Swali kwa walioolewa

Swali kwa walioolewa

Kasongo

JF-Expert Member
Joined
Jul 29, 2007
Posts
3,149
Reaction score
2,273
Nyie akina dada/mama mlioolewa hivi kuna haja sana ya kujipodoa kama mabinti ambao hawajaolewa.Sisemi msiwe nadhifu lakini mimi huwa namchallenge mke wangu anapokuwa anahangaika kwenda saloon.

Kuhangaika na kioo chumbani asubuhi akijiandaa kwenda kwenye shughuli zake.Huwa namwambia mimi nakupenda hata usipovaa hizo nywele bandia na madoido mengine,sasa hayo unayoweka unataka nani akuone tena huko nje.

Urembo kwa wanawake huwa ni kwa ajili ya kumfurahisha/kumvutia nani.Wanawake wenzenu au wanaume.Huwa ananijibu eti asipofanya hivyo mimi nitaona wengine waliofanya hivyo watanivutia.Hii ni kweli.
 
Anajiremba kwa ajili ya nafsi yake,halafu umemkuta mtu asili yake kujiremba na kujipamba kwa kuwa tu umemuoa ndio aache, ni sawa na kuolewa na mwanaume mlevi halafu utegemee aache kwa sababu tu ameoa
 
Kujiremba si kwa ajili ya mwanaume ni kwa ajli ya confidence mbele ya jamii utajisikiaje unasikia jamii inakwambia mke wa Kasongo yupo rafu na naamini kilichokuvutia kwake ni mwonekano wake pamoja na kuwa smart kujiremba ni jambo nzuri kwa mwanamke elimradi tu asijirembe akawa kama kipupe.
 
ananijibu eti asipofanya hivyo mimi nitaona wengine waliofanya hivyo watanivutia.!Hii ni kweli?

Je ni kweli kwa sasa ukiona wengine hawakuvutii,kama ni kweli acha aendelee,kama sikweli wanakuvutia basi aongeze kujikwatua zaidi.
 
Ulimkuta anajiremba leo unataka aache kwa nini? Kama ulimpenda akiwa amejiremba si utamwacha akiacha
 
tunajiremba ili tupendezeee na heshima katika jamii, ila isiwe to much.
 
Vitu ambavyo tangu zamani tukiwa ma best friends na mke wangu alikuwa anatambua sivifurahii ni;

1. Kucha bandia.
2. Tattoo.
3. Nywele bandia(ila anaweza kuweka tu kwa some cases maana wanawake kudeal na nywele zao ni challenge.
4. Kope bandia.
5. Lipstick kama tunataka kugombana.

Mke wangu anajua nini napenda toka kwake. Sometimes anajipamba ila akikumbuka heshma yake kwangu na jamii kiujumla.

Akijipamba anapendeza kimuonekano wa nje ingawa nampendea zaidi ndani(nafsi yake yeye mwenyewe.
 
Kujipamba ili apendeze zaidi ni muhim sana, ndio maana wanaume wengine hutoka nje kwa kisingizio kuwa tangia amuoe mkewe kajiachia wala hajijal tena kama mwanzo.
Huo ni wivu wa kisirisiri unahis akipendeze utaibiwa bure so Acha hizo.
 
mke ni pambo ndani ya nyumba...na pambo si bora pambo tu...pambo lina vigezo vyake kulingana na kila mtu...lkn lazima liwe zuri
 
Ila hata mie hayo mapambo mapambo siyataki.Eti akaomba atoboe pua huh! nikamwambia futa No yng ukifanya hivo,akaogopa na hakutoboa.Baki ulivo mama nakupenda hivohivo.
 
Nyie akina dada/mama mlioolewa hivi kuna haja sana ya kujipodoa kama mabinti ambao hawajaolewa.Sisemi msiwe nadhifu lakini mimi huwa namchallenge mke wangu anapokuwa anahangaika kwenda saloon.

Kuhangaika na kioo chumbani asubuhi akijiandaa kwenda kwenye shughuli zake.Huwa namwambia mimi nakupenda hata usipovaa hizo nywele bandia na madoido mengine,sasa hayo unayoweka unataka nani akuone tena huko nje.

Urembo kwa wanawake huwa ni kwa ajili ya kumfurahisha/kumvutia nani.Wanawake wenzenu au wanaume.Huwa ananijibu eti asipofanya hivyo mimi nitaona wengine waliofanya hivyo watanivutia.Hii ni kweli.
Kuna msemo unaosema "miruzi mingi humpoteza mbwa"
Kiukweli tunawafadhaisha muno wadada/wamama mpaka wanashindwa kuelewa
ni nini haswa wanaume tunapenda.
Humu jf mara nyingi zimewekwa mada zinazohusu wanawake kujisahau pindi wanapoolewa,
wakijitahidi kujiweka vizuri,tunawauliza unapendeza kwa ajili ya nani.
Ngoja niseme hivi wanaume wenye wivu jitahidini kubadilika,mke wako hata asipojiremba
vicheche wakimtaka watamchukua.
Tuwape uhuru wake zetu kama sisi wanavyotuacha huru
kila mmoja azingatie wajibu wa kujilinda akijua afya
yake si yake tu bali inamhusu na mwenzi wake.
 
Mke kujiremba kwa minajili ya kuionesha jamii yake kiukweli haiko njema muhimu afanye hayo kwaajili ya mumewe tu na kama mume hayataki hayo mambo vema mke ukatii lakin tukumbuke kuna tofauti kubwa kati ya kujiremba na kuwa nadhifu. Unaweza kuwa nadhifu bila hata kujipodoa hususan kwa arficial things.
 
Nimeipenda hii
Kuna msemo unaosema "miruzi mingi humpoteza mbwa"Kiukweli tunawafadhaisha muno wadada/wamama mpaka wanashindwa kuelewa ni nini haswa wanaume tunapenda.Humu jf mara nyingi zimewekwa mada zinazohusu wanawake kujisahau pindi wanapoolewa,wakijitahidi kujiweka vizuri,tunawauliza unapendeza kwa ajili ya nani.Ngoja niseme hivi wanaume wenye wivu jitahidini kubadilika,mke wako hata asipojirembavicheche wakimtaka watamchukua.Tuwape uhuru wake zetu kama sisi wanavyotuacha hurukila mmoja azingatie wajibu wa kujilinda akijua afya yake si yake tu bali inamhusu na mwenzi wake.
 
Kuna msemo unaosema "miruzi mingi humpoteza mbwa"
Kiukweli tunawafadhaisha muno wadada/wamama mpaka wanashindwa kuelewa
ni nini haswa wanaume tunapenda.
Humu jf mara nyingi zimewekwa mada zinazohusu wanawake kujisahau pindi wanapoolewa,
wakijitahidi kujiweka vizuri,tunawauliza unapendeza kwa ajili ya nani.
Ngoja niseme hivi wanaume wenye wivu jitahidini kubadilika,mke wako hata asipojiremba
vicheche wakimtaka watamchukua.
Tuwape uhuru wake zetu kama sisi wanavyotuacha huru
kila mmoja azingatie wajibu wa kujilinda akijua afya
yake si yake tu bali inamhusu na mwenzi wake.

umenifurahisha mno
 
Aisee..... unakunywa kinywaji gani???

Nitalipa...
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom