndio maoni ya wananchi sio kweli.

Katika vitu vya aibu ambavyo tume imefanya ni kuchukua maoni ya wanasiasa kuhusu serikali tatu na kuyaita maoni ya wananchi .Ni aibu kwa tume. Najisikia vibaya tume kwa hili imekula posho ZA KODI ZA WANANCHI bure kabisa.

wewe ndio wale wale. hao wananchi uliwahoji kama nani? wewe uko kwenye tume ipi? na ni sheria gani inakuongoza kuwahoji wananchi?
 
Back
Top Bottom