Nape anahusika vipi na mambo yanayotakiwa kushughulikiwa na serikali.
Nape anahusika vipi na mambo yanayotakiwa kushughulikiwa na serikali.
Teh teh... hahusiki ila kufukuza wafanyakazi wa serikali wasiotaka kuhudhuria vikao vyao anahusika
mhh uvuvi wa kuwaza ndio nini we gamba?acha uvuvi wa kuwaza
acha uvuvi wa kuwaza
Nape anahusika vipi na mambo yanayotakiwa kushughulikiwa na serikali.
Bila kushirikisha ubongo ukakurupuka kujibu hivi....Teh teh... hahusiki ila kufukuza wafanyakazi wa serikali wasiotaka kuhudhuria vikao vyao anahusika
Sasa naomba ujibu haya hapa yaliyoandikwa kwenye Mtanzania na hadi sasa Nape wako hajakanusha, kisha jipime wewe na mimi nani mvuvi wa kufikiri..acha uvuvi wa kuwaza
CCM yabuni mbinu mpya
CHAMA Cha Mapinduzi (CCM), kimesema kuanzia sasa, kitawashughulikia watendaji wa Serikali wanaoitwa katika vikao mbalimbali vya chama hicho, kuelezea utekelezaji wa ilani ya chama hicho, lakini wanagoma kuhudhuria na wakati mwingine kuamua kutuma wasaidizi wao.
Kauli hiyo ilitolewa mjini hapa jana na Katibu wa Idara ya Itikadi na Uenezi ya CCM Taifa, Nape Nnauye, wakati akifungua semina ya Halmashauri Kuu ya Wilaya ya Nyamagana, Mkoa wa Mwanza.
Alisema kwamba, baadhi ya watendaji hao wamegeuka kuwa miungu watu katika sehemu zao za kazi na wamekuwa wakikaidi kuitikia wito wanapoitwa na viongozi wa chama katika ngazi za utawala.
"Kama kuna mtendaji ambaye anakichukia chama kinachounda Serikali anayoitumikia kisa tu chama kinafuatilia utekelezaji wa ilani yake, anapaswa kutupisha.
"Kwa hili hatutanii, tutamtimua kazi mara moja na nyie viongozi wa CCM mnapaswa kumjadili katika vikao vyenu na pale mtakapotuletea kuwa kiongozi fulani ni mzigo kwa chama, hatutaweza kuchukua zaidi ya dakika tatu kubariki uamuzi wa vikao vyenu ili iwe fundisho kwa watendaji.
Nape anahusika vipi na mambo yanayotakiwa kushughulikiwa na serikali.